Mchumba wangu ana mimba ya mwanaume mwingine

hussein boxer

JF-Expert Member
Dec 21, 2013
800
500
Habari za muda Huu wakuu.
Mwanzoni mwa mwaka Huu nilikuwa natokea moshi kwenda arusha nakumbuka nilikuwa nimepanda basi la lim safaris, akaja mdada mmoja akakaa karibu na siti niliyokaa mimi.

Wote tulikuwa kimya kwa mda mrefu ila nikaona nianzishe mazungumzo ya hapa na pale mwisho tukabadilishana namba za simu. Tulipofika arusha tukawa tunawasiliana kama kawaida.

Mimi nikarudi moshi kuendelea na kazi yangu ambayo mpaka leo naendelea kuifanya ila mwisho wa wiki nikawa narudi arusha ili nionane nae pia nifanye usafi chumba changu kwani sijahama arusha ila mwezi wa7 ndio nahamia moshi kwani nimepata kazi ya kudumu tofauti na ya mwanzo ambayo ilikuwa ya mda mfupi.

Baada ya kuwasiliana na huyu mchumba wangu kwa muda wa mwezi mmoja akaniambia kuna mama mmoja amekuja anatafuta msichana wa kumsaidia kazi ya duka huko DAR ikabidi nimruhusu akafanyekazi ila kwa muda wa miezi mitatu halafu nimtumie nauli arudi.

Baada ya kufanyakazi kwa muda wa wiki mbili huyo mama akamfukuza pia hakumpa nauli ya kurudi arusha. Pia kazi aliyeikuta ni ya ubeki tatu na sio ya kuuza duka. Kwa kuwa alikuwa na rafiki aliyesoma nae anayeishi huko DAR ikabidi akakae huko kwa muda ili nimtafutie nauli arudi arusha.

Baada ya wiki moja akaniambia amepata kazi sehemu nyingine ila kwa jamaa mmoja mwenye watoto wawili ila mke wake alishafariki. Ikabidi nimruhusu afanye ila akawa ananiambia huyo jamaa anatongoza kila mara ila yeye hamtaki. Nikamtumia nauli arudi ila akadai mshahara hajapewa nisubiri akipewa atakuja.

Baada ya mda mrefu kupita nikatuma nauli tena arudi ila akaniambia nisubiri baada ya siku4 atapewa hela yake. Alipopewa hela yake kesho yake akapanda basi nikamuambia ashuke stendi ya moshi akakataa ikabidi nimpe ufunguo nikapiga simu arusha kwa mpangaji mwenzangu akaelekezwa mpaka kwangu akafika na kuonyeshwa chumba changu akalala.

Kesho yake asubuhi sana nikaenda arusha kabla sijafanya nae mapenzi akaniambia ana mimba ya yule jamaa aliyekuwa akifanyakazi za ndani kwake, kwani huyo jamaa alitumia nguvu akafanya nae mapenzi bila ridhaa yake na kama sipo tayari kuishi nae nimuambie aende akaishi mbali pia abadili namba za simu ili asiwasiliane na mtu yoyote anayemjua.

Nikamuambia asijali nitamuoa hivyo hivyo alivyo. Ni binti ambaye ananijali na kunipenda kwa dhati hata kabla hana Huu ujauzito natamani kumuoa ila kwenye maisha yangu siku fikiria hata siku moja nitakuwa baba wa kambo. Nimeishi nae wiki mbili ila ameniomba akasalimie kwao kwani hajaenda miaka 6 nimempa nauli akae mwezi ili na Mimi nifanye utaratibu wa kuhamisha vitu vyangu ili nihamie moshi.

Naomba ushauri nifanyeje kwani nampenda na yeye ananipenda ila sijaridhika kulea mimba ambayo sio yangu nikifikiria kuitoa anaweza akafa pia ni dhambi kutoa mimba pia na yeye amekuwa muwazi na mkweli kwangu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom