Mdahalo - Slaa Vs Sita ruksa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mdahalo - Slaa Vs Sita ruksa

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Nyambala, Sep 18, 2010.

 1. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #1
  Sep 18, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Dk. Slaa, Sitta kuvaana ruksa - Makamba


  na Irene Mark


  KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yusuf Makamba, amerudia kauli yake inayowazuia wagombea wa nafasi mbalimbali ndani ya chama hicho kushiriki kwenye midahalo aliyodai kushirikisha wenye njaa.
  Pamoja na zuio hilo, Makamba ametoa ruhusa kuwepo kwa mdahalo kati ya Spika wa Bunge, Samuel Sitta (CCM) na mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa.
  Alisema hayo mjini Dar es Salaam jana alipokutana na waandishi wa habari ofisini kwake na kuwaeleza msimamo wa chama hicho kutoruhusu wagombea kushiriki midahalo wakati huu wa kampeni.
  Alisema wanaotaka mdahalo na wagombea wa CCM wanatakiwa kumwomba kwa niaba na kupanga mada husika, maswali na kujua washiriki wa mdahalo huo ili kuepuka makundi ya wenye njaa.
  Kuhusu ombi la Spika Sitta kukutana na Dk. Slaa kwenye mdahalo, Makamba ameruhusu, kwa maelezo kwamba wanasiasa hao wamepakana matope, hivyo ni ruksa kwao kujisafisha.
  Alisema si busara kunyamaza unapopakwa tope na mwanasiasa mwenzako, hivyo Sitta ambaye pia ni mgombea ubunge wa Urambo Mashariki, ameruhusiwa kufanya mdahalo ili kujibu mapigo.
  “Hivi wewe mtu akikupaka tope utanyamaza? Huwezi, lazima ujipanguse halafu ulirudishe tope lile lilikotoka... hiyo ndiyo siasa bwana, si kunyamaza tu unatakiwa kujibu,” alisema Makamba huku akinukuu baadhi ya mistari ya kwenye Biblia.

  Source: Tanzania Daima

  My take:

  Makamba is truly a joke!!!!!!!!, Mgombea uraisi afanye mdahalo na mgombea urais period. Hii sasa inadhihirisha ni namna gani JK alivyo mwoga kwa debate.
   
 2. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #2
  Sep 18, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Rais wetu mtarajiwa Dr. Slaa lazima afanye mdahalo na rais anayemaliza muda wake JK. Sitta kama anataka kudahala na Chadema atafutiwe mtu wa saizi yake. It is that simple.
   
 3. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #3
  Sep 18, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Yaani nilikuwa sifikirii kama Makamba is this much of a joke!!!!!!
   
 4. Sir R

  Sir R JF-Expert Member

  #4
  Sep 18, 2010
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 2,177
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Sitta atafutiwe Tundu Lissu.
   
 5. Malafyale

  Malafyale JF-Expert Member

  #5
  Sep 18, 2010
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 11,214
  Likes Received: 3,626
  Trophy Points: 280
  Siamini kama mtu mwenye akili timamu anaweza ongea upupu kama huu;kwa kweli nitaendelea kuwa "Tomaso" na kuamini labda magazeti yametunga tu na wala Makamba hajasema hivyo!

  Please nihakikishieni kama Makamba kweli kasema haya madudu ili kila nikiona habari inayohusu Makamba niwe naifuta nikiamini siwezi soma habari za"chizi"
   
 6. Indume Yene

  Indume Yene JF-Expert Member

  #6
  Sep 18, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 2,932
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Yaani huyu mzee is full of s&#@<^t. Yeye anadai kuwa Sitta ruksa mdahalo kwa sababu wamechafuana na Slaa. Ok, kwa hiyo sasa utaona CCM walivyo nyoka, walidai kuwa siku ya ufunguzi wa kampeni cha CHADEMA pale Jangwani yalitolewa matusi. Sasa kama yalitolewa matusi kwa nini msikutane na huyo/hao waliotoa matusi mkdahala nao? Kwa kukimbia mdahalo, that means yaliyosemwa ni kweli, na ndiyo maana hata Makamba mwenyewe hajataka kuongelea issue yake ya kufukuzwa kazi ya ualimu. Si na yeye alichafuliwa kuwa alibaka? Kwa nini hasije before the Tanzanians na kuwaeleza ukweli?
   
