THE BIG SHOW
JF-Expert Member
- Feb 28, 2012
- 18,543
- 14,803
mwana ccm pekee uliyebakiKuwa na aibu wewe, umenunua Cheti. Kila ukiulizwa unasema mtandao wa madawa wanakufatilia..!!
Kuwa na aibu wewe, unakitia aibu chama chetu..kosa siyo kupata ziro..kosa kwanini unatumia Cheti cha MTU. Humu mitandaoni tunaonekana ccm wote tunaakili za kibashitebashite. Haiwezekani ununuaji wako Cheti uharibu image ya chama na Rais: jiuzulu usitie aibu chama na Rais.
Mheshimiwa Rais mtoe huyu kijana inaonekana unadouble standard ..!! Sisi tumekupigia kura, haiwezekani wengine uwatumbue sembuse huyu. Rais huyu anaharibu image ya Urais. Ukimwacha utaleta mtikisiko bungeni.
Salaam wadau!
Huu mjadala hadi hivi sasa umefikia patamu, humu jamvini kumekuwa na nyuzi nyingi zinazohusu hili sakata la Mkuu wa mkoa wa Dsm kwamba alitumia vyeti ambavyo siyo vyake, kuna habari iliyoandikwa kwenye gazeti la mwanahalisi kuonyesha shule alizosoma na majina aliyokuwa akitumia na kubainisha alipata daraja zero kidato cha nne!
Hoja yangu ni je kama hizi tuhuma ni za kweli na hili suala likaachwa lipite kwa kupuuza hizi taarifa, nani atakayeweza kusimama kidete na kuzungumzia vyeti feki?
Je huko serikalini siyo kwamba kwenye sekta nyeti kuna watu wanaotumia majina ya watu wengine lakin zoezi la uhakiki halikuwagusa?
Nashauri mamlaka husika ziingilie kati bila kujali cheo cha mtu, la sivyo itakuwa ni fedheha kubwa siyo tu kwa mamlaka bali kwa taifa zima
Hapa Ben Saanane hausiki, swala Saudi Bashite aweke vyeto vyake mezani lazima tuvihakikiHakuna kesi ya kuingilia kati hapo.Blah blah tupu.Ungeshauri Ben Saanane atafutwe kwa nguvu zote ungeonekana wa maana badala ya kuzungumzia suala ambalo halipo
Kweli wewe punguani
Hivi kuna aliyethibitisha kwa kuvionyesha hivyo vyeti?Au bado tunamsubiri Gwajima avionyeshe?Kweli ni aibu kubwa. Afu kuna mijitu hata humu inatetea. Watu wameondelewa makazini kwa kutumia vyeti vya kugushi. Mkuu wa mkoa failure anapeta na vyeti vya kugushi
uhakiki wewe kama nani acha upuuziHapa Ben Saanane hausiki, swala Saudi Bashite aweke vyeto vyake mezani lazima tuvihakiki
Hivi unafahamu kuwa katika muda huu kuna majaji wanne, wapo kazini, huku wawili wakikabiliwa na tuhuma za kuwasaidia wauza unga na wawili wakiwa miongoni mwa waliopokea mgao wa Tegeta Escrow? Ukidhafahamu hilo huenda ukaanza kuwekeza nguvu zako katika masuala ya maendeleo yako binafsi kuliko kujipa matumaini hewa kuhusu "kutumbuliwa kwa Makonda."Salaam wadau!