Mdada anapomkunjia ndita ampendaye atarajie nini?

Mdada anapomkunjia ndita ampendaye atarajie nini?

Unajua kukunjiwa ndita bila ya sababu kunakera kuliko maelezo manake huyu mdada anahamisha matukio,kaboreka labda toka kwa ofisi basi ni mpaka nyumbani..sometime busara inabidi ichukue mkondo wake kwa hali kama hizi japo zinaweka mahusiano kwenye hatihati..
 
Yupo huyu mdada kweli anapendeza sanaaaaaa
Yupo huyu kijana kweli anampenda huyu mdada lol..
Penzi lao laelekea kuwaka na halina kizima moto lakini,
Upo mushkeli katika dimbwi la mahaba yao tarajiwa..
Mdada anapokunjia ndita ampendaye atarajie nini?

Sijui ana deko lipi huyu mdada badala ya kicheko
Kila amwonapo njemba wake huanza kukuda ndita!
Jambo aulizwapo huanza kujibu mazogo bila lengo
Kijana ameghafilika hajui anapendwa au anavumiliwa tu
Mdada anapokunjia ndita ampendaye atarajie nini?

Swahiba wa mdada wadai naye kashikwa pabaya
Ila hizo ni hadaa zake aonekane kama hajapenda sana
Khofu yake akionekana kafa pengine asije kufa kikwelikweli
Hana imani na kijana kama naye anampenda kiuthabiti
Mdada anapokunjia ndita ampendaye atarajie nini?

Njemba sasa imetosheka na udhia sasa yawasha mataa
Mdada kaghafirika hajui la kufanya kwani ndita siyo utu
Kibuti chanukia nami kuwasuluhisha nimeghairi kabisa
Waswahili husema wagombanapo ndugu chukua kapu ukavune
Mdada anapokunjia ndita ampendaye atarajie nini?

Sasa ndio njia unayotumia kutongozea?
 
Mkuu huyu mdada ana kisebusebu na .............!.
Na bila kujua alishaoza ndiyo maana kaghafirika hajui la kufanya.

Kyaiyembe kwenye mazingira ya namna hii ungelimshauri vipi mdada husika?
 
Last edited by a moderator:
akikunja ndita nami naweka makunyanzi usoni.

[MENTION]Philipo Kidwangwa[/MENTION] tatizo utakuwa umetumia mzinga kuua nyuki.....wakati "Doom" tu yatosha.......
 
Ruta Mwanamke hatakiwi amkunjie Mwanaume Ndita! Mwanamke anatakiwa Amrembulie Mwanaume!
[MENTION]
Ndallo[/MENTION] akikukunjia ndita utamsaidiaje ajirekebishe na kukuremburia?
 
Mwanamke anayekunja ndita hafai kutongozwa............... Duh kama mie wala haisimami kabisaaaa.............!
Jamani namaanisha miguu yangu haisimami nikikutana naye kwa sababu ya kuchoka......... Maana watu wenye tabia mbaya weshaanza kunielewa vibaya hapo juu....................LOL
 
Ruta Mwanamke hatakiwi amkunjie Mwanaume Ndita! Mwanamke anatakiwa Amrembulie Mwanaume!
Mkuu Ndallo wa siku hizi badala ya kurembua wanajiremba alafu wanajiona bora kwa urembo wa Salon.
Wanasahau kuwa dhana yote ya kujiremba ni ili wakirembua wawe mwake zaidi!
 
"Usiache mbachao kwa mswala upitao"
Alafu asiishi maisha ya mwaka arobaini na saba! maana atatoswa mara nyingi.
Na hajachelewa afanye mabadiliko nina hakika atayafurahia maisha ya kimahaba.
[MENTION]
Kyaiyembe[/MENTION] mara nyingi watu wa namna hii huwa hawajiamini kwa hiyo huzua rafu ambazo hazina utetezi..................anahitaji kuimarishwa kisaikolojia kabla hajaanza kuifaidi ndoa yake........
 
Mwanamke anayekunja ndita hafai kutongozwa............... Duh kama mie wala haisimami kabisaaaa.............!
Jamani namaanisha miguu yangu haisimami nikikutana naye kwa sababu ya kuchoka......... Maana watu wenye tabia mbaya weshaanza kunielewa vibaya hapo juu....................LOL
[MENTION]
Mtambuzi[/MENTION] hivi hujui wewe ya kuwa ng'ombe mkali ana maziwa matamu?
 
Unajua kukunjiwa ndita bila ya sababu kunakera kuliko maelezo manake huyu mdada anahamisha matukio,kaboreka labda toka kwa ofisi basi ni mpaka nyumbani..sometime busara inabidi ichukue mkondo wake kwa hali kama hizi japo zinaweka mahusiano kwenye hatihati..
[MENTION]
Iza[/MENTION] ni kweli lakini ushauri wa Freema Agyeman naona unatija kama tukiutafakari ya kuwa..............
 
Last edited by a moderator:
jamaa king'ang'anizi kama kupe mpaka unakunjiwa ndita upo tu!!! sasa subiri matumla af refa hakunaga kwenye penzi.
 
nimeipenda hii

kaka yangu nshomile, naomba chukua tano...
ukiona anakunja ndita nyumbani wala usihangaike,
we jua ni visirani, mikosi au kiburi...

lakini usisahau, siajabu una mwenza,
na sasa kulinganisha, ndio huwa kamtindo,
basi ulopungukwa, yeye hukunjia ndita,
usipoangalia kwa sana, utakunjiwa na midomo,
na tena so domo moja, bali yote iliyomo,
wa juu hata wa chini, na ukavu ukusute

njia moja yakufaa, kwa anayekunja ndita
we kunjua ako, na uende palo pema
jivutie na furaha, tena kwa kujituma
jifinyie kiso ndita, na utaaaamu ufaidi
 
Back
Top Bottom