Ye single baba wa mtoto wa kike na mi single mama wa mtoto wa kike tukubaliana tuyajenge tulee mabinti zetu.
Cha ajabu hataki nimwambie yeyote kuhusu huu uhusiano wetu.
Kanivisha pete mbele ya wanetu tu.
Katoa mahari.
Tunatarajia kufunga ndoa mwezi ujao.
Anataka ndo ihudhuriwe na wanetu na mashahidi 2 tu ambao atawasuggest yeye.
Hataki sherehe, get together wala shamra shamra yeyote.
Hataki marafiki wowote wajue anataka kunioa.
Anasema yeye ni introvert!
Naombeni ushauri ndugu zangu, wake kwa waume... kuna mahusiano ya hivi? I mean ya siri hata baada ya mahari kutolewa?
Is this a red flag au kuna wanaume wa hivi?
I am confused and frustrated.