Mchungaji Anthony Lusekelo: TB Joshua ni tapeli

Amri kuu kuliko yote aliyotuambia Bwana wetu Yesu Kristu nu UPENDO. Upendo haubagui,hauna visa,visasi wala chuki. Mwenzako akikukosea,muombee.
Naona Lusekelo amesahau huu msingi mkuu wa dini ya kikristu. Amekuwa akitoa matamshi makali kwa watu mbali mbali yenye lengo la kuharibu badala ya kujenga. Akumbuke kuwa kazi za shetani ni kuu 3. Kuua,kuharibu na kuiba. Matamshi yake Lusekelo yanamfanya afuate kazi za muovu shetani na siyo na Mkombozi wetu,Yesu Kristu.
Jukumu letu ni kumuombea huyu baba. Ajue wito wake. Inawezekana kabisa akawa anafanya kazi ambayo hana wito nayo. Au pengine aliacha mlango wazi ambao adui alipita na kumfanya akengeuke.
Neema ya Mungu na itawale
 
Mzee wa upako, hana washauri au? Sina tatizo na Huduma yake. Mengine ni tabia tu.
Ila angepanga safu ya washauri wake kuliko kuwa One man show...sawa ministry kaanzisha yeye....ila sasa ni taasisi...inabidi mambo mengine apate ushauri kwa walio pembeni yake, kabla hajaenda media, au kuyatoa hadharani , hasa mambo yasiyohusu mahubiri ya kiinjili.
 
Ni vizuri shetani anaanza kuwasaliti ...yafanyikayo gizani shetani utafuta ukuu kwa kuyaanika wazi huku akikuacha uabike

This is Good
 
Mchungaji wa Kanisa la Maombezi GRC la jijini Dar es salaam, Anthony Lusekelo maarufu kama 'Mzee wa Upako' ametema cheche kwa Nabii maarufu kutoka Nigeria TB Josua wa Kanisa la SCOAN kuwa ni tapeli na kusisitiza kuwa hapaswi kuaminiwa kwa lolote.

View attachment 469048

Akijibu maswali katika kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa LIVE kila Jumatano kupitia ukurasa wa facebook wa EATV, Mch. Lusekelo amesema kuwa Nabii TB Joshua ni tapeli kwani alikwisha tabiri uchaguzi wa Marekani kuwa Bi. Hillary Clinton atashinda lakini matokeo yakawa tofauti na utabiri pamoja na uchaguzi wa Tanzania alikosea kutabiri ushindi katika uchaguzi mkuu uliofanyika 2015.

Aidha Lusekelo amezidi kupigilia msumari huo kwa kudai kuwa TB Joshua hana unabii unaosomwa kwenye biblia kama kina nabii Elisha, Eliya na wengineo ambao walikuwa na uwezo wa kuona vita au maadui kabla hata hawajakaribia katika maeneo ya ufalme.

"Yule ni tapeli kwa sababu nchini kwake kuna wale mabinti waliotekwa kipindi kile mpaka leo ameshindwa kuwakomboa sasa mtu kama huyo unamuamini vipi? si mliona alimtabiria yule mama Hillary atakuwa Rais lakini akakosea hata hapa nchini si alitabiria watu watano watakuwa marais katika hali ya kawaida nchi itaongozwaje na marais wote hao ?" alihoji Mzee wa upako

Lusekelo aliongeza pia kuwa siyo kila mtu anaweza kuwa nabii huku (bila kuziweka hadharani) akisema unabii unahatua zake na sifa zake ambazo TB Joshua hana na ndiyo maana alishindwa hata kuona kuwa jengo la kanisa lake linaelekea kuanguka na badala yake akaacha watu wakapoteza maisha huku yeye akienda Afrika Kusini.
Mzee wa upako anamfahamu TB Joshua ila sina hhakika kama TB Joshua anafahamu kitu inaitwa Mzee wa Upako.
 
Kaka ilikuwa ni tarahe ngapi ya march? lazima tuweke kumbukumbu hapa!

Mie ni DADA, kuhusu tarehe kamili siijui ila alisema kuwa kufika March, 2017 wote waliomwandika vibaya wataaga dunia, wasipokufa basi yeye ataenda kuuza gongo
 
Chuki tu hizo sababu Joshua ana mshiko wa maana unajua Mzee wa upako siyo level ya Joshua yeye adeal na kina Mwingira ,Kakobe hata Gwajima siyo level yake
 
Mchungaji wa Kanisa la Maombezi GRC la jijini Dar es salaam, Anthony Lusekelo maarufu kama 'Mzee wa Upako' ametema cheche kwa Nabii maarufu kutoka Nigeria TB Josua wa Kanisa la SCOAN kuwa ni tapeli na kusisitiza kuwa hapaswi kuaminiwa kwa lolote.

View attachment 469048

Akijibu maswali katika kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa LIVE kila Jumatano kupitia ukurasa wa facebook wa EATV, Mch. Lusekelo amesema kuwa Nabii TB Joshua ni tapeli kwani alikwisha tabiri uchaguzi wa Marekani kuwa Bi. Hillary Clinton atashinda lakini matokeo yakawa tofauti na utabiri pamoja na uchaguzi wa Tanzania alikosea kutabiri ushindi katika uchaguzi mkuu uliofanyika 2015.

Aidha Lusekelo amezidi kupigilia msumari huo kwa kudai kuwa TB Joshua hana unabii unaosomwa kwenye biblia kama kina nabii Elisha, Eliya na wengineo ambao walikuwa na uwezo wa kuona vita au maadui kabla hata hawajakaribia katika maeneo ya ufalme.

"Yule ni tapeli kwa sababu nchini kwake kuna wale mabinti waliotekwa kipindi kile mpaka leo ameshindwa kuwakomboa sasa mtu kama huyo unamuamini vipi? si mliona alimtabiria yule mama Hillary atakuwa Rais lakini akakosea hata hapa nchini si alitabiria watu watano watakuwa marais katika hali ya kawaida nchi itaongozwaje na marais wote hao ?" alihoji Mzee wa upako

Lusekelo aliongeza pia kuwa siyo kila mtu anaweza kuwa nabii huku (bila kuziweka hadharani) akisema unabii unahatua zake na sifa zake ambazo TB Joshua hana na ndiyo maana alishindwa hata kuona kuwa jengo la kanisa lake linaelekea kuanguka na badala yake akaacha watu wakapoteza maisha huku yeye akienda Afrika Kusini.
kwa mjinga asiye na akili ndo atakubali kuwa karne hii ya 21 atatokea kiumbe nae atakua mtume mwenye akili ashtuki acha wapigwe ata wewe nyote ni walewale muogopeni Mungu acheni utapeli
 
Siku yaja....Bwana nilitoa pepo kwa jina lako naye atajibu....TOKENI KWANGU SIWAJUI. Kabla ya kuangalia kibanzi kilicho kwenye jicho la mwenzako toa kwanza 2x2 yako.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom