bless on
JF-Expert Member
- May 22, 2026
- 901
- 2,180
Limpopo, Afrika Kusini — Mchungaji Christ Penelope, mwanzilishi wa Seven Fold Holy Spirit Ministries, amekuwa gumzo baada ya kuhusishwa na njia isiyo ya kawaida ya kuwaombea waumini wanaotafuta uponyaji.
Inadaiwa kuwa wakati wa ibada hiyo, mchungaji hukaa juu ya uso wa muumini na kumjambia, akidai kuwa kitendo hicho ni sehemu ya kuonyesha “nguvu za Mungu” na kwamba baadhi ya waumini huponywa baada ya kupata huduma hiyo.
Ripoti zinaeleza kuwa baadhi ya wafuasi wake husubiri kwa miezi kadhaa ili kupata nafasi ya huduma hiyo.
Kwa upande mwingine, jambo hilo limezua mjadala mkubwa mitandaoni, huku baadhi ya watu wakijiuliza kama kweli kujambiana kanisani kumefikia hatua ya kuwa huduma ya uponyaji.