Mchungaji Anthony Lusekelo awapa onyo CHADEMA

embu tujiulize maswali tukiwa sober kidogo - no politicking!

kwa hiyo ina maana Lusekelo ameitapeli hadi serekali iliyoahidi kumjengea barabara? kwa hiyo serekali yetu ni naïve kiasi cha kutapeliwa hata na "mlevi"?

napata woga sasa na hata hizi ziara za watu kama mfalme wa Morocco, rais wa Vietnam, nk - hawa wanaonekana wapo sober, sasa mtu sober na mlevi ni yupi mwenye uwezo wa kutengeneza utapeli wenye madhara zaidi kwetu?
 
MCHUNGAJI ANTONY LUSEKELO MAARUFU KAMA MZEE WA UPAKO AMEWATAKA WAPINZANI WASIVURUGE AMANI YA NCHI YETU.

Mzee wa upako aliyasema hayo katika Ibada takatifu tarehe 18 September 2016 na baadae, mahubiri hayo kurushwa hewani na Channel ten tarehe 22 September 2016.

Mchungaji Lusekelo aliwaambia waumini wake kuwa kwa sasa maisha yanaenda vizuri na Rais Magufuli anafanya tulichokuwa tunataka kwa miaka mingi kusimamia nidhamu ya watumishi wa umma.

Kuhusu suala la pesa kukosekana mtaani Mchungaji Lusekelo alisema ninanukuu "Pesa zipo mtaani kama kawaida lakini kwa watu wanaofanya kazi na sio wavivu, na zamani pesa zilizagaa kwa sababu ya ubadhirifu wa mali za umma" pia kasema yeyote anayelalamika ni yule aliyekuwa anapata pesa kwa njia zisizo halali.

Katika hatua nyingine Mchungaji Lusekelo alimtaka Dr.Magufuli asisumbuke kubadili pesa za nchi kwani fedha zipo mtaani na maisha ni mazuri tu hakuna ugumu wowote.

Pia aliwataka waumini wake wasijaribu kushiriki katika maandamano yeyote yale na wala wasidanganyike kuchezea amani ya nchi kwa watu wenye uroho wa madaraka na kuwadanganya kuwa Magufuli kabana demokrasia wakati sio sahihi kabisa.

Mchungaji Lusekelo, alitoa mifano miwili ili kuwaelimisha waumini wake, wa kwanza ni nchi ya Gaboni mzee wa upako aliwaambia nchi hii imeharibiwa na watu wasiozidi elfu 3,000 kwa kuingia barabarani na kuanzisha maandamano na sasa nchi ile imevurugika.

Mfano mwingine katolea nchi ya Brazili, kuwa Taifa hili limevurugwa na watu wasiozidi elfu 10,000 baada ya kuingia barabarani na kuandamana na kusababisha machafuko na nchi kutotawalika.

Mzee wa upako alilaaani vikali oparesheni UKUTA iliyokuwa imetangazwa kufanyika tarehe moja September mwaka huu kwa kusema, ilisababisha Taifa kukosa watalii kuja kuangalia kupatwa kwa jua kule Mbeya kwa kuhofia machafuko nchini nakuwataka wapinzani wasirudie kitendo hiki.

Mwisho Mzee wa upako ametangaza kutumbua majipu mpaka kanisani na ikiwezekana kukata mguu wenye jipu ili jipu litoke na mtu aweze kuishi, baada ya hapo alimalizia kwa kuimba wimbo wa Tanzania.

Hongera sana mchungaji Lusekelo hakika umenena vyema.
Imeandaliwa na wenu,
MWITA NYARUKURURU
Wakati anasema haya je kile kinywaji kikali Alikuwa amekunywa?
 
Mura
 
Muulizeni leo akitoka polisi ndiyo akili itakuwa sawa. Nadhan kwenye ibada takatifu alikuwa tungi.
 
Ji-bapa la Konyagi ni hatari kwa usalama wa ubongo
 
Mupa! ,MUpatie!, Muruke! Tingisa kama imekwisha!!! Njo vilee papaa!!!!
 
Usitukane mamba kabla hujavuka mto jamani, au nyie ni watakatifu kivile?
 
Back
Top Bottom