The Consult
JF-Expert Member
- Jan 20, 2017
- 220
- 252
"Executive Succession" ni kitendo cha ubadilishaji wa uongozi katika kampuni, hususani Mtendaji Mkuu (Top Manager) kwa ajili ya kuongeza ufanisi. Wastani wa muda ambao Mtendaji Mkuu wa kampuni (CEO) hutumikia ofisi hutegemeana na sheria za nchi husika. Moja ya tatu ya makampuni makubwa ulimwenguni (Major Corporations) hubadili watendaji wake wakuu mara moja kwa kipindi cha miaka mitano (5), na ni muhimu kwa kampuni za kati kuwa na utaratibu huu.
Kuna namna mbili za kumchagua mtu kwa ajili ya kushika nafasi ya Mtendaji Mkuu wa kampuni; Mosi, mtendaji wa ndani (internal candidate) hutambuliwa na kisha kuandaliwa kwa ajili ya kuja kushika nafasi ya u-CEO. Tafiti zinaonyesha kwamba kampuni zinazoongozwa na CEO aliyetoka ndani ya kampuni, hufanya vizuri zaidi sokoni ukilinganisha na kampuni ambazo CEO wake hutoka nje ya kampuni. Makampuni kama Cititcorp, General Electric, Hewlett-Packard, McDonald’s, McKinsey & Company, Microsoft, Nike, PepsiCo yanasifika kwa kuwatengeneza CEOs wao na ni dhahiri yanafanya vizuri sokoni. Kampuni ili ifanikiwe katika kumuandaa CEO kutoka ndani, mambo yafuatayo yanapaswa kufanyika;
- Bodi ya wakurugenzi (Board of Directors) kumshinikiza CEO kuandaa mpango wa urithishaji (Succession Plan)
- CEO kufanya utambuzi wa warithi wake kutoka ngazi za chini (hapa kwa kaisi kikubwa itategemea utendaji wa kazi wa mlengwa)
- Utoaji wa vivution vya kifedha kwa watendaji wazuri (financial incentives)
KUTAMBUA WATU MUAFAKA NA UWEZO WAO NDANI YA KAMPUNI
Kampuni inaweza kuwatambua watu muafaka na kuwaandaa kwa ajili ya kushika nafasi mbalimbali za juu kwa kutumia njia zifuatazo;
- Kuwa na mfumo wa tathmini ya utendaji (a sound performance appraisal system), kwa ajili ya kuwatambua watendaji wazuri wa kampuni na kuwa-motisha
- Kampuni kuanzisha " Leadership Development Center " kwa ajili ya kuwapika watendaji kwa ajili ya kushika nafasi mbalimbali katika kampuni.
- Kuwa na mfumo na utaratibu mzuri wa uajiri (a good human resource system) usio na upendeleo wa aina yoyote.
- Kutumia "Assessment Centres" kwa ajili ya kupima uwezo wa watendaji wanaotarajiwa kushika nafasi za juu katika kampuni. Utaratibu huu unatumiwa sana na makampuni kama; Standard Oil, IBM n.k
- Kuwa nautaratibu wa kuwahamisha watendaji kutoka idara moja kwenda nyingine (job rotation) hii inamsaidia mlengwa kupata zoefu mbalimbali za kimajukumu katika kumuandaa kushika nafasi ya juu ya kampuni.
The Consult; +255 719 518 367
E-mail; theconsult38@gmail.com
Dar es Salaam
Tanzania
Home of Project Management, Strategic Management & Fundraising Strategies