MDAHALO: Elimu ya Msingi iwe miaka 5 halafu Middle School then Secondary na High School...

nakubaliana na wewe!!ni lazima tuandae kundi dogo la 'wasomi' lakini tusisahau kutoa ujuzi kwa 'vilaza' waliobakia.

Meningitis,

..nilichopendekeza hapo ni a "TACTICAL RETREAT" ili tuweze kujipanga upya ktk kuboresha sekta ya elimu.

..kwa mtizamo wangu ni vema serikali ika-consolidate shule chache kati ya shule za kata, na kuhakikisha shule hizo zinapatiwa nyenzi zote, pamoja na waalimu, ili kuziwezesha kutoa wanafunzi waliofikia viwango.

..baada ya kufanya hivyo serikali sasa inaweza kujipanga upya na kuleta mpango makini zaidi wa UNIVERSAL SECONDARY EDUCATION.

NB:

..nakubaliana na wewe 100% kwamba tusisahau kutoa ujuzi kwa "vilaza" waliobaki.

..kuhusu suala la "vilaza" au "vipanga" mimi naamini every child is special, kinachotakiwa ni wazazi na waalimu kuhakikisha kwamba tunafanya kila tuwezalo kuvumbua kipaji cha kila mtoto/mwanafunzi. mimi nakumbuka shuleni kulikuwa na watoto hawafanyi vizuri darasani tukiwaita "vilaza" but they were very good in sports. Sasa wazazi na waalimu wangeviendeleza vipaji vile leo wangekuwa watu muhimu ktk jamii.
 
shule za kata zigeuzwe VETA tumemaliza problem, VETA kuwa na michepuo ya bongo flevour , bongo movie tumemaliza problem.
 
Companero,

..tatizo ni kwamba hatufundishi Kiingereza kabisa halafu tunakuja kulalamika kwamba wanafunzi hawaimudu lugha hiyo.

..mimi binafsi nilisoma shule ya sekondari ya serikali ambayo ni "elite" lakini ktk english literature tulisoma kitabu kimoja tu, "The River Between", tena wala hatukukimaliza kwasababu mwalimu aliugua na hatukupatiwa mwalimu mwingine.

..bahati nzuri nilikuwa na ndugu zangu walionitangulia shuleni hivyo niliweza kusoma madaftari yao na kuwa na idea vitabu vingine kama "Things Fall Apart", "No Longer at Ease", etc vinazungumzia nini. Hicho ndicho kilichoniwezesha kujibu mtihani wa Kiingereza kidato cha 4.

..binafsi nadhani tuweke jitihada kwa watoto wetu waweze kuzungumza kwa ufasaha KIINGEREZA na KISWAHILI.
 
Me nafikiri wazo lako si baya,ila kwa nchi yetu kinachotakikina nikureview hiyo mitaala kwani ni mibofu na waalimu wenyewe ni wabobofu,wanachojua ni kuchapa wanafunzi na wala sio kufundisha.Nchi hii quality of education ni nzuri na ndio maana wanafunzi wanafeli.kumfundisha mwanafunzi ni process kama process zingine na kma ni hivyo ukiprocess low quality eduaction then unaexpect kupata mtu anaefaulu wakti input yako ni poor. unavuna ulichopanda.
 
Companero,

..tatizo ni kwamba hatufundishi Kiingereza kabisa halafu tunakuja kulalamika kwamba wanafunzi hawaimudu lugha hiyo.

..mimi binafsi nilisoma shule ya sekondari ya serikali ambayo ni "elite" lakini ktk english literature tulisoma kitabu kimoja tu, "The River Between", tena wala hatukukimaliza kwasababu mwalimu aliugua na hatukupatiwa mwalimu mwingine.

..bahati nzuri nilikuwa na ndugu zangu walionitangulia shuleni hivyo niliweza kusoma madaftari yao na kuwa na idea vitabu vingine kama "Things Fall Apart", "No Longer at Ease", etc vinazungumzia nini. Hicho ndicho kilichoniwezesha kujibu mtihani wa Kiingereza kidato cha 4.

..binafsi nadhani tuweke jitihada kwa watoto wetu waweze kuzungumza kwa ufasaha KIINGEREZA na KISWAHILI.
Mkuu wangu nakubaliana na wewe lakini bado unachanganya lugha na elimu. watoto wetu wanazungumza kiswahili hakuna sababu ya kuwafundisha lugha hii isipokuwa itumike kwa kuwafundishia maana ndio lugha ya mawasiliano baina ya mwalimu na mwafunzi. Somo la Kiswahili lifundishwe pia kwa sababu ni somo linalomkuza mtu ktk fani ya usanii na uandishi.

