Mdada anapomkunjia ndita ampendaye atarajie nini?

Mdada anapomkunjia ndita ampendaye atarajie nini?

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
219,502
Reaction score
911,254
Yupo huyu mdada kweli anapendeza sanaaaaaa
Yupo huyu kijana kweli anampenda huyu mdada lol..
Penzi lao laelekea kuwaka na halina kizima moto lakini,
Upo mushkeli katika dimbwi la mahaba yao tarajiwa..
Mdada anapokunjia ndita ampendaye atarajie nini?

Sijui ana deko lipi huyu mdada badala ya kicheko
Kila amwonapo njemba wake huanza kukuda ndita!
Jambo aulizwapo huanza kujibu mazogo bila lengo
Kijana ameghafilika hajui anapendwa au anavumiliwa tu
Mdada anapokunjia ndita ampendaye atarajie nini?

Swahiba wa mdada wadai naye kashikwa pabaya
Ila hizo ni hadaa zake aonekane kama hajapenda sana
Khofu yake akionekana kafa pengine asije kufa kikwelikweli
Hana imani na kijana kama naye anampenda kiuthabiti
Mdada anapokunjia ndita ampendaye atarajie nini?

Njemba sasa imetosheka na udhia sasa yawasha mataa
Mdada kaghafirika hajui la kufanya kwani ndita siyo utu
Kibuti chanukia nami kuwasuluhisha nimeghairi kabisa
Waswahili husema wagombanapo ndugu chukua kapu ukavune
Mdada anapokunjia ndita ampendaye atarajie nini?
 
Mkimbize kama hasomeki ,badala ya kuonyesha furaha anaweka ndita ili iweje ?

Mnama ukimkimbiza utakimbiza wangapi? Anachohitaji ni kusomeshwa somo likamwingia barabara kichwani ya kuwa ndita hazina tija
 
Last edited by a moderator:
Mkuu huyu mdada ana kisebusebu na .............!.
Na bila kujua alishaoza ndiyo maana kaghafirika hajui la kufanya.

 
Sasa huyo mdada anakunja ndita wakati gani? na hiyo tabia hiyo huwa anamfanyia mpenzi wake tu? na ameanza lini hiyo tabia au ni kawaida yake?
 
Mnama ukimkimbiza utakimbiza wangapi? Anachohitaji ni kusomeshwa somo likamwingia barabara kichwani ya kuwa ndita hazina tija

Ha haaa mpaka apatikane the right one, we hujajua tu kinachoendelea hapo anamtisha mtu mzima ili awe mdogo kama piriton,sasa mtu mzima ukiona haiwezekani ya nini kubaki.
 
Rutashubanyuma umepotea wewe hata salamu hamna?
bwana wewe mimi haijawahi nitokea nikakunja ndita mini nikimuona wa moypo wangu popote huwa nakufa kicheko na kutabasamu yeye anacheka sana wala sijui kwa nini mfano labda ananisubiri sehemu nikitoa sura tu huwa anacheka mimi pia hoi,saa nyingine huwa anauliza haya leo umefanya nini mbona unacheka ila huwa nafurahi sana mpaka najikuta napitiliza nacheka wee.mimi nimejifunza Mtambuzi kasema kutabasamu ndio uzuri wa mwanamke nimefundwa mie na Mtambuzi hata nikiwa sina raha hujitahidi kutabasamu mie ili nipendeze pole yako wewe unayekunjiwa ndita Rutashubanyuma
 
Last edited by a moderator:
hafurahii matendo yako..inaonekana nje anafurahishwa sana...
hivo akija kwako anaona kero tu..
whatchout..
 
Mapenzi kizungumkuti
Ila kuna aina ya kukunjia ndita, wengine hata huwezi wakunjia aisee
 
Back
Top Bottom