Nawaza kwa sauti,hivi na Mbasha nae angevumilia kipigo?au wangepigana.Adam kakosea sana ilibidi baada ya ule mtama angemshindilia na ngumi na konzi juu kwenye upara alafu angemtemea mate
Hit on the focal point....hiyo ndio picha kubwa zaidi ambayo wengi hawakuiona n kudhani anajadiliwa mchomvu ama anatetewa mbasha...wakati kumbe hao wametumika tu kama catalyst ya kukamilisha tafsiri deep zaidi kirohoMkuu umesema hili jambo lipo kiroho zaidi hata mimi nakubali, tukisema ni kiroho zaidi ni wazi hakuna yeyote angeweza badili matokeo yale sababu wote waliendeshwa kiroho, mara ngapi mtu anafanya kitu cha ajabu lakini anakuja kujishangaa mwenyewe ilikuwaje? pale kuna picha kadhaa zina tafsiri sahihi kabisa
- Mtumishi ameadhibiwa na Mungu hadharani kupitia Mchomvu kwa matendo yake ya nyuma ya pazia, watu wanamuona, kwa watu wa tungi wakirudia zile clip wataona kabisa kwa mtumishi yale ni maseke ya tungi kabisa.
- Mungu anasisitiza kufanya kazi,sasa mtumishi analeta utani kwenye kazi, Adam kamwakilisha Mungu kumuonya jamaa utani na kazi hauendi kabisa
- Hii ndiyo picha kubwa kabisa nayo ipo kiroho, kuna chama kinaumbuliwa hapa. Hakuna anayeweza control hili suala limetokea kiroho zaidi.
Naomba kuwakilisha.
Hekima ya mtu haionekani kwenye majisifu furaha na shangwe hapo kila mtu huonesha hekima sana...hekima halisi huonekana kwenye changamoto hasa mlengwa anapoguswa uhalisia hasi wa ndani yake.Mchomvu ni mfano sahihi wa ule msemo wa UKWELI UNAUMA
😁😁Inafurahisha kuona mpaka sasa tunakaribia robo ya karne hii ya 21 na bado kuna watu wanapigana mateke hadharani na kuahidi kutafutana mitaani ili wamalizane! Huu ubabe wa kizamani nilidhani uliishia karne ya 19 na 20.
HAHAHAHAHA WATU MNAMBINU!Tatizo mbasha nae sio mjasiriamali, ningekuwa mimi ule mtama nisingenyanyuka ningejigalagaza pale mpaka nilipwe hela ya kufungulia kampuni.
Fursa kabisa ile ila hajaiona.
Mnaosema Adam kakosea mnakumbuka Zidane alichokifanya kwa Materazzi kwenye fainali za kombe la dunia 2006. Chanzo chake hakina tofauti na chanzo cha mbasha. Kumvunjia mtu heshima mbele ya hadhara si jambo jema, ukuzingatia hadhara yenyewe hadi Rais wa nchi yupo anatizama.
Nina imani hata Mh. Magu kimoyo moyo amesupport uamuzi wa Adam. Majina ya watu maarufu ni Brand jitahidi kuyaheshimu haswa unapokua mbele ya Hadhira, ila kama mko chobingo huko vichochoroni utani ruksa.
Unalifahamu neno 'Mfano'?Watu wanaongelea habari za Adam na Mbasha, wewe unaleta story za Zizzou na Materrazi...asee kiungi gani cha mwili unatumia kufikiria.?