Sizitaki mbichi hizi! Wivu tu, tambua hizi shule zinafundisha sio mchezo na kitu kingine ni kwamba watoto wanasoma kwenye shule hizi ni wale waliochunjwa sana, yaani ni wale VIPANGA kwa lugha ya wasomi kwa hapa bongo!Mkuu una point japo watanzania wengi huwa sio wadadisi na wanaojiuliza mambo. Ni uvivu kwa kwenda mbele anacholetewa ndio hicho hicho. Udadisi ulio uonyesha kwenda maswali yako ni mzuri. Mimi mfumo wa mtahani wetu unatoa nafasi kwa wanaokariri kushinda. Lakini ni muhimu sana ukajua kwamba hizo shule nyingi unazoona zinapazisha kwa kiwango cha juu (hasa binafsi) pamoja na kufundisha vizuri lakini huwa ni wajanja wa ''kuonyesha'' wanafunzi mitihani ili shule zao zikubalike. Hili nalo ni jipu linalohitaji umakini wa hali ya juu sana kulitumbua kwani linafanyika kwa uficho sana.
kiswahili cha kwenye mtihani si cha kuongea,ingekuwa hivyo wale waliozaliwa uswahilini ndo wangeongoza mtihani wa kiswahiliTuhuma za fedha kutumika kuhonga wasimamizi na walinzi wakati wa mitihani, hasa kwenye shule binafsi, awamu hii ya utumbuaji majipu izifanyie kazi.
Nimemsikiliza yule Mwanafunzi mchina , wakati anahojiwa, lakini kiswahili anacho ongea si kiswahili sahihi sana japo anajitahidi sana na ninapenda kumpongeza kwa kuiweka Tanzania ktk Ramani ya Dunia.
Mfano nimesikia akisema " watoto mengi", "nilitumia masaa nyingi" napata wasiwasi sana kwenye mfumo wetu wa Elimu na kujiuliza maswali yasiyo na majibu pengine.
1. Inawezekana mitihani ya sasa ivi ni kama ya kuchagua huhitaji kujua kila kitu. Au ni udhaifu wa mitihani yetu kwa kuwa haina mtihani wa kuongea japo sidhani kama ni muhimu sana kuwa na mtihani wa "oral"
2. Inawezekana wasahihishaji waliamua kupotezea baadhi ya makosa ambayo hayana athari kwenye tafsiri iliyokusudiwa na mwandishi.
3. Watoto wa sasa ivi wavivu kusoma hadi kupelekea asiye kiwezea vizuri kiswahili akifanya bidii anakuwa bora kuliko wale wanao kijua vizuri.
4. Je serikali imejiandaa vipi kupambana na matumizi ya fedha kwenye usahihishaji wa mitihani au wizi wa mitihani ( sina maana mchina kaiba)
5. Angeongeza bidii kidogo angepata A kali kabisa.
Je tinajifunza nini hapa?
Sina maana amependelewa. Naheshimu bidii yake na natambua kuwa ni mwanafunzi mwenye akili sana.
Kama wewe hapo unavyoweza kutamka "samahani" lakini hujui kabisa kuandika "samahani"Samahan wakuu...unawezaje ukaandika halafu ukashindwa kuongea??
Hilo swali waulize watu wote waliosoma combination za sayansi kama PCB,pcm hawa Kiukweli kwa kushuka tu ni hatare lakin mwambie aongee english ni mitihani,fanya utafiti utajua
mlimwuliza ni mzungu wa wapi? maana isijekua jamaa alikua mreno mkategemea angekua vizuri kwenye ngeli. ukweli ni kwamba si kila mzungu anajua vema kimombo.Wakati tunaingia chuoni..kuna mzungu alifeli screening test ya English wakati sisi wengine tulipeta..sasa sioni haja ya kushangaa...
Ndiyo hayo maneno yako kweli kbs !! Mie nilikuwa msemaji kweli shule mtaani mjini..ila ktk mitihani yote ya kiswahili sikuwahi kupata hata D!! ilikuwa zero tupu!!Unaweza kujua lugha ukashindwa kutamka maneno bali ukajua kuyaandika.
Na kwenye mitihani wanapata A ila kuongea wanaungaunga tuMbona Wabongo ni Wale wale tu Hajui kuongea Kiingereza ila kuandika Ni mzuri
Bahati nzuri ni kuwa nina uzoefu na hizo shule. Nilishawahi kuona cases nyingi za wanafunzi kupewa hints za mtihani. Japo nakubali kabisa bila shaka yoyote kuwa hizi shule zinafundisha vizuri sana na wanafunzi wake wana uwezo mzuri. Lakini kwenye mtihani huwa wanapewa hints nyingi sana. Jambo jingine ni kuwa japo wanaonyeshwa lakini ni kwa disaini fulani hivi kiasi kwamba kama mwanafunzi hana uwezo hataweza kupasi.Sizitaki mbichi hizi! Wivu tu, tambua hizi shule zinafundisha sio mchezo na kitu kingine ni kwamba watoto wanasoma kwenye shule hizi ni wale waliochunjwa sana, yaani ni wale VIPANGA kwa lugha ya wasomi kwa hapa bongo!
Well said, sawa anastahili hongera kwan amejitahidi sana kwa kweli lakini mbona hatuoni the same publicity to the first runner up. Mimi naona si sawa kwa kumfanya huyu mchina kuwa ndio central theme ya ufaulu wa mitihani ya kidato cha nne. Embu tumpe credit na mdogo wetu aliyeshika nafasi ya kwanza.tanzania kweli ni tanzania,........ hongera mchina.... embu tumpate na yule binti aliyekuwa wa kwanza kiingereza kapata ngapi?
Alitisha sanaView attachment 324142
Mara Nyingi Sana jina linaweza kuwa sababu ya wewe Kupenya ama Kukwama kwenye maisha. Baada ya matokeo ya Kidato cha Nne siku ya Jana Story kubwa ni Mchina aliye pata nafasi ya Pili kitaifa ambaye ni Mchina.
CongCong Wang ambaye amepata A tisa na B Moja Ya Kiswahili anasema Cong Maana yake ni Clever na Wang Maana yake ni King... So Jina lake lina maana Clever Clever King. Katika Mtihani wa Mock mkoa wa Dar alikuwa wa 2.
Alianza kusoma darasa la pili alipomaliza darasa la saba akaamua kuchagua NECTA badala ya Mfumo wa CAMBRIDGE sababu mfumo wa NECTA ni mgumu zaidi.
Kiswahili ni lugha yake ya 4 kujifunza anasikitika kupata B wakati MOCK alipata A.
Kati ya masomo aliyokuwa anafurahia zaidi ni somo la Historia ambalo mwalimu alikuwa anafundisha vizuri sana kama Movie.
Source: Clouds Media Group
Ni mchina bwana acha ubishiKuna mahali nilisoma kwamba huyo ni mtanzania, yaani ni raia wa Tanzania. Kama hivyo ndivyo kumuita mchina ni vibaya. Yeye ni mtoto kama watoto wengine. Hongera zake kwa kufanya vizuri