Adamu Mchomvu usiposhika adabu, yatakukuta kama yaliyomkuta Chidi Benzi "mikono mfululu"

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Oct 6, 2016
10,295
12,790
Hii tabia ya kupiga wasanii in public imeshakua ni tabia yako Sasa, ukidhani kuwa wewe ni nunda na ni mkakamavu sana.

Ulimpiga mtama mbasha kwenye jukwaa bila aibu na ukajizolea umaarufu ukajiona wewe ni ninja sana katika mapigano.

Muulize chidi benzi kilichompata, na yeye alikua na tabia Kama yako Tena alikua anajiita mikono mfululu akimaanisha kuwa yupo fiti katika mapigano.

Chidi alimpiga marehemu mangwea na alikuja akampiga profesa jay

Nafikiri adamu wewe ni msanii hizo stori unazo kuhusu utukutu wa chid benzi, kiufupi alikua anapenda kupiga watu ambao hata ugomvi hawapendi na siyo watu wa ugomvi kabisa.

Hutokuta sehemu marehemu ngwea kagombana na mtu au prof jay kagombana na mtu.

Lakini kilichokuja kumkuta chidi benzi ni aibu kubwa alipokuja kuchezea ngumi za kutosha na mwanahiphop mmoja anayefahamika kwa jina la kimbunga.

Kimbunga alimkanda chidi benzi ngumi za kutosha na huo ndiyo ukawa mwisho wake wakujifanya anapiga watu kumbe si lolote.

Kalapina nae kwenye show yake alimuadabisha chidi benzi mbele za watu baada ya kuleta ubabe mbele ya wanaume.

Nakusihi adamu mchomvu ipo siku utayakanyaga usije kusema hatujakubia na endelea kuwapiga hao hao wanyoge.
 
Adamu mchumba na anazidinkuisha sijui anawezaje kumpiga mtu mwenye nguvu zake. Bhange zinafanya unajiona mwamba ila kuna miamba ukipiga umeumia na haitopita muda utaskia kakandwa maana kila mtu atakua makini na yeye
 
Back
Top Bottom