 7. Indume Yene

  Indume Yene JF-Expert Member

  #7
  Sep 18, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 2,932
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Sitta akitolewa nishai kwenye huo mdahalo, utasikia Makamba akidai kuwa Sitta hakuwa anawakilisha CCM bali alikuwa anajiwakilisha mwenyewe.
  Atumwe Lissu naamini ndo saizi ya Sitta. Guridi always anaweka mkia matakoni kwa woga hata kama akiona kivuli cha mwezi.
   
 8. Ilumine

  Ilumine Senior Member

  #8
  Sep 18, 2010
  Joined: Dec 27, 2008
  Messages: 196
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dk.Slaa amechafuana na CCM na hasa JK, sio Sitta kama mtu binafsi. Waseme tu kwamba JK sio 'saizi' ya Dr.Slaa!!!
   
 9. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #9
  Sep 18, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,710
  Trophy Points: 280
  Nadhani ingekuwa ni kumleta Ki'wete na wagombea wengine kwenye mdahalo si Sitta. Makamba ni kama vuvuzela tu!
   
 10. M

  Masauni JF-Expert Member

  #10
  Sep 18, 2010
  Joined: Aug 15, 2010
  Messages: 378
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kinachoniudhi hawa CCM wanatuona watanzania wengine hatuna akili, walisema mdahalo haiwezekani ratiba zimejaa, leo anasema sitta na slaa wamepakana matope mdahalo ruksa. Kikwete amewabeza wapinzani kama alivyofanya sitta mdahalo hakuna. FATAKI MAKAMBA UNAFICHA NINI AMBACHO HUTAKI WATANZANIA TUJUE KWA KIKWETE?
   
 11. M

  MWANALUGALI JF-Expert Member

  #11
  Sep 18, 2010
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 601
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kama Six na Makamba wake wako serious, wajitokeze wafanye mdahalo na mpiganaji wa cCHADEMA anayegombea Ubunge pale Urambo kabla ya kutafuta sifa za mgombea ubunge kutaka mdahalo na Rais Mtarajiwa.

  Samwel Sitta na Makamba hawana adabu kabisa!!!!!!
   
 12. I

  ICHONDI JF-Expert Member

  #12
  Sep 18, 2010
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 588
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Hebu tusome gazeti la mwananchi la leo, nadhani hawa waandishi wa habari wameripoti tofauti. Nilivyosoma gazeti la mwananchi nimemuelewa Makamba, kuwa suala la Sita na Slaa ni lao binafsi na si la ccm na kama wanataka mdahalo it is ok but hautakuwa na baraka za ccm. I think Makamba was clear kwenye hilo, kuwa Slaa almpaka tope Sita, Sita naye katiak kujisafisha akampaka mwenzake tope-- sound funny but huo ndio ukweli. So sikuona kama Makamba amesema kuwa anamruhusu Sita kwa niaba ya CCM afanye mdahalo na Slaa kama hii post inavyosomeka!!

  Kwani angeruhusu ningejua Makamba ni kichaa, kwani sasa huo mdahalo utakuwa ni wa nini, kwani huyu mmoja ni mgombea ubunge na mwingine ni mgombea uraisi. Slaa anatakiwa afanye Presidential debate, sasa hawezi kufanya na Sita, mgombea ubunge, ni sawa na kuchezesha timu ya footbal na basketball, sijui hiyo gemu itaitwaje

  But Makamba kawatukana watu wa kariakoo, kuwa wana njaa, kwamba watakuja kwenye mdahalo wakiwa na njaa kwa kuwa jana yake hawakula halafu waulize swali kwa nini ccm imewalaza njaa? Nadhani Makamba haelewi maana ya debate, hajui kuwa debate ina muongozaji na maswali yanakubaliwa before, na muongozaji ana rungu la kukataa au kukubali swali. Ndio maana aliogopa, akakataza kitu ambacho hakijui, maskini Makamba ameicost CCM darely!
   
 13. I

  ICHONDI JF-Expert Member

  #13
  Sep 18, 2010
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 588
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  CCM yakataa ombi la Spika Sitta Send to a friend
  Saturday, 18 September 2010 08:24

  Waandishi Wetu

  CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kimenawa mikono kuhusu ombi la mgombea ubunge wa Urambo Mashariki, Samuel Sitta la kutaka mdahalo na mgombea urais wa Chadema, Dk Willibrod Slaa kikisema hakihusiki na mgogoro baina ya wanasiasa hao.

