Mchepuko wa Kikorea umeng'ang'ana nirudi nao Tz

Kuna African movie moja intaitw Billo from Dakkar it's very interesting. Billo alisoma Madras Mali, baadae alifundishwa charahani, alitafutiwa mchumba. Kabla ya kuoa alikwenda Italy kwa boat, katika kuhustle na maisha akakutana na msichana mzuri sana wa kiitaliano, yule msichana alimsaidia Billo kupata tender ya kushona jeez za mpira. Ndugu zake yule msichana walikuwa against Billo lakini wote walipendana.

Siku Billo anakwenda Mali mwitaliano alitaka kwenda lakini Billo alikataa. Amefika Mali Billo alimuoa mchumba aliyekuwa anamsubiri mchumba akitegemea anakwenda Ulaya baada ya ndoa alikuwa disappointed Billo alimwambia utakuwa mke wa Afrika. Aliporudi Rome alimwambia siri binamu yake kuwa nimeoa home, binamu kiherehere mpaka familia ya msichana, akawaambia, msichana alikuja juu, Billo alimwmbia sikiliza mimi Mwislam ninaweza kuwa na wake wawili.

Italy alifunga ndoa ya bomani, basi aliishia kuwa na wake wawili na wote walielewa position zao. Unaweza kuipata hiyo movie you tube.
 
Wewe ni mkiristu na kwa hiyo nitakayosema hapa utayaelewa:
1.Maisha ya Kristu kama Mungu na binadamu yawe rejea katika suala hili.Kwamba kunapotokea tatizo shurti suluhisho hata kama ni la kufedhehesha kiasi gani lichukuliwe.Kukimbia matatizo sio njia aliyowahi Yesu kutuasa hata siku moja.Yeye aling'ang'ania msalaba hadi dakika ya mwisho
2. Time heals.Mkeo mtanzania na Mkorea ni watu wamekulia tamaduni tofauti kabisa.Unahitaji kumfundisha taratibu na kwa upole kwamba hilo lilotokea ni mambo ambayo Afrika yanatendeka.Njoo naye kuwa naye karibu.Usijaribu kumuumiza akiwa mjamzito.Ni kipindi anahitaji utulivu sio vurugu.Mkeo mtanzania ukifika mueleze.Hataelewa lakini wewe umeshakosa kama ambavyo yeye pengine amekosa kwa mambo mengine japo kuwa wewe hujui.
3.Tukio la wewe kuanguka dhambini usiliangalie kwa sura moja tu ya ubaya.Mungu ndiye anajua yote.Yapo mambo huja kwa sura ya ubaya lakini nyuma yake ni neema na yapo yajayo kwa sura nzuri lakini nyuma yake ni ubaya mkubwa.Usifikirie utafika Mbinguni kwa sababu umeweza ku-maintain ndoa ya mke mmoja mume mmoja na wala usifirie hutafika mbinguni kwa sababu ya kuongeza Mkorea
4.Huyo Mkorea kwa huo mtaji alionao nao unaweza kumuanzishia biashara nyumbani na ikawa msaada baadaye hata kwa mke mwenzie
Mafundisho ya dini hayana maana kama mwisho hayalengi kumsaidia mwanadamu.Mwanadamu hayupo kwa sheria na torati bali torati kwa ajili ya mwanadamu.Unakumbuka majibu ya Yesu juu ya wanafunzi wake kuparamia masuke ya ngano siku ya Sabato?
4.Hakikisha hatua yoyote utakayochukua hai-spoil passport yako.Dunia ya leo ni kijiji.
 
Mkuu nianze tu kwa kukupa pole..hilo jambo ni lakwaida kabisa hasa hasa kwa waafrika wengi waishio nchi za wazungu.. Waafrika waliowengi wanakosaga kabisa control wakikutana na wazungu kimapenzi..wanajiona wa maana sana..na mara nyingi hutegemea kufaidi kifedha kutoka kwa wazungu...Naongelea wote wanaume na wanawake.
Sasa kwa swala lako hili..kwanza ukubali umekosea sana na hakuna reverse yakurekebisha kosa hilo...mimi nakushauri kwanza maliza mtihani wako, kisha baada ya mthihani mwite huyo mkorea wako pahali then mwambie ukweli wote kua una familia achague chakufanya...ataumia sana ila atakubali tu coz ndo ukweli huo...
Ukubaliane na kitakachotokea. Huyo mkorea akijua ukweli..badae atafanya abortion akusahau kabisa.

Ila mkuu iwe fundisho kwako...usijesema uongo tena.
Wacha dhambi na usijikoshe eti unampenda mkeo wakati umemsaliti.
 
ushauri mzuri sana huuu
 
Point namba nne nimeielewa hasa
 
Uongo Ni mbaya, and it will cost u, mwambie ukweli akikufuata awe ameufaham


 
Kwanza pole na ukome vilevile.Truth heals,na usitegemee kufunika kosa kwa kosa tena.
Mwisho story yako very interesting bongo muvi wachukue hii script ya bure
Nami naiona kama story maana amesema mkorea yupo smart na ameishampekua jamaa anajua mambo mengi kumhusu eti ashindwe kujua kama ameoa na familia? Ngumu kumeza, kwa vile tumeambiwa ana wivu anapekua kila kitu itawezekana vipi awe hajaona hata picha za familia, calls za wife, hata documents za usajili wa vyuo vingi nje huwa unajaza marital status!!! Kama amemudu kumficha haya yote kwa muda wote basi anaweza kuficha zawadi atakazonunulia familia na Kumficha mkorea buguruni kwenye chumba atakachompangia wakifika bongo.
 
Hapo umenena mkuu
 
Aiseee kumbe anaweza mficha mkorea buguruni??
 
Dili nipe namba ya mkeo unifumanie naye and then mtimue Maisha yataenda... Watoto utamuambia umesingiziwa ni wangu ila unawapenda moyoni... na unataka kuishi nao kama baba yao wa kufukia... ila ndio mkeo nitampangia sehemu niwe namla kimapozi tu hutoumia am sure.. Bonge la Ushauri... Habari ya Kifacebook inajibiwa kifacebook pia Alamsiki.
 
naona harufu ya huyo mtoto kuja kuwa Obama wa korea kusini wa miaka ijayo
 
Nimefananisha story yako na movie za ki_Korea yaani chief umelenga kweli doo!!
 
Usimuache huyo binti. Kwanza subiri mtihani uishe mpange safari.

Mwambie huyo mkeo wa bongo ulimzalisha long time so huna jinsi.

Kiukweli hapo ukizingua tu umemuua huyo binti.
 
Hahahaha hii kitu inanikumbusha mshua alimtania mama siku moja nitakuletea Mke wa Kikorea hapa ndani ,tuone utafanyaje ,kiswahili hajui wala kingereza ukimzingua ni huuu haaa za kutosha

Dah sina hata cha kukushauri ila nikutakie kila la kheri kwenye maamuzi yoyote utakayo chukua hata kama ni kujitundika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…