Mchungaji akutwa akizini na binti wa kaka yake

Mchungaji akutwa akizini na binti wa kaka yake

Status
Not open for further replies.
Shetani ni mjanja sana wengi wanazidiwa ujanja na shetani sio mchungaji peke yake
dunia imeisha,tumwamini nani sasa kama mtu wa Mungu ndiye anakuwa kiongozi wa maasi tena kwa bintiye!!!
 
Tupo kwenye siku za mwisho, sishangai kwa mambo kama haya kuwepo.
 
Ibilisi katika ubora wake.Na kwa kuwa ibilisi ameshachezea akili zetu na kutufanya MAZUZU na MAHAYAWANI kiasi kwamba mambo ya hovyo,machafu na ya aibu kwetu yamekuwa mazuri na yenye kupendeza,matukio ya namna hii yataongezeka maradufu.Angalia jibu la huyo binti na jibu la huyo mchungaji;utagundua tu kwamba AKILI ZAO HAZIKO SALAMA ingawa ziko timamu.
 
Shetani ni mjanja sana wengi wanazidiwa ujanja na shetani sio mchungaji peke yake
Shetani anasingiziwa mambo mengi sana, sidhani kama kila kosa ni shetani kwa dunia hii chafu ya leo
 
Teh teh teh.
Maalim Mahmood mbavu zangu huku!
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] .
Hawa makafiri ni Balaa wallah.

Yaani Kuzini na watoto wai ni km sisi kunywa gahwa na Tende.
Watu wa ajabu sana kutetea upuuzi huu wanaamini mchungaji rukhsa kufanya lolote hata akisema laleni wote sawa tu
 
Mwaka mzima, akapigwa fine Tshs 20,000?

Kweli Elimu inatakiwa ipewe kipaumbele cha hali ya juu. Mungu gani huyo anayeruhusu mtumishi wake kuombea wenzie ukichaa kisa uzinzi?

Aliyeandika kwamba watu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa, hakukosea. ....

Mwisho,
Hizi sheria za mtaani itabidi ziangaliwe upya. ..
Hako kabinti nako kalipenda tu kanaona mambo yamesanuka ndio kanazuga eti kaliambiwa kataombewa kuwa kichaa! si ajabu hata huyo mtoto wa miezi 4 ni wao sababu akienda nje na mtoto ananyonya huwa mtoto anadhurika. Ni kahuni tu.
 
Ole wake yeye yule amtegemeaye kuwa kinga yake. Yesu aliseme"...mafarisayo na waandishi wamekalia kiti cha Musa, fuateni wanayosema, lakini msifuate wanayotenda" kama wote tutawaamini kuwa huwa hawatendi dhambi, tutapotea. Take note my fellows
 
Uli


Mkuu ulitaka atoe ngapi?, kama ni raha wote walipata raha, kwanza kwa nini mmoja tu ndiye apigwe faini kwani yule binti hana kosa?

Aisee. ...Hata kama alitishwa ili kupata hiyo raha?
Ninachoangalia ni thamani ya utu na sio pesa. ..
 
Huyu mchungaji kafanya makosa mengi tu.

1) Kazini
2) kavunja sheria ya uongozi
3) kazini na mtoto wa kaka yake
4) Kawataka kondoo wake waseme uongo
5) Kamdanganya mwanamke huyo kwamba akikataa kuzini nae atamwombea Dua kwa Mungu ili awe kichaa.
6) Kadanganya eti kazidiwa nguvu na shetani kuzini na mtoto wa kaka yake!!
Huyu siyo mchungaji jamani. Ni mhuni mzinzi tu wa kawaida kabisa. Wala hazini na huyo tu. Hana akili. Eti shetani kamzidi ujanja. Uzinzi wake utampeleka motoni kama asipouacha na kumwamini Yesu.
 
anasema hivi" alizidiwa ujanja na shetani" du ni shidaaaa!!...kila baya ni shetani....!!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom