Mchungaji Gwajima: Daudi Albert Bashite alipata division Zero

Sakata la Makonda

Najiuliza:-

1. Kwanza tangu lini MTU aliyepata div 0 akapata cheti cha Necta?

2. Gwajima ametoa wapi cheti chenye Zero wakati Serikali haitoi cheti hicho cha Zero?

3. Ni lini Baraza la mitihani limeanza kutoa vyeti kwa mtu yeyote aliyehitaji hata kama sio vyake?

4. Inawezekana vipi Watu wawili kumiliki vyeti original vya aina moja?

5. Watumishi wote wa umma na wa Serikali walifanyiwa zoezi la uhakiki wa vyeti, kama Gwajima alikuwa navyo vyeti original na ana uhakika Makonda anadanganya juu ya vyeti vyake alikuwa wapi kujitokeza kumuwekea pingamizi Makonda mpaka asubiri aguswe kwanza ndio aibuke?

Shilatu E. J
 
Jambo kubwa ni kuwa waungwana na kuachia ofisi ya Umma mkavue samaki maana nasikia mmesomea uvuvi ati, alaaa...kuendelea kushupaza shingo na kubishana na umma mtasababisha lile LIBASHITE likuu la Magogoni nalo PhD yake ifukunyuliwe, na mnajua hayuko salama kivile!
 
Reactions: Qj_
Yaan mtasema yote kumbe viongoz wengine wapo kwa ajili ya kuchafulia basi embu wekeni wazi
 
Kosa lingine Makonda anashindwa kuelewa anadhani anapambana na Gwajima as individual. Gwajima ni institution, ana waumini wengi sana. Lakini kuna watu wengi sana wako kinyume na Makonda wako serikalini, wengine ni watumishi, wengine ni wanasiasa, tena ambao wanajua details zote za mhusika. kwa hiyo wanachofanya kwa kuwa hawana uwezo wa kusema wao wenyewe, wanapeleka kwa Gwajima anapasua pwaaaaaaaaaaaaaaaah.
 
Hapo ndo najiuliza, huyu hawezi kweli kupunguza waumini kwa style hii ya kugeuza madhabahu kuwa sehemu ya mipasho ktk masala ya kisiasa?
 
Hili la Makonda limekwisha...nasubiri sasa ile PhD feki; Dr gani hawezi kuongea hata sentensi moja ya kimombo fasaha hadi anazidiwa na watoto wa Grade 1 pale St.Mary's?
Ni hatari kufukua kaburi maana utakuta marehemu bado ana harufu cjui utamkimbia akati unamfahamu. [emoji2]
 
Tokea lini div 0, akapewa certificate? Miaka hiyo anasoma Makonda mtu alipata div 0, kulikuwa hakuna cheti
Na hapo ndipo watz tulipofungwa akili zetu,tunafuata mkumbo tu,div 0 na cheti wapi na wapi?
 
gwajima ni docta....anawatibu wanaojitoa akili...
makonda kumbe mzito sanaaaa darasani..hivi vi..laza aliosema mkhulu sindo kama hawa....
alafu jamaa bashite anapenda shortcut sanaaa..kutoka kimaisha kwa shortcut..alafu tangu aoe tangu 2009,,hadi leo hana mtoto?????????????kulikoni bashitee
 
Fikria nje ya boks bas, hivi matokeo ya jumla yenye zero huachwa?

 
Uchungaji wa kipindi hiki hauhitaji hadi uwe na Elimu ya juu. Mtu akishakuwa na uwezo wa kuongea sana, kukemea mapepo na kuwa na mikakati ya kuweza kushawishi waumini watoe sadaka, basi unakuwa mchungaji. Mimi hakuna mchungaji ninayemtoa thamani kama huyu mchungaji Gwajima. Kama angekuwa na hicho cheti, basi angekitoa hadharani na kukionyesha humo kanisani mwake ili waumini wake wakione. sasa yeye bado analeta blaablaa.
 
CV ya hapa na pale!
 
Mkuu ukiishi na watu vizuri bila kuwaonea na kuwadhalilisha Hamna MTU hata mmona atakaetaka kujua mapungufu yako.....
Ukiwaumiza watu lazma watafute pa kukuumizaaaa
inamgharimu sana kwa jinsi ninavyoliona hili jambo
 
Vipo na miaka ya,kwa wale waliomaliza miaka 2003 kushuka walikuwa wanapewa ndo serikali ikasitisha na kuanza kuwanyima 2004 na kuendelea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…