Mdahalo - Dawati la Jinsia lifike mpaka Vijijini

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944

MDAHALO - DAWATI LA JINSIA LIFIKE MPAKA VIJIJINI

Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Singida Mhe. Martha Gwau mnamo tarehe 06 Machi, 2023 katika wiki ya kuadhimisha Siku ya Mwanamke Duniani alishiriki mdahalo wa Wanafunzi wa kike katika shule ya sekondari Mwanamwema.

Mhe. Martha Gwau, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida ni miongoni mwa viongozi waliofika shuleni hapo kusikiliza mdahalo ambao ulihamashisha wazazi na viongozi mbalimbali kujadili na kuchukua hatua mbalimbali za kupinga unyanyasaji wa kijinsia

Wanafunzi wa kike katika shule ya sekondari Mwanamwema wameshauri serikali kupeleka huduma ya dawati la jinsia maeneo ya vijijini ambako wahanga wa unyayasaji wa kijinsia wanapatikana kwa wingi.

Wanafunzi hao wametoa pendekezo hilo tarehe 06/03/2023 katika mdahalo uliohusu binti wa kitanzania katika ulimwengu wa kidigitali, ulioendeshwa na Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Mwl. Dorothy Mwaluko ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mdahalo huo.

Wanafunzi hao wameeleza kuwa kuna kila sababu ya kupeleka huduma ya dawati la jinsia mpaka vijijini ili kuwasaidia wanawake na mabinti ambao ndiyo wahanga wakubwa wa unyanyasaji pamoja na udhalilishwaji kijinsia kutokana na mila na desturi za ukandamizaji.

Mabinti hao wa kidato cha kwanza mpaka cha sita, katika Shule ya Mwanamwema Shein, iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Singida wametaja mila kandamizi kwa wanawake zinazopaswa kuachwa ni pamoja na, kukosekana kwa uhuru wa maoni na maamuzi kwa wanawake na mabinti, suala la mahari linaloondoa utu wa mwanamke na hasa mtoto wa kike, mwanamke kuchukuliwa kama chombo cha starehe na wanawake kunyimwa haki ya urithi.

Katibu Tawala Mkoa, Mwaluluko, amewaasa mabinti hao kuwa chachu ya mabadiliko katika jamii, na kuwataka kuwa na ujasiri utakaowawezesha kujisimamia ili kuiwezesha jamii kuondokana na dhana iliyojengeka kuwa mwanamke ni dhaifu.

Mwaluko pia alitumia fursa hiyo kuwaasa mabinti hao kutojihusisha na masuala ya mapenzi wakiwa shuleni huku akiwataka kuepuka vishawishi mbalimbali kama lift wakati wa kwenda shule na zawadi kutoka kwa vijana na watu wenye tamaa.

Mbunge Mhe. Martha Gwau aliamsha msisimko kwa mabinti baada ya kutoa ushuhuda ulio hai wa safari ya maisha yake hata kufikia hapo alipo sasa, kutokana na kujithamini na kujituma na hata kufikia malengo yake.

Mhe. Martha Gwau pamoja na kuongea na wanafunzi pia alitoa zawadi kwa wanafunzi hao. Wengine waliopeleka zawadi kwa wanafunzi ni Chama cha Walimu Tanzania Mkoa wa Singida wakiongozwa na Bi. Digna Nyaki , Katibu wa CWT Mkoa.

WhatsApp Image 2023-03-09 at 11.45.18.jpeg
WhatsApp Image 2023-03-09 at 11.45.18(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-03-09 at 11.45.21(2).jpeg
WhatsApp Image 2023-03-09 at 11.45.20(2).jpeg
 
Kwani vijijini hakuna madawati ya kijinsia. Mbona Rombo Kilimanjaro nimeyaona?
 
Dawati ni la muhimu, ila muhimu zaidivbi kuifahamu sheria ya mtoto hapa
 
Dawati la jinsia ni ujinga mtupu. Yaani hawa wazungu wametuletea huu ujinga tuanze nao na jinsia tukimaanisha mtoto wa kike tu ili baadaye waje watuambie jinsia si mwanamke na mwanaume bali jinsia mtu anaweza kuamua kiasi kwamba zitakuwa ofisi za kushughulikia mashoga zaidi badala ya ustawi wa jamii. Mi kwangu dawati la jinsia ni ujinga ambao serikali imeuendekeza, sisi matatizo yanayo tukabili ni makubwa zaidi ya jinsia na hata huko ulaya hawana haki ya usawa wa kijinsia, yaani ukiwa mwanamke utalipwa kidogo hat kama sifa mtakuwa sawa na mwanaume na hii ni kwa sababu uwezo wa mwanamke ukija kwenye hedhi utamfanya abaki home tu.
 
Back
Top Bottom