MCHUNGAJI ANTONY LUSEKELO MAALUFU KAMA MZEE WA UPAKO AMEWATAKA WAPINZANI WASIVURUGE AMANI YA NCHI YETU.
Mzee wa upako aliyasema hayo katika Ibada takatifu tarehe 18september 2016 na baadae, mahubiri hayo kurushwa hewani na channel ten tarehe 22 September 2016.
Mchungaji Lusekelo aliwambia wahumini wake kuwa kwasasa maisha yanaenda vizuri na Rais Magufuli anafanya tulichokuwa tunataka kwa miaka mingi kusimamia nidhamu ya watumishi wa umma.
Kuhusu swala la pesa kukosekana mtaani Mchungaji Lusekelo alisema nina nukuu "Pesa zipo mtaani kama kawaida lakini kwa watu wanaofanya kazi na sio wavivu, na zamani pesa zilizagaa kwa sababu ya ubadhilifu wa mali za umma" pia kasema yeyote anayelalamika ni yule aliyekuwa anapata pesa kwa njia zisizo halali.
Katika hatua nyingine Mchungaji Lusekelo alimtaka Dr.Magufuli asisumbuke kubadili pesa za nchi kwani fedha zipo mtaani na maisha ni mazuri tu hakuna ugumu wowote.
Pia aliwataka waumini wake wasijaribu kushiriki katika maandamano yeyote Yale na wala wasidanganyike kuchezea amani ya nchi kwa watu wenye uroho wa madaraka na kuwadanganya kuwa Magufuli kabana demokrasia wakati sio sahihi kabisa.
Mchungaji Lusekelo, alitoa mifano miwili ili kuwaelimisha wahumini wake, wa kwanza ni nchi ya Gaboni mzee wa upako aliwambia nchi hii imehalibiwa na watu wasiozidi elfu 3,000 kwa kuingia barabarani na kuanzisha maandamano na sasa nchi ile imevulugika.
Mfano mwingine katolea nchi ya Brazili, kuwa Taifa hili limevulugwa na watu wasiozidi elfu 10,000 baada ya kuingia barabarani na kuandamana na kusababisha machafuko na nchi kutotawalika.
Mzee wa upako alirahani vikali opalesheni Ukuta iliyokuwa imetangazwa kufanyika tarehe moja September mwaka huu kwakusema, ilisababisha Taifa kukosa watalii kuja. kuangalia kupatwa kwa jua kule Mbeya kwakuhofia machafuko nchini nakuwataka wapinzani wasirudie kitendo hiki.
Mwisho Mzee wa upako ametangaza kutumbua majipu mpaka kanisani na ikiwezekana kukata mguu wenye jipu ili jipu litoke na mtu aweze kuishi, baada ya hapo alimalizia kwakuimba wimbo wa Tanzania.
Hongera sana mchungaji Lusekelo hakika umenena vyema.
Imeandaliwa na wenu,
MWITA NYARUKURURU