Au mnasubiri mpaka KKKT waseme neno? Unanikumbusha mambo ya Lowassa na walutheri 2015 kule Tabora. Maana ukianza na Lowassa, Mbowe, Sumaye wote wa KKKT.
Kwa sasa Mwenyekiti wa Umoja wa Jukwaa ka Kikristu ni Askofu Mkuu wa Lutheran.Na ndiyo msemaji Mkuu wa Jukwaa hilo.Ndiyo sababu ninemuongelea
RAHA SANA, NAWAPENDA WASEMAO YESU ANAWEZA YOTE LAKINI WANATEMBEA NA BASTOLA KIUNONI.
Mwisho wa ubaya ni aibu , kiko wapi sasa mkuu Lusekelo ?MCHUNGAJI ANTONY LUSEKELO MAARUFU KAMA MZEE WA UPAKO AMEWATAKA WAPINZANI WASIVURUGE AMANI YA NCHI YETU.
Mzee wa upako aliyasema hayo katika Ibada takatifu tarehe 18 September 2016 na baadae, mahubiri hayo kurushwa hewani na Channel ten tarehe 22 September 2016.
Mchungaji Lusekelo aliwaambia waumini wake kuwa kwa sasa maisha yanaenda vizuri na Rais Magufuli anafanya tulichokuwa tunataka kwa miaka mingi kusimamia nidhamu ya watumishi wa umma.
Kuhusu suala la pesa kukosekana mtaani Mchungaji Lusekelo alisema ninanukuu "Pesa zipo mtaani kama kawaida lakini kwa watu wanaofanya kazi na sio wavivu, na zamani pesa zilizagaa kwa sababu ya ubadhirifu wa mali za umma" pia kasema yeyote anayelalamika ni yule aliyekuwa anapata pesa kwa njia zisizo halali.
Katika hatua nyingine Mchungaji Lusekelo alimtaka Dr.Magufuli asisumbuke kubadili pesa za nchi kwani fedha zipo mtaani na maisha ni mazuri tu hakuna ugumu wowote.
Pia aliwataka waumini wake wasijaribu kushiriki katika maandamano yeyote yale na wala wasidanganyike kuchezea amani ya nchi kwa watu wenye uroho wa madaraka na kuwadanganya kuwa Magufuli kabana demokrasia wakati sio sahihi kabisa.
Mchungaji Lusekelo, alitoa mifano miwili ili kuwaelimisha waumini wake, wa kwanza ni nchi ya Gaboni mzee wa upako aliwaambia nchi hii imeharibiwa na watu wasiozidi elfu 3,000 kwa kuingia barabarani na kuanzisha maandamano na sasa nchi ile imevurugika.
Mfano mwingine katolea nchi ya Brazili, kuwa Taifa hili limevurugwa na watu wasiozidi elfu 10,000 baada ya kuingia barabarani na kuandamana na kusababisha machafuko na nchi kutotawalika.
Mzee wa upako alilaaani vikali oparesheni UKUTA iliyokuwa imetangazwa kufanyika tarehe moja September mwaka huu kwa kusema, ilisababisha Taifa kukosa watalii kuja kuangalia kupatwa kwa jua kule Mbeya kwa kuhofia machafuko nchini nakuwataka wapinzani wasirudie kitendo hiki.
Mwisho Mzee wa upako ametangaza kutumbua majipu mpaka kanisani na ikiwezekana kukata mguu wenye jipu ili jipu litoke na mtu aweze kuishi, baada ya hapo alimalizia kwa kuimba wimbo wa Tanzania.
Hongera sana mchungaji Lusekelo hakika umenena vyema.
Imeandaliwa na wenu,
MWITA NYARUKURURU
hahahah et hongera wakati unajua kabisa kanisani si pa siasa na kila mtu ana uhuru wake hivyo hata kama akiwaambia nini kila mtu atachanganya na za kwake maana si lazima uchukue za kuambiwa.mtahema sana kipindi hiki kutoa elimu hata kusiko takiwa kama chama kimekufa mihemko na hekaheka za nini si itakua kama mnampigia mbuzi gitaa mnahangaika na mfu ?hahahaha shame on you kweli mfa maji haach kutapatapa.kaeni kimya basi muone mnajihami ya nini?Hongera sana Mch Lusekelo a.k.a Transformer! Ingawa kanisani si pa hala pa siasa ila ni muhimu kuwaelewesha kwani amani ikikosekana hata wewe huwezi kutoa huduma. cc BAK, Daudi Mchambuzi, Nyani Ngabu na wale wanafiki wote wa kila chama kilichokufa siku nyingi
Bwana amuhurumie tu.Mwisho wa ubaya ni aibu , kiko wapi sasa mkuu Lusekelo ?
Km mamvi?Tapeli tuu ilo
si ya bbusara hata kama ni mahaba niue.Hakuna kizuri kisicho na kasoro yeye pia ana mapungufu yake hivyo wanaokosoa ndo wanaona.we kama unamwona mzuri mkeo au mmeo usilazimishe mwengine kumwona hivyo.Hii nchi ilikuwa inaumwa sasa dokta magufuli anaitibu (isingeweza kutibiwa na mgonjwa ila dokta) sasa dozi yake ni kali,wapo watakaoweza kuvumilia machungu ili kupona lakini wapo ambao kwao bora waepuke dozi kali waendelee kuumwa.
Namshauri dokta magufuli asimamie profesheno yake vizuri asimamie dozi mpaka ugonjwa upotee.
Hapo wanaolalamika watakukimbilia dokta ili wakubusu kwakuwa umewapa maisha
Note; mwanaume aliyetahiriwa na mwanamke aliyezaa anajua kuvumilia maumivu ili kukamilisha uanaume/uanamke wake...Wamebaki manungayembe wanapaparika! Hapa kazii juu!
ha ha ha ha sitaki kusema sana aiseeMchungaji hawezi hata kutoa pepo
mamvi ndo nani?Km mamvi?
We bwana wee!!!Mchungaji hawezi hata kutoa pepo
CCM mmemtumia weeee ! Sasa baada ya kukutwa yuko njwiiii mnamkana !Mauaji ya kimbari Rwanda yalianzia kwa hizi hotuba za makanisani.