  Hayo yametokea wakati mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Jakaya Kikwete akizomewa na kikundi cha watu wanaosadikiwa ni wafuasi wa Chadema wakati akihutubia wilayani Mbulu.


  Sitta, ambaye ni spika wa Bunge linalomaliza muda wake, aliiambia Mwananchi katikati ya wiki kuwa yuko tayari kufanya mdahalo na Dk Slaa kuhusu ukweli juu ya uwezekano wa kutoa elimu bure kama Chadema inavyojinadi kwenye kampeni zake.

  Alitoa ombi hilo wakati CCM ikiwa imeshawaandikia wagombea wake wa ubunge na udiwani ikiwakataza kushiriki kwenye midahalo inayoendeshwa na kituo cha televisheni cha TBC1 hadi kwa maelekezo maalum.

  Ombi la Sitta, ambaye alidai kuwa Dk Slaa ni saizi yake, lilionekana akama ahueni kwa chama hicho baada ya Chadema na CUF kutaka mdahalo wa wagombea urais wa vyama hivyo pamoja na CCM.

  Lakini katibu mkuu wa CCM, Yusuf Makamba, ambaye aliandika waraka huo wa kuzuia wagombea CCM kushiriki kwenye midahalo, alisema jana kuwa mvutano kati ya Dk Slaa na Sitta ni ni wao binafsi na si wa chama.
  "Sitta na Dk Slaa wana mambo yao wenyewe. Dk Slaa alimrushia Sitta tope, yeye akajipangusa akamrudishia," alisema Makamba.
  Aliuelezea mgogoro huo hauihusu CCM kama chama na hata wakiamua kufanya mdahalo, hautaingiliana na mpango mkakati wao wa kukataza wagombea wao kushiriki midahalo na wapinzani.

  Makamba alifafanua kuwa CCM imekataa midahalo kwa sababu hukusanya watu hovyo na hakuna mkakati maalumu ya kuiendesha kwa kujieleza na kukosoana kulingana na sera za vyama.


  Alisema CCM haiogopi midahalo bali isingependa kuona inashiriki kwenye midahalo kwa sababu zinaweza kuibuliwa hoja zisizo na msingi kwa makusudi kukichafua chama hicho tawala.

  "Tunataka mdahalo uwe wa sera. Sio unakusanya watu Kariakoo halafu anajitokeza miongoni ambaye jana alilala njaa halafu anasema jana CCM Ilitulaza njaa," alisema.

  Sitta alieleza kushangazwa na ahadi ya Chadema kuwa itatoa elimu bure, akisema suala hilo haliwezekani na kwamba hakuna serikali inayoweza kuendeshwa bila ya kodi.

  Kauli yake ilimfanya Dk Slaa kumjibu vikali akieleza kuwa kama serikali itaweza kudhibiti ufisadi na kukusanya kodi, elimu bure inawezekana na kwamba ndio maana Sitta na Kikwete walisoma bure.


  Dk Slaa alidai kuwa katika uongozi wake, Spika Sitta alizima kashfa nzito za ufisadi, likiwemo sakata lililotikisa nchi la zabuni ya ufuaji wa umeme wa dharura iliyokwenda mikononi mwa kampuni ya Richmond Development LLC, wizi wa fedha kwenye akaunti ya EPA, ufisadi wa kampuni za Deep Green Finance na Meremeta.

  Wakati huohuo, Makamba alisema jana kwamba CCM haitang'oa hovyohovyo mabango ya kumnadi mgombea wao wa urais ili kutekeleza agizo lililotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) baada ya kuonekana yanakiuka kanuni za uchaguzi.
  Badala yake, Makamba alisema kwamba wanatoa mabango maeneo yale tu ambayo Nec itasema kuwa kuna bango lenye tatizo.

  Alitaja baadhi ya mabango ambayo tayari wameyang'oa kuwa ni pamoja na ambayo Rais Kikwete alikuwa amepiga picha na maaskofu.

  Nec Ilikuwa Imetangaza kwamba mabango yote ambayo yanaonyesha mgombea huyo wa CCM akiwa Ikulu, ni kinyume na taratibu na yanapaswa kung'olewa mara moja.
  Katika hatua nyingine, aliyekuwa mwenyekiti wa chama kilichokufa cha CCJ, Richard Kiyabo amejiunga na CCM.
  Kiyabo alitangaza uamuzi huo jana mbele ya Makamba akisema ameachana na upinzani kwa sababu siyo makini bali unaeneza propaganda.

  Kutoka Mbulu, habari zinasema kuwa wakati Kikwete akihutubia mkutano wake wa mwisho mjini Mbulu, kikundi hicho cha watu kilichokuwa upande wa pili wa uwanja kilikuwa kikipiga miluzi na kuzomea, ambayo ilionekana kuudhi wafuasi wa CCM.

  Kutokana na kucheleewa kufika Mbulu, Kikwete alihutubia kwa dakika chache na baadaye kumtambulisha mgombea ubunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya CCM, Phillip Marmo na baadaye kumaliza mkutano huo.
  Kutoka Monduli, katika hali isiyokuwa ya kawaida waandishi wa habari waliopo kwenye msafara wa mgombea urais wa CCM, Jakaya Kikwete jana walizuiwa kuripoti habari za mgombea huyo kwenye Jimbo la Monduli ambalo linawaniwa na aliyewahi kuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa.

  Ratiba ya jana ya mgombea huyo ambaye yupo katika ziara mkoani Arusha ilionyesha kuwa angenza mkutano wake wa kwanza Namanga na baadaye Ngaramtoni, Monduli, Mto wa Mbu na kumalizia Mbulu.

  Taarifa zilizolifikia gazeti hili kutoka mkoani humo zilieleza kuwa asubuhi ya jana waandishi hao waligawanywa katika makundi mawili; baadhi wakianzia Longido na wengine Namanga.

  Taarifa hizo zilieleza kuwa mara baada ya mkutano wa Longido kumalizika waandishi hao walielezwa kuwa waende moja kwa moja Mbulu na wale walioelezwa kuwa wangeanzia Namanga na kisha kwenda Monduli wakielezwa kuwa hawatakiwi kuhudhulia mkutano wa Monduli na badala yake waende moja kwa moja Mbulu.

  Taarifa hizo zilieleza kuwa waandishi maalum walichaguliwa kuripoti mkutano huo ili baadaye wawape wenzao taarifa za mkutano huo.
  Mjini Monduli, Lowassa alisema hakuna serikali iliyofanya maendeleo makubwa katika awamu zote zaidi ya serikali ya awamu ya nne inayoongozwa na Kikwete.
  Lowassa alisema serikali hiyo imetekeleza Ilani yake katika nyanja zote, ikiwa ni pamoja na kilimo, afya, elimu na mioundombinu.

  Lowassa ambaye ni mgombea wa ubunge wa jimbo hilo, ambaye alipewa nafasi ya kwanza ya kuongea mara baada ya Kikwete kutua Monduli na helkopta, alisema katika jimbo lake la Monduli serikali imetekeleza ilani kwa asilimia 99.
  Mgombea huyo alisema serikali imeondoa tatizo la maji kwa kutumia mradi uliogharimiwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), kujenga sekondari kila kata na sasa ipo katika hatua ya mwisho ya ujenzi ya sekondari tatu za kidato cha tano.

  Naye Kikwete aliuambia mkutano huo kuwa wakazi hawana budi kummchagua Lowassa kwani anawapenda.
  "Nyie mnajua Lowassa anawapenda naomba muendelee kumchagua kuwa mbunge wenu ili muendelee kupata maendeleo," alisema Kikwete.

  Katika mkutano huo, Rais Kikwete aliahidi Serikali yake kulipa kifuta machozi kwa wafugaji ambao waliathirika na ukame mwaka jana.

  "Tumesikia kilio chenu na ingawa hatuwezi kulipa fidia ya ng'ombe kama ng'ombe 200 wa Mzee Loiboki ambao walikufa kwa ukame, tutajitahidi walau kidogo ili kuwafuta machozi," alisema Kikwete.
  Viswani Zanzibar, wakati CCM inazindua rasmi kampeni zake kwenye Viwanja vya Demokrasia mjini Unguja, bado meneja wake hajawekwa bayana.