Kiingereza kama lugha ndio inatakiwa kuwekewa mkazo ili vijana wetu wanapomaliza darasa la tano wawe na uwezo wa kuwasiliana kwa lugha hii, hivyo wanapoanza masomo kwa lugha hii wawe wanajua wanafundishwa kitu gani. Na somo la kiingereza kama lilivyo somo la kiswahili lifundishwe kwa malengo ya kumjenga mwanafunzi ktk fani zake. Kumfundisha mtoto lugha haichukui miaka kama utawapata walimu wenye ujuzi wa kufundisha lugha na sio somo la kiingereza.

Na sababu pekee ambayo binafsi yangu napitisha matumizi ya kiingereza sio swala la mawasiliano isipokuwa bado kabisa kiswahili hajitajikita ktk sayansi na teknologia japokuwa lugha nyingi duniani zimeweza kukuzwa na kuchukua maneno mapya haraka ili kukuza lugha hizo kulingana na sayansi na teknologia, sisi tunakikuza kiswahili kwa sababu ya usanii na Bongo Flava... malengo yetu hayakidhi sababu ya kuipanua lugha yetu tupate kushindana ktk dunia hii ya sayansi na teknologia.

Hivyo, kiingereza kitumike tu kwa sababu ya kuwajenga watoto wetu kielimu japokuwa tena ni kazi kubwa na ngumu zaidi na nchi hasa maskini nyingi zimeshindwa kujikwamua ktk lindi la Ujinga. Sio Nigeria wala South Afrika kote tunaongoza duniani kwa Ujinga kutokana na kutumia lugha ambayo sii ya mawasiliano baina ya mwalimu na watoto..
 
Miaka ile 5 ya kwanza ya elimu ya msingi iwe ni kwa ajili ya:

Kusoma (Kiswahili na Kiingereza)
Kuandika na Uelewa (comprehension)
Kuhesabu (arithmetic)
Michezo na Sanaa

(Mwaka wa kwanza uwe katika kujifunza kusoma na kuandika - exclusively).

Middle School miaka 2 iwe kwa ajili ya:

Kuzama katika hesabu na lugha
Sayansi, Siasa (Civics) na Sanaa
Character development (kupitia michezo na extra curricular activities)

secondary (secondary education) miaka 2
Miaka 2 ya pure liberal arts (introductory courses)

High School - kuzama katika liberal education na semi specialization. (unafuta combination zilivyo sasa). Mwaka wa mwisho mtoto atakiwe kujua anataka kusomea nini Chuo Kikuu au onother tertiary institution.

Au mfumo gani mzuri zaidi wa kujaribu kudeal na hili tatizo la wanafunzi kufeli sana kuanzia shule ya msingi, sekondari na vyuo?

Mkuu Mwanakijiji inawezekana tukawa na mipango mingi ya kuboresha elimu lakini kama hakuna commitment kwa maana ya HAKI na WAJIBU kati ya Serikali na Walimu things will remain the same. Tatizo la elimu sio la muundo tu ila ni la mfumo na kwa kiasi kikubwa ubovu wake unachangiwa na poor governance. Imekuwa ni bora liende na pamoja na kuruhusu watu kuchezea mfumo kwa sababu binafsi (remember Mungai).
 
Miaka ile 5 ya kwanza ya elimu ya msingi iwe ni kwa ajili ya:

Kusoma (Kiswahili na Kiingereza)
Kuandika na Uelewa (comprehension)
Kuhesabu (arithmetic)
Michezo na Sanaa

(Mwaka wa kwanza uwe katika kujifunza kusoma na kuandika - exclusively).

Middle School miaka 2 iwe kwa ajili ya:

Kuzama katika hesabu na lugha
Sayansi, Siasa (Civics) na Sanaa
Character development (kupitia michezo na extra curricular activities)

secondary (secondary education) miaka 2
Miaka 2 ya pure liberal arts (introductory courses)

High School - kuzama katika liberal education na semi specialization. (unafuta combination zilivyo sasa). Mwaka wa mwisho mtoto atakiwe kujua anataka kusomea nini Chuo Kikuu au onother tertiary institution.

