Mchumba wangu ana mimba ya mwanaume mwingine

Mchumba wangu ana mimba ya mwanaume mwingine

Hiv wanaume tumerogwa wap,hiv ni maharage ya wap haya tumekula,daaah,hiv we una akil kwel?[emoji41]
 
Kwanza nianze kwa kukulaumu wewe mwenyewe, uliwezaje kumruhusu huyo mchumba wako akafanye kazi na kuishi kwenye nyumba yenye dume tu bila mke? Ni mazingira ambayo hakuna mwanamke atayeweza kuachwa salama. La pili jali moyo wako unasema nn, usisikilize watu papuchi nyingi watu wanagongeana tu ila uzuri haziongei tu, kama kweli ni mazingira hayo uliyosimulia bado anaweza kuja kuwa mke bora
 
Yaani Mleta uzi ni makosa yako. Huwezi ukasema ni mchumba wako, wewe una kazi nzuri then ukamruhusu aende kuuza duka.

Unajua tafsiri sahihi ya neno duka Kwa baadhi ya maeneo au jamii!?


Haaa haaa Haaa haaa teeeh teeeh teeeh . For sure, you can't be serious at the age of 25+!?

Hebu muoe tu maana maisha hayana mwenyewe.
 
Achana nae huyo anatafuta kurahisisha maisha wa hivyo wako wengi istoshe hata kwa jamaa kaaga kuwa ameenda nyumbani kwao kumbe yuko kwako!
Siyo rahisi abakwe siku moja na mimba siku hiyohiyo!!!!!
Tuwe makini wanaume hawa dadazetu sometime ni mastaa wazuri wa kutuchezeshea movie na akienda kwa mwingine tena nae atamwambia hiyo ni mimba yako pia....
STUKA
 
Mtoa Uzi una moyo,lakini linapokuja suala la kuoa unatakiwa utazame mbali zaidi,kuoa ni zaidi ya kuzaa na mimba,,,ila msimamo wa huyo binti unanipa mashaka ya baadaye,misimamo dizaini hii haijawahi kumuacha mtu salama.
Mpaka sasa hivi naona naona Giza tu sijapata ila ameenda kwao asipopiga simu inabidi nimpotezee
 
Utoto kazi kweli. Unafanya maisha mchezo mchezo sio!? Kua kimwili na kiakili. Uwezo wako wa kufikiri ni mdogo sana, usipokuwa makini utapigika sana na maisha kwa usawa huu
Uwezo wangu wa kufikiria ni mkubwa sana nikikukabidhi kichwa changu huwezi kulala njaa
 
Kama uko serious Bro basi utakuwa unampenda sana huyo mwanadada, ila naomba nikupee ushaur wang nnavyofikir maana naona umeamua kukubaliana nae hvyhvy;
1.Kama ana mahali pa kuishi usimpeleke kwako kwanza, we fanya tu kumpea mahitaji akiwa hapo hapo mpaka ajifungue akule uzazi pia n.k
2. Akuhakikishie kutokuwa na aina yoyote ya mawasiliano na huyo jamaa aliyempa mimba, maana umeamua kuvaa uhusika na umuhakikishie kumlea mtoto wake bila kikwazo mkija kuoana
3. Akishajifungua akipona vizur kama unaweza mtafutie mtaji kidogo wa biashara au kama utaweza kumpeleka koz yoyote ya bei ambayo haitakuelemea umpeleke ili apate namna na kujisimamia mwenyew
Nb: Fanya yote haya kama unamfanyia rafiki yako unaempenda sio mke wako na usimwamin kwa asilimia zote 100 maana na yeye ni mwanadamu. Otherwise Hongera kwa moyo ulionao
Aisee nipo siriazi na yeye ameomba nauli aende kwao na nimempakia kwenye basi jana. Ila atakaa mwezi mzima ndio arudi. Ila nitampima kwenye mawasiliano akinitafuta nitakumuoa ila akikaa kimya na mimi nampotezea moja kwa moja
 
Umeshaa penda wewe...na tayari una maamuzi yako kichwani...usitufanye MAFISIEM kutaka tuonekane TUNAKUCHONGANISHA na Demu wako...

Muoe tu na TUMBO LAKE...Hujui, pengine huyo MAKINIKIA atakusaidia UZEENI...
Kweli mkuu
 
Usibweteze akili unataka umuowe ili iweje mwache aende utakuja kumsumbuwa bule na kujilaumu mwenyewe pale penzi linapokuwa kero
Utajichosha bule huo mzigo ni wake na wa jamaa aliye mtiya mimba
La kufanya huyo binti aende dawati la jinsia akaangalie utalatibu wa kulea mimba na mtoto ajaye
Kweli aisee
 
Back
Top Bottom