Leslie Mbena
JF-Expert Member
- Nov 24, 2019
- 207
- 677
MDAU WA DIASPORA AJIBU MASWALI KUHUSU DARAJA LITALOJENGWA KUTOKA DAR HADI ZANZIBAR.
Leo 19:15pm,28/12/2019
Kutokana na Mgongangano wa mawazo ili Watanzania tufikie lengo kuu lenye kuleta tija,Mdau wa Diaspora amejibu maswali kiufasaha kuhusu ujenzi wa daraja kutoka Dar hadi Zanzibar ili wadau waelewe nini hasa kimewapelekea kuomba ruhusu kwa Serikali ili waweze kujenga daraja hilo.
Mdau huyo akielezea hayo amesema tayari wana miradi saba kwa jumla ambayo wameazimia kuiwakilisha kuanzia mwaka ujao na yote imepitishwa katika azimio la utekelezaji.
Kiuhalisia daraja kutoka Dar hadi Zanzibar likijengwa litaingia kwenye Guinness book kama daraja refu kabisa linaloelea baharini kwa lugha ya beberu "the longest floating bridge" kwa sasa daraja refu kabisa lina 2km hili la Dar hadi Zanzibar litakuwa na 30km.
Tashwishi ni kubwa na maswali ni mengi kuliko majibu, na muda ni mchache na Watanzania waishio nje wameamua kujenga daraja hilo kuunga mkono juhudi za Rais Mzalendo kabisa,Daktari John Pombe Magufuli.
Swali la msingi kutoka kwa Mwananchi wa Tanzania aliyetaka kujua zaidi kuhusu ujenzi wa daraja hilo,ni kwamba ninyi Watanzania mnaoishi nje ya Nchi mnawezaje kwenda kuomba hela kwa wafadhili kuja kutekeleza suala kubwa kama hili ambalo ni kazi ya serikali na ninavyodhani serikali ingeomba fund za kutekeleza huu mradi nadhani ingekuwa ni rahisi zaidi kuliko nyie kama diaspora,kumbuka huu ni mradi mkubwa sana,ni hilo tu napenda kujibiwa,Ahsante.
Jibu langu la msingi ni hili,Sisi watanzania tunaoishi nje ya Tanzania, Diaspora tumekuja na wazo na kuiomba serikali itupe ruhusa ya kufanya utafiti ili majibu yake yatatupa gharama za ujenzi.Katika ujenzi kuna mbinu mbili ambazo zinaweza kutumika ambayo ni PPP hii anaweza hata Bakhresa kuingiza pesa na ingine ni maataasisi kama worldbank na mengineyo.
Kwa maelezo haya toka mwanzo watu hawataki kuelewa na kuanza kupindisha story.Hakuna mwanadiaspora atakaechangishwa hata buku.
Sasa wakejeli wasikejeli serikali ikiruhusu tu watu wajiandae kupiga Selfie kwenye Daraja.Haya ndio maelezo ya mwisho.
Mdau mwingine akauliza hivi,kuna tofauti ya tunnel na floating bridge.
19km bridge iliyojengwa na Russians na kuzinduliwa mwaka huu imegharimu dola 3.6bn sasa daraja kutoka Dar hadi Zanzibar ni 30km halafu ni floating na pia litapita juu, sasa hapo kuna njia za meli zitazibwa... naomba nipate official tamko kuhusu ujenzi wa daraja la Zanzibar to Dar kama ni la ukweli.
Jibu langu ni hili,katika kila ujenzi unatofautiana na Teknologi,kuna za bei ndogo na kubwa sasa kwa upande wa daraja la znz-dar majibu ya gharama yatapatikana baada ya upembuzi yakinifu.Daraja la Russia wao walitumia Teknologi ya Russia na hili tunatarajia kutumia teknoloji ya Nchi ingine.Katika swala la jinsi gani meli zitapita hili ni jambo jepesi sana kwani uwezekano upo na mfano ni kama huu katika picha hapo chini.
-Umuhimu wa daraja litalotoka Dar - Zanzibar.
Ni daraja ambalo lilitakiwa kujengwa siku nyingi hasa kwa sababu Zanzibar ni kituo kivutio kikubwa cha utalii duniani. Watalii wengi wanaishia Dar kwa sababu ya adha ya usafiri wa kuvuka kwenda Zanzibar.
Usafiri uliopo sasa ni wa boti ambao una mapungufu yafuatayo:
1. Wakati mwingine inabidi uwahi tiketi siku moja kabla.
2. Msongamano wa watu kwenye kupanda boti unafanya muda kamili wa safari kuwa ni zaidi ya masaa matatu.
3. Ratiba ni ya mchana tu. Chukulia uko Dar unataka kwenda Zanzibar saa kumi na mbili jioni unafanyaje? Au unataka kuanza safari saa tano kamili, muda ambao hakuna ratiba ya boti.
4. Usafiri wa vyombo vya abiria haupendelewi sana na watalii.
5. Boti za abiria hazibebi mizigo mingi.
Daraja linaondoa matatizo yote hayo. Mtalii anaweza kulala Double Tree Dar, saa nne na nusu akavuka daraja, saa tano yuko Zanzibar, akapiga picha zake saa tatu usiku akavuka daraja kurudi hotelini kwake Double Tree Dar.
Njia ya baiskeli ni kivutio kikubwa sana cha watalii. Wanaweza hata kufanya mashindano ya kuendesha baiskeli.
Daraja linaweza hata kuitwa daraja la muungano. Kwa sababu ni kiungo kinachounganisha bara na visiwani.
Ieleweke boti zinazovuka sasa hivi ni za binafsi. Siku moja kampuni ikisimamisha huduma kwa sababu yeyote ile usafiri utarudi kuwa ni wa vidau au ile meli kubwa ya zamani ya masaa sita kufika Zanzibar.
Nikiishia hapa,Mimi ni,
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854