  Akizungumza na waandishi wa habari jana kwenye ofisi kuu ya CCM Kisiwandui, katibu wa kamati maalumu ya Nec &#8211;Itikadi na Uenezi, Vuai Ali Vuai alisema watamtangaza meneja kampeni katika uzinduzi wa kampeni hizo leo.
  "Meneja wa kampeni atatangazwa baadaye, uzinduzi bado uzinduzi utafanyika kesho (leo) msiwe na haraka sisi tumekuja kutangaza uzinduzi wa kampeni zetu hayo mambo mengine yatajulikana huko kwenye kampeni," alisema Vuai.

  Wakati akisema hayo, imebainika kuwa mabango ya kumnadi mgombea wa urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM, Dk Ali Mohammed Shein yamebainika kuwa na kasoro.

  Kwenye bango lililobandikwa eneo la darajani lililo Manispaa ya Zanzibar, kuna picha ya sura ya Dk Shein, lakini maandishi yanasomeka chagua CCM, chagua Kikwete.
  Lakini Vuai alisema hana taarifa hizo na wala hajaona picha hizo, lakini akasema huenda ni bahati mbaya katika uchapishaji.

  "Mimi sijaziona hizo picha inawezekana ikawa ni bahati mbaya kwa kuwa walioandika nao ni binaadamu, lakini nasema kuwa tuna mabango aina mbili aina moja mabango yanayomnadi mgombea wetu Kikwete na yanayomnadi Dk Shein na tulikuwa tuna matayarisho na uzinduzi, lakini hatujazindua na hayo mlioyaona ni bahati mbaya tu.'

  Alisema yamebandikwa kutokana na hamu ya wafuasi lakini kesho nakuhakikishieni mtajua kuwa leo ni siku ya uzinduzi wa CCM," aliahidi Vuai.


  Habari hii imeandikwa na Leon Bahati, Salma Said, Zanzibar, Boniface Meena, Karatu na Mussa Jumma, Monduli.


  Hii ndio habari ninaiamini, naona ya Tanzania Daima haiko wazi sana
   
 14. f

  fungafunga Member

  #14
  Sep 18, 2010
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 40
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Sijui kwanini nilitokea kuichukia ccm tangu elnino ya 1998. Siwapendi hawa jamaa kama nini
   
 15. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #15
  Sep 18, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  mie namshauri JK hile appointment yake nyingine ya kupimwa akili ikifika amchukue na huyu rafiki yake (makamba) nae apimwe akili,tunaweza tukawa tunamlaumu kila siku uropokaji wake kumbe mwenzetu punguani.
   
 16. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #16
  Sep 18, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Bunge linapovunjwa spika anaendelea na uspika wake? is samwel sitta still the speaker? damn
   
 17. v

  valour Senior Member

  #17
  Sep 18, 2010
  Joined: Aug 3, 2010
  Messages: 167
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Yaani anataka kusema Kweli Muasisi wa Nchi hii hajafanya mambo makubwa angalau walisomeshwa bure kitu ambacho hawawezi kufanya sasa hivi. Hata kama tunapenda kujikomba kwa viongozi wetu ili tusisahauliwe wakati vyeo vinagawiwa inabidi tujifunze kushukuru pale ambapo wamefanya mazuri
   
 18. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #18
  Sep 18, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Hivi hii michezo ya kisiasa kwa nini ni ya kipuuzi?
  Makamba should come out and clarify why hasnt he debated with Slaa ilihali alimchafua na yeye?
  Au yaliyosemwa juu yake ni kweli tupu?
   
 19. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #19
  Sep 18, 2010
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  ooh dear me! what a heaped load of mediocrity!!!

  Okay, itakuwaje kama mtu anayegombea ubunge kwa tiketi ya upinzani atakapo mtupia madongo Mh. Kikwete kwenye moja ya midahalo inayoendelea, je Mh. Kikwete kama mgombea urais atajibu mapigo hayo kupitia mdahalo, au?!! Well... madongo yapo na watu watayarusha tuone response...!!!

  Haki ya nani tena naamini kuna baadhi ya wanaCCM wanatiwa majaribuni kweikweli na kauli hizi za viongozi wao wa chama!!
   
 20. Emma Lukosi

  Emma Lukosi Verified User

  #20
  Sep 18, 2010
  Joined: Jul 22, 2009
  Messages: 932
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Baba wa taifa alivyo sema kuwa "mtoto wa mrisho hajakua" kwa kutokufahamu mafumbo ya mzee yule mlizani umri. Hawezi na bado hajakomaa.:mad2:
   
Loading...