Mdahalo kati ya Freeman Mbowe na Hamad Rashid ITV

Mdahalo kati ya Freeman Mbowe na Hamad Rashid ITV

Mbowe anawaambia wananchi washishtuke na wanasiasa wanapotofautiana ndo siasa..
CDM hawapiganii maslahi ya Slaa kama mgombea bali wanataka iundwe tume ifatilie matokeo na itoe mfumo utakaosaidia chaguzi zijazo, na anaonya kama hadi uchaguzi ujao kama katiba na tume vitabaki hivi hivi basi amani itakuwa mashakani..

ITV wanawind up sasa, wadau sasa tuchangie hoja kwa hoja. sikuweza kuandika kila kila kitu maana some times internet zetu haziko speed kama maneno yanavyotamkwa
 
Mbowe amejibu vipi swali la kama Chadema itashiriki uchaguzi ujao iwapo katiba haitabadilisha?
 
kwa nini CUF wanalazimisha kuungana na CDM wakati wao ni sehemu ya Serikali SMZ?
 
Nchi Mbili?? Zanzibar na Tanganyika? au na TAnzania? Katibaaaaa

Kama HOUR anasema tuna nchi mbili amekuja kutafuta nini huku, kwanza ilitakiwa awepo mwenyekiti prof na sio yeye
 
kwa maoni yangu naona hamadi ameshinda mdahalo kwa kujibu maswali kitaalamu zaidi na huku mwenzake kuonyesha hasira zaidi na bila kuficha makovu ya wakati wa uchaguzi!!!!
 
Kiongozi Nicky82 na reporters wengine,
Asante sana. Mmefanya kazi nzuri kwelikweli!
 
Nimegundua tatizo la msingi la CUF wakiongozwa na Hamad Rashid la kukataa kuunganisha nguvu na CDM ni wivu wa kukosa kuongoza kambi ya upinzani baada ya kuzidiwa na CDM. Hamad Rashid amejaribu kuunganisha nguvu na NCCR, TLP na UDP kwa lengo la kuchukua kambi ya upinzani lakini kanuni zinamkatalia sasa anataka zibadilishwe.

Baada ya juhudi zake kukwama sasa analizimisha CDM iwakubali NCCR vibaraka wa CCM nao waingie kwenye kambi ya upinzani akisahau wao 1995 walikataa kuunda kambi ya upinzani na NCCR ambayo ilikua na wabunge wengi ikaunda kambi na UDP yenye wabunge wachache. hamna aliyewapigia kelele lakini wao wanamchagulia kiongozi watu wa kufanya nao kazi kweli hii kali.

Sasa hivi CUF wajenga urafiki na chama chochote kile ambacho kipo against na CDM kwanini? kama siyo wivu? Wamesehau CDM ilivyowaunga mkono mwaka 2000 wao hata kuthubutu hawajawahi kwa nini? Wana wivu na madaraka hasa ya kambi ya upinzani thats why unakuta hamad ana kila aina ya vikwazo.

Upinzani wa kweli utajengwa na wapinzani wa ukweli wenye nia thabiti ya ukweli ya kuwakomboa watanzania wa ukweli wanaotaabika na umasikini kikwelikweli.

Ni mtazamo tu jamani.
 
Nimesikitishwa sana na kauli ya mbowe kuwa Chadema haiwezi kushughulikia swala la kupunguza mishahara ya wabunge eti kwa sababu hawajashinda uchaguzi mkuu. Ina maana kwa kushindwa uchaguzi mkuu, Chadema hawawezi kubadili chochote? Je, hiyo katiba moya anayoizungumzia wataweza vipi kupressurize???
 
Mbowe kaja na Mamluki nini???? Makofi hata yasipohitajika...................
hakuja na mamluki ila tu watu wanaamini kila anachoongea hata pale ambapo anakuwa bado hajaongea, they are always motivated by his words...maneno ya ukombozi ya kuifanya tz iliyofungwa ktk mikono ya umaskini na unyanyasaji ibadilke
 
Hapo ndipo muafaka utakapovunjika.watamwambia mbona umetutukana?
 
Back
Top Bottom