TATIZO NI THITHI!
Sawa kabisa nakubaliana na huyu, na hali kadhalika nakubaliana na wale wanaodai ni mfumo mpaya, mpaya kabisa.
Ukitaka CEO na Deans na HoDs kwenye vyuo vikuu, mfumo wa sasa(umeasisiwa na UDSM kusema kweli), ni kuwa wanateuliwa watu watatu, wanapewa jukumu la ku-search wanaofaa!Unajua nini hao watatu wanachaguliwa na mkuu aliye madarakani, yaani Mkandala akitaka Deputy VC wake yeye ndiye anayechagua search team, itamletea nani!!!? Haya madudu yanaacha mianya mingi ya hicho kitu kitamu cha kutamanika RUSHWA! Na thithi thote hatujali tunapoona sera mpya ambayo inaweza kufungua hio mianya, uliza kule UDSM kama wamewahi hata kukohoa kuhusu anayeteua search team. Hivi vijimambo vya kukaa kimya..THITHI...
Taasisi zetu zinaendeshwa kwa mikutano kibao tena inayochukua muda mrefu (ndio ni lazima na vibahasha viwepo), lakini amini usiamini, zaidi ya 80% ya wanaohudhuria hawafungui mdomo isipokuwa wanapokula kuku, sambusa, juisi, mapapai.
Ni kwa nini Bodi ya NHC haikuachagua mtu wao! Yaani taasisi nyeti kama NHC inaweza ikathubutu kuwa na BODI Mpya, MANAGEMENT Mpya kwa wakati...ni lazima kuna vitu vinajengwa...nitaanza kupayuka niachie hapa....