Zion Daughter
JF-Expert Member
- Jul 9, 2009
- 8,921
- 4,236
Hapo kwenye red ni kudanganyana.Hivi kweli bado hatujui kwa nini wanafunzi wanafeli?mfumo uliopo bado ni mzuri tatizo lipo kwa wasimamizi wa mfumo huu,wazazi na mwanafunzi mwenyewe.
Kiufupi serikali imeshindwa kudhibiti madhara ya utandawazi.leo hii ukikatiza kwenye vituo vya daladala jaribu kuhesabu matangazo ya '''elimu ya sekondari kwa miaka miwili''' yalivyo mengi na hakuna kiongozi yoyote aliyewahi kuelezea suala hili.
Walimu ni sehemu ya tatizo kwa sababu wanafundisha wasichokipenda na wasichokijua.
Wazazi wa siku hizi hawafuatilii maendeleo ya mtoto shuleni.wazazi hawana muda wa kufundisha watoto wao.wazazi hawashawishi watoto wao wasomee au wapende fani fulani fulani.
Wanafunzi wa sasa wana nyenzo nyingi za kusomea lakini kutwa atakuwa kwenye facebook,video game,kukariri mashairi ya hussen machozi na tamthilia za amerca kusini.hata hivyo vyote hivi sio tatizo iwapo kuna ratiba inayompatia muda wa kujisomea.
Mwisho napenda kupinga hoja ya mwanakijiji kwa sababu bado hatujajua kiukamilifu ni nini hasa chanzo cha kuanguka kwa wanafunzi wetu.
Nashauri ufanyike utafiti katika maeneo yote yanayohusu elimu ili tujue tatizo liko wapi hii ndio njia pekee ambayo ni sahihi na salama ya kubadilisha mfumo wa elimu nchini,hakuna haja ya kudesa kwa wakenya.
Walimu wana mazingira duni kama mishahara isiyokidhi,taaluma ya ualimu ni ya watu waliofeli form four wanaenda crash course miezi 6 kisha wanakuwa walimu.tena hakuna monitoring performance kwa hao walimu...etc..tujaribu kutatua hayo kwanza