Mchungaji Anthony Lusekelo awapa onyo CHADEMA

Mchungaji Anthony Lusekelo awapa onyo CHADEMA

Mbona inafahamika kitambo , unajua kosa kubwa tunalolifanya ni kuwafichia siri zao hawa wanafiki .
Nyie ndo mnaochelewesha mabadiliko.Mkuu kama kuna jambo kama hilo lenye ushahidi wekeni hadharani ili wananchi wajue kinachoendelea.
 
MCHUNGAJI ANTONY LUSEKELO MAARUFU KAMA MZEE WA UPAKO AMEWATAKA WAPINZANI WASIVURUGE AMANI YA NCHI YETU.

Mzee wa upako aliyasema hayo katika Ibada takatifu tarehe 18 September 2016 na baadae, mahubiri hayo kurushwa hewani na Channel ten tarehe 22 September 2016.

Mchungaji Lusekelo aliwaambia waumini wake kuwa kwa sasa maisha yanaenda vizuri na Rais Magufuli anafanya tulichokuwa tunataka kwa miaka mingi kusimamia nidhamu ya watumishi wa umma.

Kuhusu suala la pesa kukosekana mtaani Mchungaji Lusekelo alisema ninanukuu "Pesa zipo mtaani kama kawaida lakini kwa watu wanaofanya kazi na sio wavivu, na zamani pesa zilizagaa kwa sababu ya ubadhirifu wa mali za umma" pia kasema yeyote anayelalamika ni yule aliyekuwa anapata pesa kwa njia zisizo halali.

Katika hatua nyingine Mchungaji Lusekelo alimtaka Dr.Magufuli asisumbuke kubadili pesa za nchi kwani fedha zipo mtaani na maisha ni mazuri tu hakuna ugumu wowote.

Pia aliwataka waumini wake wasijaribu kushiriki katika maandamano yeyote yale na wala wasidanganyike kuchezea amani ya nchi kwa watu wenye uroho wa madaraka na kuwadanganya kuwa Magufuli kabana demokrasia wakati sio sahihi kabisa.

Mchungaji Lusekelo, alitoa mifano miwili ili kuwaelimisha waumini wake, wa kwanza ni nchi ya Gaboni mzee wa upako aliwaambia nchi hii imeharibiwa na watu wasiozidi elfu 3,000 kwa kuingia barabarani na kuanzisha maandamano na sasa nchi ile imevurugika.

Mfano mwingine katolea nchi ya Brazili, kuwa Taifa hili limevurugwa na watu wasiozidi elfu 10,000 baada ya kuingia barabarani na kuandamana na kusababisha machafuko na nchi kutotawalika.

Mzee wa upako alilaaani vikali oparesheni UKUTA iliyokuwa imetangazwa kufanyika tarehe moja September mwaka huu kwa kusema, ilisababisha Taifa kukosa watalii kuja kuangalia kupatwa kwa jua kule Mbeya kwa kuhofia machafuko nchini nakuwataka wapinzani wasirudie kitendo hiki.

Mwisho Mzee wa upako ametangaza kutumbua majipu mpaka kanisani na ikiwezekana kukata mguu wenye jipu ili jipu litoke na mtu aweze kuishi, baada ya hapo alimalizia kwa kuimba wimbo wa Tanzania.

Hongera sana mchungaji Lusekelo hakika umenena vyema.
Imeandaliwa na wenu,
MWITA NYARUKURURU




HIZI NDO RANGI ZA CCM HALISI LEO UMEJIPAMBAMBANUA SI ULIANZISHA THREAD YA KUMPONDA YULE PADRI ALIEMKOSOA MAGUFULI WEWE NCHI IMEJAA WANAFIKI KILA KONA HII.
 
Mchungaji hawezi hata kutoa pepo
Sio kutoa Pepo tuu .yeye mwenyewe anapepo la tama ya pesa .mchungaji gani anatunzwa pesa katikati ya mahubiri kama waimba taarabu .ashindwa na alegee katika Jina la Yesu
 
Anafananisha urahisi wa wa yeye kukinga mikono madhabauni na kupokea na maisha yetu ya kufuja jasho. Bora angekaa kimya kuficha ujinga wake
 
Huyu si mwizi kama wezi wengine, anafanya nini kama sio kuwaibia watu. Eti anaomba, si aende Muhimbili mortuary aombe wafu wafufuke. Anadanganya wagumba, mahanisi eti atawaponya, si akaponye watu Ocean road cancer institute
Unadhani hospitali hazikuwepo wakati wa Yesu, Unadhani yesu hakukutana na makaburi yaliyolala wafu??
 
Hii nchi ilikuwa inaumwa sasa dokta magufuli anaitibu (isingeweza kutibiwa na mgonjwa ila dokta) sasa dozi yake ni kali,wapo watakaoweza kuvumilia machungu ili kupona lakini wapo ambao kwao bora waepuke dozi kali waendelee kuumwa.

Namshauri dokta magufuli asimamie profesheno yake vizuri asimamie dozi mpaka ugonjwa upotee.
Hapo wanaolalamika watakukimbilia dokta ili wakubusu kwakuwa umewapa maisha

Note; mwanaume aliyetahiriwa na mwanamke aliyezaa anajua kuvumilia maumivu ili kukamilisha uanaume/uanamke wake...Wamebaki manungayembe wanapaparika! Hapa kazii juu!
 
HII NCHI ILIKUWA INAUMWA SASA DOKTA MAGUFULI ANAITIBU (ISINGEWEZA KUTIBIWA NA MGONJWA ILA DOKTA) SASA DOZI YAKE NI KALI,WAPO WATAKAOWEZA KUVUMILIA MACHUNGU ILI KUPONA LAKINI WAPO AMBAO KWAO BORA WAEPUKE DOZI KALI WAENDELEE KUUMWA. NAMSHAURI DOKTA MAGUFULI ASIMAMIE PROFESHENO YAKE VIZURI ASIMAMIE DOZI MPAKA UGONJWA UPOTEE.
HAPO WANAOLALAMIKA WATAKUKIMBILIA DOKTA ILI WAKUBUSU KWAKUWA UMEWAPA MAISHA...
NOTE; MWANAUME ALIYETAHIRIWA NA MWANAMKE ALIYEZAA ANAJUA KUVUMILIA MAUMIVU ILI KUKAMILISHA UANAUME/UANAMKE WAKE...wamebaki manungayembe wanapaparika! Hapa kazii juu! Shiii............t
. sawa kabisa na LUSEKELO YUKOSAWA kilamtu anahaki kuexpress his/her feelings bila kudhihakiwa Bali kupingwa kwa hoja
 
Kwakua yeye anakaa pale ofsin kwake waumin wanapambana wanamletea ndo maana anaona mzunguko uko smwelew pale anaposema hmna ugumu wa maisha ingekuwa makanisa yao wana dayosisi na mambo mengine angejua huo mzunguko ukwapi kwan kuna sadaka zamaendleo ya mtaa fungu la dayosis fungu la kila kitu af % kidogo ndo inabk kwajili ya dhughuli za kanisa wsngeona umuhimu ila kwakua yeye ndo dayosisi yeye ndo kila kitu


Waumin wa hya makanisa wafunguke kwani huko ni kuji suicide
 
Kwa kiongozi mkubwa wa kiroho kama huyu astahili kusema maneno kama hayo kwa sababu nyuma yake kuna Waumin wengi wa kada tofauti wanaomfuata kwan wapo watakaomuunga na wapo watakaompinga hivyo asingeyasema publically,
 
Back
Top Bottom