Au mfumo gani mzuri zaidi wa kujaribu kudeal na hili tatizo la wanafunzi kufeli sana kuanzia shule ya msingi, sekondari na vyuo?
Nimeipenda hiyo ila kidogo tu marekebisho kama itaonekana kufaa, baada ya primary education hapa tuwagawanyanye wanafunzi kulingana na uwezo na vipaji.

wale ambao wako vyema kinadharia waingie sekondari na iwe ni miaka 7 na mwaka mmoja wa maandalizi ya kujiunga na chuo baada ya mtihani jumla miaka 8

mkondo mwingine ni kwa wale wenye uwezo zaidi katika stadi mbalimbali za kazi na uwezo wa kinadharia waingie katika shule za sekondari moja kwa moja na kukaa hapa kwa miaka 4 wakitoka hapa wajiunge na vyuo kulingana na taaluma watakayoelekea na ufaulu. baada ya chuo wanaweza kwenda katika soko la ajira ila kama atapenda kuendelea na chuo kikuu basi kuwe na mwaka mmoja kwa ajili ya maandalizi ya chuo kikuu baada ya kufanya mtihani


kundi la mwisho ni kwa wale woote ambao hawataanguakia katika kundi la kwanza wala la pili, hawa wajiunge na shule ya sekondari kwa miaka mitatu baada ya hapo wajiunge na mafunzo ya ufundi(Vocational Training) kwa miaka minne baada ya hapo wanaweza kwenda katika soko la ajira au kama atataka kuendelea na masomo ya chuo kikuu basi watakaa tena mwaka mmoja kwa maandalizi ya chuo kikuu baada ya kufanya mtihani na kufaulu.

Hii ninamaana ile middle school isiwepo na mitaala itakuwa tofauti katika kila mkondo wa elimu ya sekondari

hii itawasaidia vijana wengi kutokimbia shule na kuleta changamoto katika mfumo wa ajira na ushindani katika elimu.
 
Tatizo lipo pia kwa obora wa elimu itolewayo na walimu kuanzia shule shule ya msingi.Walimu wengi wanaofundisha shule ya Msingi huwa ni wale waliopata Div 4, wengi wao hawajui Kiingereza hivyo huwapotosha watoto toka wakiwa wadogo wawafundishapo Kiingereza na madhara yake yanaendelea katika level zote za elimu muhusika atakazopitia.

.Nashauri Walimu wawe ni watu waliofaulu sana na wawe na vipaji vya taaluma husika na wawe wa level ya diploma kwa kuanzia lakini Degree iwe msisitizo.

vile vile mishahara ya walimu iwe mikubwa ili walimu wenye elimu nzuri waridhike na ajira ya ualimu kwa sababu itawatosheleza kukidhi mahitaji yao.

Pia walimu wa lugha ,iwe kifaransa ,ama kiingereza ,wapate kujifunza lugha hiyo kwenye nchi ambazo ni lugha mama,hii itawafanya wawe na uelewa mkubwa wa lugha husika pindi wataporudi nyumbani kufundisha.

Mwisho naunga mkono hoja yako ya kubadililisha structure ya elimu kwa sababu lengo lako ni kuboresha na naamin umefanya tafiti juu ya hili.
 
MKuu mwana kijiji una hoja nzuri, lakni bado tatizo letu kwenye elimu haliko kwenye structure ya muda wa kusoma... mf unaposema mwaka wa kwanza exclusively kujifunza kusoma na kuandika haitoshi, kwani kuna wanaoenda taratb mpka la saba hawajui kusoma wala kuandika, hoja ya msing hapa ni kufanya mapinduz ya kwel kwenye elimu ya msingi kama tunataka kujenga taifa imara la elimu kwa wote, tatizo linaanzia kwa walimu mpaka wanasiasa.! walimu hawaandaliwi vizuri, mazingira ya kujifunzia magumu hata choo hamna, vitabu hakuna, madawat hakuna, bado katika hal hiyo hiyo, katika nchi hiyo hiyo kuna shule za academia zenye computer,chakula bora, motivated teachers.. kwenye ada sasa..! lol matajir pekee! elimu ya veta iwe ya lazma kwa wahitimu waliokosa nafas il kujenga taifa ya watu wanaofanya kaz, tatizo kubwa ni wanasiasa, wamekuwa wakitumia matatizo ya watz kama mitaj yao na cdhan kama ametokea m2 anania ya dhat ya kuyaondoa, evryone is thinkin about him and his family(selfishnes) i wonder wat a poor country! RWANDA?
 
Back
Top Bottom