Tatizo la chama cha Mapinduzi ni kuwaachia viongozi wake kujenga ufalme [Empire] ndani ya wigo wa kila mmoja kwa ngazi yake [Watanzania wanasema kila mbuzi atakula kwa ulefu wa kamba yake]
CCM kazi kwelikweli,wakati mwingine inaniwia vigumu nashindwa kuamini inakuwaje chama kikongwe kama CCM kinashindwa kuwa na Wataalamu wake wasiojua usingizi kwa siku kadha wa kadha kuwaza na kufilkilia kiuhalisia [Reality] wananch kwa sasa wanataka nini na nini kifanyike na kwa wakati gani na nani wa kukifanya ili kupunguza mtafaruku dhidi yake na umma.
Kwa usalama wa chama hicho kikongwe na muhimu kwa Nchi kwa kuwa kimekua na dhamana ya KIUTAWALA WA TAIFA HILI kwa miongo kadha wa kadha.Si vyema kikawa ni sehemu ya kuibua mtafaruku wa kusambalatika kwa TAIFA kwa kuwa dhambi hiyo kwao itakuwa kubwa sana.
Japo ni sahihi chama hiki kikatambua kuwa ni asilia [Nature] na hata kisayansi imethibitika kuwa hata biashara upitia mzunguko CYCLE,yanii kuanza kukomaa na kisha kuzeeka,kwa misingi ya kuwa biiashara hiyo yaitaji kuzaliwa upya.TANU NA ASP ni mwanzo wa kizazi kipya cha TANU miaka hiyo.
Kujivua gamba sijui ndio ubunifu mpya wa CCM mpya,na kama ndio picha ya uji mpya wa CCM mpya basi CCM bado ina kazi kubwa sana.Kujivua gamba ambako wengi tunakuona kwa kauri mbiu ya kuwaondoa mafisadi ndani ya CCM.Lakini kumbe kuna mafisadi wa matendo na kauri dhidi ya Wananchi wa Taifa hili.
Hakuna wakati huwa nawasihi CCM kutambua kuwa ili jamii ikubali japo kuwasikiliza kwa uchache ni kuwa na WATU wenye kauri njema na za unyenyekevu usio wa kinafiki na kauri za kejeri kama za waheshimiwa walio wengi ndani ya chama hicho.Kauri Jeuri na kupitiwa na kiburi cha kimadalaka ya kushindwa kutambua kuwa vyeo vyao ni dhamana limekuwa ni ugonjwa kwa Viongozi wengi wa CCM.Wengi wa viongozi hao wamekuwa na ulevi wa kimadaraka [AuthoritativeOpium].Wakijijenga na kuamini wao wamezaliwa daima kuwa viongozi wa kutawala Watanzania,wanajisau kiasi kuwa wengine wanageuka kuwa na damu ya kifalme [Royal blood] ya kuwafanya wengine si chochote katika ujenzi wa Taifa hili.
Alichoonesha Ndugai ni ugonjwa ambao ndio ufisadi mwingine wa Viongozi wa CCM,wamefika sehemu wamejiona wao ni raia namba moja [First Citizen] na wengine wapo kuwahudumia raia wa daraja la kwanza.
Kwa walio makini unamuona Kiongozi hata macho yake na mwili wake unavyozungumza body language [kwa hili Mwalimu alisema unamwangalia machoni unajiuliza huyu nae kweli?].Ndip CCM inakazi ya kuanza kutafuta na kuchambua kwa kiwango cha kasi kubwa kuakisha kuwa kinakuwa na watu walio makini na wenye uwezo wa kusoma nyakati katika kujibu majibu ya Wananchi na si kuzalisha kejeri na kiburi cha madaraka.
Viongozi wote WALIO NDANI YA CCM KIMADALAKA wenye haiba ya UJIVUNI,KEJERI,UKOLOFI,UONGO,USANII,WASIO WAVUMILIVU KWA KAURI, WADANGANYIFU, MATAPELI, WAZUSHI, WACHOYO NA WASIO NA VSION ZA NYAKATI,WANYIMWE DHAMANA YA KUONGEA NA VYOMBO VYA HABARI KAMA MAGAZETI,TELEVISHENINA RADIO [PUBLIC MEDIA] KUEPUSHA WALOPOKAJI.
BADO CCM NI CHAMA MUHIMU CHA KULIVUSHA TAIFA KWENYE KIPINDI HIKI CHA UJIO WA KIZAZI KIPYA CHA JAMII YENYE UELEWA TOFAUTI WA SIASA ZA TANZANIA.JAPO KUFA NI LAZIMA,VINGINEVYO NI VYEMA CCM KUTAFUTA JAWABU KWA KUIBADILISHA CCM KIITIKADI NA KUTOA TAFSIRI MPYA YA ITIKADI YAKE NA HATA JINA JIPYA LA CHAMA HICHO.