Mdada anapomkunjia ndita ampendaye atarajie nini?

...Anatakiwa aulizwe mpenzi ni aje leo mbona umeninunia? labda anaweza kufunguka kwa mpenziwe, na akagundua tatizo lilikuwepo ni dogo sana....Mwanamke kudeka ndani ya mapenzi muhimu.

Mdada anapokunjia ndita ampendaye atarajie nini?
 
Last edited by a moderator:
BAK hivi na mwanaume anayekunja ndita huwa ni nini?

...Anatakiwa aulizwe mpenzi ni aje leo mbona umeninunia? labda anaweza kufunguka kwa mpenziwe, na akagundua tatizo lilikuwepo ni dogo sana....Mwanamke kudeka ndani ya mapenzi muhimu.
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: BAK
na nyie wanaume wake / wapenzi wenu wanapowakunjia ndita hebu mjishushe mtafakari mlipokosea mrekebishe maisha yaishe.......

n wewe dada ndita za nini? kama kakukosea si umwambie, na akirudia makosa si umweleze? kama hajirekebishi si uanze?
 
Sasa huyo mdada anakunja ndita wakati gani? na hiyo tabia hiyo huwa anamfanyia mpenzi wake tu? na ameanza lini hiyo tabia au ni kawaida yake?

Jibu la swali lako liko kwenye hiyo beti hapo chini mkuu....

Swahiba wa mdada wadai naye kashikwa pabaya
Ila hizo ni hadaa zake aonekane kama hajapenda sana
Khofu yake akionekana kafa pengine asije kufa kikwelikweli

Hana imani na kijana kama naye anampenda kiuthabiti
Mdada anapokunjia ndita ampendaye atarajie nini?

Inabidi naye aulizwe kulikoni leo? mbona una kisirani hivyo?.....sikulala vizuri usiku wote nilikuwa macho nawaza mafisadi wanavyoimaliza nchi lol!

BAK akikujibu wewe ndiye unmtia kisirani itakuwaje?
 
Last edited by a moderator:
na nyie wanaume wake / wapenzi wenu wanapowakunjia ndita hebu mjishushe mtafakari mlipokosea mrekebishe maisha yaishe.......

n wewe dada ndita za nini? kama kakukosea si umwambie, na akirudia makosa si umweleze? kama hajirekebishi si uanze?

BADILI TABIA ni sahihi kuomba msamaha kwa kosa ambalo hata hulijui?
 
Last edited by a moderator:
Best inabidi wanawake tupige kura kung'oa mafisadi, manake kumbe wanaathiri ndoa hivi eeh? Tunabembeleza ham'bembelezeki
Inabidi naye aulizwe kulikoni leo? mbona una kisirani hivyo?.....sikulala vizuri usiku wote nilikuwa macho nawaza mafisadi wanavyoimaliza nchi lol!
 
Ila kweli ki2 smile bwana huwa ni suluhisho sometimes,
mie siku moja my nan wangu huyu karud home kachelewa, na mara nyingi akichelewa bla taarifa huwa nakasirika bt this tym ckuwa hata mekasirika, sasa mwenyewe kaja nimempokea akaanza, so nambe umekasirika hata hujaniuliza nimechelewa kwa nn......na blabla kibao, mie niko kimya tu namwangalia, alipomaliza nlichofanya nilitabasam tu kwa jinsi alivyokuwa anajieleza wakat mie hata nlikuwa cjakasirika,kuona nasmile na yy hapo hapo mood ikabadilika coz alikuwa analalamika, na kunisifia akanisifia kuwa huwa napendeza na nnavutia zaid nkismile heheheee na anapata aman sana akiiingia kwa door akakumbana na hyo smile.
nlijifunza ki2 pale,
 
Yupo huyu mdada kweli anapendeza sanaaaaaa
Yupo huyu kijana kweli anampenda huyu mdada lol..
Penzi lao laelekea kuwaka na halina kizima moto lakini,
Upo mushkeli katika dimbwi la mahaba yao tarajiwa..
Mdada anapokunjia ndita ampendaye atarajie nini?

Sijui ana deko lipi huyu mdada badala ya kicheko
Kila amwonapo njemba wake huanza kukuda ndita!
Jambo aulizwapo huanza kujibu mazogo bila lengo
Kijana ameghafilika hajui anapendwa au anavumiliwa tu
Mdada anapokunjia ndita ampendaye atarajie nini?

Swahiba wa mdada wadai naye kashikwa pabaya
Ila hizo ni hadaa zake aonekane kama hajapenda sana
Khofu yake akionekana kafa pengine asije kufa kikwelikweli
Hana imani na kijana kama naye anampenda kiuthabiti
Mdada anapokunjia ndita ampendaye atarajie nini?

Njemba sasa imetosheka na udhia sasa yawasha mataa
Mdada kaghafirika hajui la kufanya kwani ndita siyo utu
Kibuti chanukia nami kuwasuluhisha nimeghairi kabisa
Waswahili husema wagombanapo ndugu chukua kapu ukavune
Mdada anapokunjia ndita ampendaye atarajie nini?

oooh cam'on guys..... wanaume wanaume wanaume.... jamani mbona mnajifanya wa gharma kubwaaa kihivyo?? yaani nyie mkiwa kwenye mahusiano mnataka kuenziwe kama wafalme??? niliwahi kusoma post moja inayosema eti mwanamume huwa haambiwi nakupenda a.k.a I love you! hivyo anapanga kumuacha mkewe kisa hicho tu, huyu tena ndita zinamfanya ataka kupiga kibuti mpenzi.... hivi ni kweli haya mapenzi ni ya dhati?? mbona kwenye mahusiano kuna maudhi mengi mengi sana ambayo yanaweza kuwapata na bado watu tunavumiliana tunaendelea na maisha pamoja? unaweza hata ukamfumania mke/mume na bado mkasameheana hasa mkikumbuka mema mengi mliyotendeana, sembuse ndita? you must fair guys, si kila wakat mnamind vitu vidogo vidogo mnatia doa mapenzi yenu bure.
 
Exactly Rutashubanyuma chukua kapu ukavune. Hakuna cha kusuluhisha hapo mdada hana raha mapenzini ndio maana anakunja ndita, mkaka shurti atafute sababu ya kukunjiwa ndita. Kama hawapeani raha ya nini kujitia karaha? Uamuzi wanao wenyewe
 
Last edited by a moderator:
Usiogope bana!!! kubembelezana kwa waliojaliwa mapenzi muhimu!!!

BAK kama wajua chanzo cha ndita zake.....pengine she has reached a point of no return.........
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom