Mchumba wangu anataka mahusiano ya siri

Mchumba wangu anataka mahusiano ya siri

Uttarra

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2019
Posts
468
Reaction score
783
Yeye single baba wa mtoto wa kike na mimi single mama wa mtoto wa kike, tukubaliana tuyajenge tulee mabinti zetu.

Cha ajabu hataki nimwambie yeyote kuhusu huu uhusiano wetu.

Kanivisha pete mbele ya wanetu tu. Katoa mahari. Tunatarajia kufunga ndoa mwezi ujao. Anataka ndoa ihudhuriwe na wanetu na mashahidi 2 tu ambao atawasuggest yeye. Hataki sherehe, get together wala shamra shamra yeyote.

Hataki marafiki wowote wajue anataka kunioa. Anasema yeye ni introvert!

Naombeni ushauri ndugu zangu, wake kwa waume. Kuna mahusiano ya hivi? I mean ya siri hata baada ya mahari kutolewa?

Is this a red flag au kuna wanaume wa hivi?

I am confused and frustrated.
 
Wanawake bhana, sijui huwa mnataka mbwembwe za sherehe za Nini!?

Mtu katoa Hadi mahari aafu unajiuliza maswali ya kijinga jinga hivi

Wenye akili angekuwa alishabeba hata mimba baada ya mahari kutolewa
 
Sijaelewa hapo kuna siri gani wakati anatambulika kwenu au ulikua unataka mapicha picha ya kupost mitandaoni

Wala mie sio wa kupost. Nahisi ana matatizo ya kisaikolojia. Shughuli ni watu.
 
Back
Top Bottom