Ni mshirikina tu hana lolote huyo ngoja viongozi wa chadema wafukue madhambi yake atajuuta kuwafahamu.Tangu mtukufu rais aende kanisani kwake basi imekuwa shida
Kwani hata kodi analipa kulingana na mapato yake?Hivi zile hela anazokusanya huwa anatangaza mapato na matumizi?
Kama zinakusanywa kwenye camera,kwanini mapato na matumizi hatujawahi yasikio/yaona?
Mda mwingi anajipendekeza hawezi kuthubutu kumshauri Rais chochote kile.Kama tunazungumzia uchochezi basi Lusekelo ni mchochezi namba moja.
JE itakuwaje iwapo kila anayejiita kiongozi wa kidini wakitoa matamko ya kisiasa kama ya huyu Bw.Lusekelo?
Ninaamini viongozi wa dini wanapaswa kutokuwa na upande katika mambo ya kisiasa isipokuwa wanatakiwa kutetea wananchi pale haki zao zinapominywa.
Nilitegemea Lusekelo angetumia ukaribu wake na Rais kumshauri Rais aruhusu vyama vyote vifanye siasa kwa mujibu wa katiba.
Kwahio nyie CHADEMA ambao mnasema Serikali inaminya uhuru wa kujieleza mmeanza lini kupangia watu waseme nini na waache nini?Mchungaji Lusekelo ni kiongozi wa kiroho, maneno anayohubiri kwa waumini wake ni dogmatic statements........ hayahojiwi!!!! Ushauri: asipende sana kuzungumzia mambo ambayo ni ya kisiasa na kutoa vule judgements. Yeye ahubiri, aonye, na kutoa maelekezo bila kuzungumzia dialogue za kisiasa zinazoendela
du! kujipendekeza kwingine hatari sana....MCHUNGAJI ANTONY LUSEKELO MAARUFU KAMA MZEE WA UPAKO AMEWATAKA WAPINZANI WASIVURUGE AMANI YA NCHI YETU.
Mzee wa upako aliyasema hayo katika Ibada takatifu tarehe 18 September 2016 na baadae, mahubiri hayo kurushwa hewani na Channel ten tarehe 22 September 2016.
Mchungaji Lusekelo aliwaambia waumini wake kuwa kwa sasa maisha yanaenda vizuri na Rais Magufuli anafanya tulichokuwa tunataka kwa miaka mingi kusimamia nidhamu ya watumishi wa umma.
Kuhusu suala la pesa kukosekana mtaani Mchungaji Lusekelo alisema ninanukuu "Pesa zipo mtaani kama kawaida lakini kwa watu wanaofanya kazi na sio wavivu, na zamani pesa zilizagaa kwa sababu ya ubadhirifu wa mali za umma" pia kasema yeyote anayelalamika ni yule aliyekuwa anapata pesa kwa njia zisizo halali.
Katika hatua nyingine Mchungaji Lusekelo alimtaka Dr.Magufuli asisumbuke kubadili pesa za nchi kwani fedha zipo mtaani na maisha ni mazuri tu hakuna ugumu wowote.
Pia aliwataka waumini wake wasijaribu kushiriki katika maandamano yeyote yale na wala wasidanganyike kuchezea amani ya nchi kwa watu wenye uroho wa madaraka na kuwadanganya kuwa Magufuli kabana demokrasia wakati sio sahihi kabisa.
Mchungaji Lusekelo, alitoa mifano miwili ili kuwaelimisha waumini wake, wa kwanza ni nchi ya Gaboni mzee wa upako aliwaambia nchi hii imeharibiwa na watu wasiozidi elfu 3,000 kwa kuingia barabarani na kuanzisha maandamano na sasa nchi ile imevurugika.
Mfano mwingine katolea nchi ya Brazili, kuwa Taifa hili limevurugwa na watu wasiozidi elfu 10,000 baada ya kuingia barabarani na kuandamana na kusababisha machafuko na nchi kutotawalika.
Mzee wa upako alilaaani vikali oparesheni UKUTA iliyokuwa imetangazwa kufanyika tarehe moja September mwaka huu kwa kusema, ilisababisha Taifa kukosa watalii kuja kuangalia kupatwa kwa jua kule Mbeya kwa kuhofia machafuko nchini nakuwataka wapinzani wasirudie kitendo hiki.
Mwisho Mzee wa upako ametangaza kutumbua majipu mpaka kanisani na ikiwezekana kukata mguu wenye jipu ili jipu litoke na mtu aweze kuishi, baada ya hapo alimalizia kwa kuimba wimbo wa Tanzania.
Hongera sana mchungaji Lusekelo hakika umenena vyema.
Imeandaliwa na wenu,
MWITA NYARUKURURU
sitii neno juu ya mpakwa mafuta wa Bwana
Njaa itamfanya huyu mchungaji awe mwehuAmekua sendeka sawa ahubili siasa
Nadhani wanatoa sadaka na ile kumtuza ni nyongeza kwa anayejisikia kufanya hivyo!Katika huduma yake hawatoi sadaka bali waumini wanamtunza kama wafanyavyo Jahazi Modern Taarab
Pale ni kama unalipia siti,ukiingia unaulizwa una shilingi ngapi then unapewa siti accordingly wenye kiasi kikubwa mbele.Hiyo ilikuwa zamani lakini sijajua kama utaratibu umebadilikaNadhani wanatoa sadaka na ile kumtuza ni nyongeza kwa anayejisikia kufanya hivyo!
Tulivyoualika kwenye kikao cha chadema na ukawa pale Mlimani city kuelekea uchaguzi mkuu mwaka jana hatukujua haya yote. Mbona tulishangilia wote.Mchungaji gani, jizi tu linakula kwa wajinga. Wenye shida za ugumba, uhanisi masikini wa natafuta faraja.