Mdau LiverpoolFC Apata Msiba

Mdau LiverpoolFC Apata Msiba

PakaJimmy

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2009
Posts
16,202
Reaction score
8,781
Wadau,

Nasikitika kuwatangazieni nyote kuwa mwenzetu LiverpoolFC amefiwa na Baba-Mkwe wake hapo jana, na muda huu ndio yupo kwenye maandalizi ya safari kuelekea huko jirani na Ngorongoro kwa shughuli za maandalizi ya mazishi.

Kwa harakaharaka amenijuza kuwa huenda mazishi yakafanyika kati ya Alhamis au Ijumaa hii.

Pia amenieleza kuwa chanzo cha kifo cha huyo baba ni ajali ya baiskeli, ambapo vijana wawili waliokuwa wamepakizana kwenye mteremko walimparamia na bike yao, wakimwangusha chini ambapo alipigiza kichwa kwenye lami.

Juhudi za kumwahisha Hospitali hazikuzaa matunda, maana alifariki kabla ya huduma yoyote.

Mungu ailaze roho ya arehemu mahala pema peponi.
Pole sana LiverpoolFC kwa maswahibu hayo na tuko pamoja na wewe.

Habari hizi ziwafikie: Mtambuzi Jiwe Linaloishi, Madame B Arushaone Mzee wa Rula Preta lily Flower Dark City Filipo Blaki Womani Tonykp Cantalisia IGWE Yericko Nyerere Chasha 'Valentina' kisukari Lady doctor Mchaka Mchaka sweetlady Malila
Na wanajamvi wote wanaohusika na msiba huu
 
Pole sana mkuu LiverpoolFC........Mungu ana kila sababu kwa kila kitu...........
 
Last edited by a moderator:
Pole sana Mpwa wangu, Duh kiburudisho kimefiwa na Mzazi? Hii hatari, pole sana sana na MUNGU awabariki
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom