TANZIA Mchora katuni gazeti la Mwananchi, King Kinya afariki dunia

TANZIA Mchora katuni gazeti la Mwananchi, King Kinya afariki dunia

Umetoka nje ya uhalisia na kuchagua kutoa mfano ambao utasupport ulicho kisema,hapa wala hatujaongelea issue ya Wilaya wala Kijiji,tumeongelea Hospitali nje ya Dar,ndio maana nimekwambia kua umetoa mifano ambayo utaona ina support ulichokisema,
Ninaweza kukupa mifano ya ndani ya Dar pia. Hospitali zina level, Hospitali ya Palestina haipo sawa na Mwananyamala na Mwananyamala haipo sawa na Mhimbili.
Kama kaamua kula miti shamba na kukataa matibabu ya hospitali,hiyo ndio justification ya kuona kua Hospitali nje ya Dar hazina matibabu bora? umechagua kutoa mfano wa Cancer coz unajua Hosp kuu ipo Dar,mgonjwa kukataa matibabu na kwenda kwa waganga wa kienyeji ndio ina maanisha kua,Hospitals bora zipo Dar peke yake? issue ya kwenda kwa mganga wa kienyeji inahusiana vipi na ubora wa matibabu ya Hospitali?
Mfano niliotoa ulilenga kuonyesha sababu ya mgonjwa kurudi nyumbani. Ambayo ni kufuata tiba mbadala haijahusiana na kulinganisha ubora wa mitishamba na ubora wa hospitali za Dar.
Lakini kwa swali lako jingine la ikiwa hospitali bora zipo Dar peke yake ninakujibu ndiyo, ukitaja KCMC ya Moshi kuna level ya KCMC zaidi ya 3 Dar, Ukitaja BMC ya Bugando kuna level ya BMC zaidi ya tano Dar, ukitaja Benjamin ya Dodoma kuna Benjamin zaidi ya Moja Dar.
Sasa hapa hili ni tatizo la mgonjwa kukataa matibabu au Hospitali kutokua na matibabu bora?
Naona umetoka kabisa kwenye mada,hii mifano yako wala haihusiani na nilichokisema kuhusu ubora wa matibabu ya Hospitali.
Kwenye mfano niliotoa wa Mgonjwa kukataa matibabu haina tofauti na ndugu kumtoa marehemu hospitali Dar na kumpeleka Morogoro.

Hapana, sijatoka kwenye mada, naona nimekuchanganya kwavile umesema ugonjwa niliotaja hospitali kuu ipo Dar.
Ndio maana nikakwambia kua,mgonjwa anaweza kufia popote pale,hata wanao enda India na Europe hufia huko pia,
Swala siyo kufa. Swala ni je alipofia alikua ana hata fursa ya kuweza kuishi tena?
Tanzania inapoazimia kwamba huu ugonjwa uende India au Europe ni kwakua inaona kwa wataalamu wetu na vifaa vyetu huu ugonjwa una % za kupona India au Europe.

Tanzania ikiona ugonjwa ufikishwe Europe, ndugu wakarudi nyumbani na mgonjwa ila siku akazidiwa wakampeleka hospitali hiyohiyo iliyosema mgonjwa aende India au Europe watakua wameamua kucheza na uhai wa ndugu.
Una data zozote za kusupport ulichokisema hapa?
Ndiyo.
Sasa kuhudumia wagonjwa wengi inahusiana nini na ubora wa matibabu? hujui kua Dar ina population kubwa? so,hata wagonjwa ni lazima watakua wengi?
Kwa mfumo wetu wa afya sehemu ya chini kabisa ya matibabu ni Zahanati, kisha Kituo cha Afya, kisha inakuja Hospitali ya Wilaya itakuja ya mkoa, Rufaa na kuendelea.

Magomeni siyo hospitali ni kituo cha Afya kinachotarajiwa kihudumie kata ya Magomeni, kwa mfano niliotoa hapo, hoja siyo population. Hapo hoja ni kwamba kituo cha afya cha kata ya Magomeni kinahandle watu wengi kuliko hospitali ya Wilaya.
 
Mfanyakazi wa Idara ya Habari ya Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), Kinyaguli Tuzo, maarufu King Kinya, amefariki dunia leo, Septemba 17, 2026 baada ya kuugua kwa kipindi kifupi.

Taarifa iliyotolewa Ofisi ya Rasilimali watu MCL imethibitisha kutokea kifo cha King Kinya aliyehudumu kwa miaka 17 kama mchora katuni wa magazeti yanayochapishwa na kampuni hiyo.

Akizungumza na Mwananchi kaka wa marehemu, Kiondo Mjema, amesema King Kinya alianza kuugua akiwa nyumbani Tabata mwanzoni mwa Julai,2026 hali iliyomfanya kukaa ndani kwa muda kabla ya kupelekwa Morogoro.

Amesema akiwa Morogoro hali yake ilizidi kuwa mbaya na baadaye alipelekwa hospitalini na kupewa rufaa ya kwenda hospitali ya Mloganzila alikolazwa kwa wiki moja kabla ya kuruhusiwa kurejea nyumbani. “Alipotoka hospitali aliambiwa arudi tena kwa ajili ya ufuatiliaji. Juzi alirudi hospitalini baada ya kusumbuliwa na tumbo, kuharisha na kutapika, akapewa dawa na kuruhusiwa kurudi nyumbani,” amesema.

Kwa mujibu wa Kiondo, hali ya marehemu ilizidi kuwa mbaya usiku wa kuamkia jana Septemba 16, 2026, akilalamikia maumivu makali ya tumbo na kichwa pamoja na kutapika na kuharisha, ambapo alifariki dunia.

Kiondo amesema msiba upo Kimara Kona na mazishi yanatarajiwa kufanyika kesho Ijumaa Septemba 18,2026 saa 10 jioni katika makaburi ya Mwananyamala.
 
Kwahiyo wanao ugua Dar wote hua wanapona kwa vile kuna huduma bora za kimatibabu?
Kwahiyo wanaougua nje ya Dar,wote hua wanakufa kwa vile hakuna huduma bora za kimatibabu?

Kuna watu husafirishwa mpaka India kwenye matibabu bora zaidi,ila hua wanafia huko,kuna wagonjwa hupelekwa kutibiwa Europe na US ila hufia huko huko.
Kuna wagonjwa wanaotoka India, Europe na USA kuja kutibiwa Dar
 
Kuna wagonjwa wanaotoka India, Europe na USA kuja kutibiwa Dar
Hapa umesupport hoja yangu pia,mgonjwa anaweza kufia popote pale haijalishi kuna matibabu ya aina gani au ubora gani sehemu aliyo enda kutibiwa,
Na anaweza kupona pia,haijalishi katibiwa wapi,issue ni ugonjwa gani unao msumbua.
 
Hapa umesupport hoja yangu pia,mgonjwa anaweza kufia popote pale haijalishi kuna matibabu ya aina gani au ubora gani sehemu aliyo enda kutibiwa,
Na anaweza kupona pia,haijalishi katibiwa wapi,issue ni ugonjwa gani unao msumbua.
Sijasupport hoja yako, hakuna mgonjwa wa kutoka Marekani aje kutafuta matibabu bora Dar.
 
Mtu anaumwa Dar.

Hali inakua mbaya.

Unampeleka Morogoro.

Dar kuna health facilities na kila huduma stahiki ambayo angeweza kuipata.

Ila akapelekwa Morogoro.

Kwa ninavyojua mimi kwenye hizi ishu hapa walijaribu tiba mbadala.

Zikadunda. Wakamrudisha hospital.

Sasa hospitali ya Morogoro na ya Dar hizi ni hospitali mbili tofauti.

Turudi kwa kampuni yake. L

Bima ya mfanyakazi wao wa miaka 17 ilikua inaweza kumpa huduma za ubora gani? Hospitali gani?
ajira? Huenda alikuwa mchoraji wa kujitegemea tu, media nyingi hasa magazeti haziajiri wachora katuni, ni day worker tu
 
We nani, mbona hatukujui kama ni mchora katuni tanzania. Kundi la kina king kinya wote wanajulikana, anzia bussines times, the guardian, habari corporation hadi mwananchi communication wachora katuni wote tunawajua
 
Wenzake hawa hapa waliochorea magazeti ya bussines times hadi huko mwananchi communication, masoud kipanya, nathan mpangala, noah yongolo, oscar makoye, masoud jr, chris shola, zahran, nick mtui, ibra washokera, james gayo, robert mwampembwa, dullah, fadhil moh'd na wengine wengi ambao hawakuwa maarufu sana. Huyu jamaa kwenye top 3 ya wachora katuni tanzania yupo, nazungumzia political cartoonist. Aliishaitwa bungeni na kamati ya maadili na hadhi ya bunge akajieleze kwa nini alichora katuni inayoonesha bunge ni kijibwa kisichokuwa na meno ya kung'ata. Sijui huo msala uliishaje.
 
Hii ni habari mbaya sana, huyu jamaa nilikuwa nakubali sana arts work zake.
 
Inasikitisha na kutafakarisha Hali ya uchumi wa huyu mwandishi,alianza kuumwa akiwa Dar kwenye huduma za afya Bora,akaamua kwenda Moro kwenye huduma mbaya za afya

Baadae akafa kwa kuharisha na kutapika

😭😭😭

Akili yako kama bado ya kitoto ,King Kinya alikua ni zaidi ya mtu hakua chawa kama wewe!
NB
WALI MTAMU MSIBA WA JIRANI!!
 
Back
Top Bottom