Mchepuko wa Kikorea umeng'ang'ana nirudi nao Tz

Mchepuko wa Kikorea umeng'ang'ana nirudi nao Tz

Kwann ulidanganya?
Kweli itakuweka huru
Vip korea kuko vizuri,nami mwakani nataka nende kwa masters yangu
 
Kumbe maandiko yako sahihi kabisa kuwa apandacho mtu, ndicho atakachovuna.

Nashindwa hata kukuonea huruma kabisa, lkn maumivu na huruma zangu na masikiko yangu ni kwa huyo dada wa Kikorea, jinsi ulivyomtendea, tena kwa makusudi bila huruma. Kama ulishindwa kumuonea huruma huyo dada na kumdanganya, iweje ujionee wewe huruma?

Kwa ukatili uliomtenda huyo dada, uovu wako na uwe juu yako mwenyewe.

Vv
 
Wadau,

Nahitaji mchango wa mawazo yenu kama kichwa cha habari kinavyojieleza. Kisa chenyewe ni hivi mimi ni diaspora ambaye nipo Korea kimasomo tangu November 2014. Mwezi Juni 2016 nahitimu masomo. Nimeoa na tumebarikiwa kuwa na watoto wawili.

Nikiwa huku Korea ya Kusini nilianza mahusiano na mdada wa kikorea, ni mrembo ila si wa kutisha sana si unajua watu wa ukanda huu kinachowapendezesha ni rangi tu waliyonayo vinginevyo kama wangelipakwa rangi nyeusi hakuna atakaye watamani.

Mdada huyu anajiheshimu sana tulianza kuzoeana kama classmate tu. Alikuwa karibu sana na mimi mpaka tukaanza kuvuka mipaka na kuwa wapenzi. Kosa nililofanya ni kwamba sikuwahi kumweleza ukweli kuhusu hali yangu ya ndoa, yaani nilimdanganya kwamba mimi sijaoa.

Tulianza mahusiano kwa siri kwasababu ya kuhofia jamaa zake wasijue kuwa anamahusiano na ngozi nyeusi. Ilifika wakati usiri ukawa unashindikana maana tulikuwa tunaenda club pamoja na kurudi na kulala aidha sehemu ninayoishi au anayoishi yeye. Kuna wakati mama yake aliwahi kuja juu sana akasema kwamba niachane na bintiye vinginevyo ataliwasilisha swala hilo polisi na ninaweza kufutiwa visa ya kuishi Korea.

Tulishauriana na binti kuwa tuachane ili nisije nikaharibu future yule binti akadai yeye akadai hawezi kuachana na mimi kwasababu hajawahi mjua mwanamume mwingine zaidi yangu tangu azaliwe. Na swala la yeye na mama yake anasema hawezi fanya chochote kwasababu yeye ni mtu mzima anapaswa kufanya maamuzi yake bila kuingiliwa na mtu. Nilimsihi tuendelee kwa siri ili nisije nikaharibikiwa kimasomo.

Mwezi uliopita mdada kanimaliza kabisa kaniambia anaujazito wangu, nimechoka mpaka sasa anasisitiza kuwa tunarudi wote Tanzania. Mwanzo nilijua ni utani lakini mpaka nimejua kuwa hatanii. Kwasababu ya urahisi jana Jumatatu nilimtuma yeye aende kunikatia ticket ya ndege amerudi na ticketi mbili yangu na ya kwake tunayosafiri pamoja.

Nimeshikwa na mfadhaiko, nimejaribu kumwambia tu kwa busara kwamba yeye angebaki kwanza ili nikafanye maandalizi ya kumpokea maana mimi nilipotoka nilikabidhi nyumba niliyokuwa naishi hivyo kwenda mahali na mgeni sina mahali pa kufikia itakuwa si vizuri.

Yeye amesisitiza kuna shida gani nikatapo lala naye atalala hata kama kibarazani. Pia akasema hawezi kuendelea kuwepo Korea maana ndugu zake wanaweza hata kumwambia atoe ujauzito wangu na pia wanaweza kumtenga ni heri akaondoka akaenda kuishi na mtu anayempenda hata kama ni sehemu ya tabu.

Kuhusu pesa yeye anasema sio shida anakiasi cha fedha ambazo ukizibadili zinaweza kufikia hadi 150 m ambazo zilikuwa ni mirathi ya marehemu baba yake. Kiukweli mdada huyu amenisaidia sana kifedha. Sikuwahi kuwa na shida ya kifedha muda wote nikiwa Korea.

Hofu yangu ni nyumbani ambako mke na watoto wangu wananingojea kwa hamu, nimeshindwa hata kuwanunulia zawadi maana huyu mdada anajua kila kitu ninachofanya. Ndani kwangu ni kama kwake. Jana nilipanga nimwambie ukweli lakini nilipokuwa namtazama nikajua anaweza nivuruga mpaka nikashindhwa kufanya mitihani yangu ya mwisho. Pia nilimwonea huruma sana kwamba naye anaweza asifanye vizuri hiyo mitihani yake. Ananipenda sana mpaka namuonea huruma sijui nikimwangalia.

Nilikuwa nafikiri nimwache wakati narudi nikifika Doha wakati wa kubadili ndege nimchenge potelea mbali hata kama nitakula hasara ya ticket. Lakini nimejikuta naona hiyo itakuwa ni kazi bure maana mdada huyu anajua mpaka ninapofanya kazi anwani yangu ya Tz anazo hata akaunti namba ya benki yangu anayo mana kuna wakati nikiwa likizo Tz alishawahi kunitumia pesa kwenye akaunti zangu.

Mke wangu na wanangu wananisubiria kwa hamu sana, na wanadai niwapelekee zawadi japo natoa kisingizio kwamba nimebakiwa na fedha ya nauli tu. Cha ajabu wife akasema basi atanitumia kwa Western Union mana kuna vitu nilishawahi kuwapelekea ni vizuri sana na vilikuwa vinauzwa bei ya chini sana. Huku mrembo wa kikorea naye anahesabu siku zilizobakia ili aweze kuruka nami kuja Tz.

Msaada wa kutatua tatizo hilo wadau. Niko njia panda nampenda mke wangu nawapenda wanangu. Namhurumia Mkorea alivyojitoa kwangu.

Nawasilisha kwa ajili ya ushauri.
Mkuu pole kwa maswaibu. Ila ulivyokuwa korea ULIVUA PETE YA NDOA?
 
Aise pole sana, hapo naona fanya umlete Tz alafu danganya familia utachelewa kidogo, mpangishie mahali alafu nenda kwa mke na watoto. Alafu ufanye uwe unatembelea potepote, maana kwamba huyo ashakuwa nyumba ndogo regardless dini yako bro. Akijifungua mwambie ukweli wote na kwamba yeye atakuwa nyumba ndogo na akusamehe kwa uongo, maisha yasonge.

Ila umebugi kinyama we jamaa, na nyie ndio mnafanya hadi race yetu as black melanin peeps tuonekane hovyo.
Daaah...pote patam,Mkorea naye kakorea kinyama,kuna hatari Mkorea akawa Mwehu au kujiua akikukosa mkuu,na amekutoa mbali mbali na alionesha lake penzi la dhati kwako kitambo kiasi cha kukosana na Wazaz na ndugu kwa ajili yako,tafadhali mkuu usimuache,ukimuacha atakuwa mgeni wa nani?,mchukue na uje naye Tz,tafuta chumba mpangishie na uwaeleze Wazazi wako ukweli wa mambo,baada ya hapo utakuwa unamtembelea huku ukitafuta mbinu na huku ukimsoma mkeo kabla ya kumpa ukweli,na huku ukizidisha mapenzi kwa mkeo Mbongo,kama kumjali na kumnunulia zawad mbali mbali na mambo ya 6*6 ilimradi tu kumjengea mazingira ya kumwambia ukweli,Ukifanikiwa kumweka mke wa Ktz sawa,basi kwisha mchezo,utaweza kumtambulisha hata mkeo kwa Mkorea kuwa ni binamu,sister,mdogo wako au vyovyote vile utakavyo na kama Mwanamke ni muelewa atauvaa uuhusika,na sababu Mkorea hajui Kiswahili wambea itakuwa ngumu kumwambia ukwel,na maisha yatakuw poa
 
Aise pole sana, hapo naona fanya umlete Tz alafu danganya familia utachelewa kidogo, mpangishie mahali alafu nenda kwa mke na watoto. Alafu ufanye uwe unatembelea potepote, maana kwamba huyo ashakuwa nyumba ndogo regardless dini yako bro. Akijifungua mwambie ukweli wote na kwamba yeye atakuwa nyumba ndogo na akusamehe kwa uongo, maisha yasonge.

Ila umebugi kinyama we jamaa, na nyie ndio mnafanya hadi race yetu as black melanin peeps tuonekane hovyo.
Mkuu, dawa ya dhambi ni kukiri na kutubu, vinginevyo dhambi huzaa dhambi na mwisho ni maisha ya kitumwa. Ni afadhali kusema ukweli ili awe huru.

Vv
 
Kwann ulidanganya?
Kweli itakuweka huru
Vip korea kuko vizuri,nami mwakani nataka nende kwa masters yangu
Korea Kusini kuko vizuri sana tofauti na nchi zingine za ukanda huu. Karibu ila mimi ndio narudi Jun mwaka huu.
 
Fanya hv, we njoo nae kisha weka mazingira ya kukaa nae ht kwa mwezi mmoja bila kumwambia ukweli, wakati huo uwe umeshanionesha huyo mkorea, mimi ntaweka nae ukaribu wa hatari lkn tukiwa hutujuani kabisa, mm ntajua ntakachofanya ndani ya mwezi huo mmoja, halaf sasa mwambie ukweli, ila ujue ntamchukua mm tutakulelea mtoto wako lkn usitusumbue baadae
 
Korea Kusini kuko vizuri sana tofauti na nchi zingine za ukanda huu. Karibu ila mimi ndio narudi Jun mwaka huu.

Asante ngoja nimalize kumshughulikia mshenz mmoja then,i will take a break with my baby boy
Nilitaka nende dubai sema nimeona sitasoma vizuri,
Next year panapo majaliwa naenda na mwanangu kuchukua masters yangu,
Nimejipanga na namwomba Mungu anisimamie nipate break,just me and my little man.
 
Baki huko tu. Kazi watakupa. Ukija huku labda utibu kwa mitishamba na zile sindano zao au ukalimani.
Naamini ulisharopoka sana kwa hiyo hata kijijini kwenu ulishamwambia.
Kumkimbia unajisumbua.
Rudi badili dini au oa kimila.
Mbona unamwogopa mkeo hivyo? Au unaishi ukweni kama wahindi?
 
Asante ngoja nimalize kumshughulikia mshenz mmoja then,i will take a break with my baby boy
Nilitaka nende dubai sema nimeona sitasoma vizuri,
Next year panapo majaliwa naenda na mwanangu kuchukua masters yangu,
Nimejipanga na namwomba Mungu anisimamie nipate break,just me and my little man.
Ukihitaji taarifa zaidi waweza nicheki hata kunipm
 
Mkuu wazo ni zuri sana ila nafikiri nikikosa wazo mbadala lililozuri nitalifanya aidha airport ya huku Seoul tukiwa tumeshacheck in au Doha ili akachachamaa nampotezea.

Kwa nini unataka kumtoroka! Hapa unakili kwamba alikuwa anakusaidia sana kumaisha/kifedha halafu ana mimba yako - kama ulikuwa umpendi mbona ukutumia kinga ya kuzuia mimba?

Ndiyo hivyo tena umelikoroga mwenyewe, kama utamwambia ukweli kwamba una mke na watoto akag'ag'ania kuja Tanzania njoo naye - ukimwacha Korea yeye na mtoto wako watapata wakati mgumu kutoka kwa jamii - kwa nini utake kumtesa mtoto wako wa halali na mama yake.

Mimi nina hakika akija Tanzania na kuona hali alisi atajipima mwenyewe kama aendelea kuishi hapa au arudi Korea na kukuachia mtoto, mtoto atakuwa na amani akikulia Tanzania kuliko Korea, hapa hakuna ubaguzi wa rangi - yaani kuona machotara kama kituko.

Chunga sana wenzetu hawa hawana simile ukifanya mchezo anaweza kukuua, nimewahi kupoteza baadhi ya marafiki zangu kutokana na mambo haya ya kutaka ku double cross wanawake wa kizungu na vile vile na wanawake wa Far East wote hulka zao zinafanana - chunga sana.
 
Yaani kuna uzi unasoma halafu unaishia kucheka basi na huu nimecheka hivyo.

Ndio maisha uliyochagua, bora ungekuwa mkweli tangu mwanzo, ila shida ya pesa ndio ukaendelea kuwa nae na uongo umeubeba.

Haya hongera na wake wawili....mresho upo?sababu June imeshasepa
 
Yaani kuna uzi unasoma halafu unaishia kucheka basi na huu nimecheka hivyo.

Ndio maisha uliyochagua, bora ungekuwa mkweli tangu mwanzo, ila shida ya pesa ndio ukaendelea kuwa nae na uongo umeubeba.

Haya hongera na wake wawili....mresho upo?sababu June imeshasepa
Mkuu Avatar Yako Ni Princess Diana Of Wales ?
Umecheka Sana
Matatizo Yapo

Huyu Mleta Mada Atakuwa Karudi Bongo Na Mkorea Wake
 
Mkuu Avatar Yako Ni Princess Diana Of Wales ?
Umecheka Sana
Matatizo Yapo

Huyu Mleta Mada Atakuwa Karudi Bongo Na Mkorea Wake

Ndio yeye.

Ameleta mrejesho mrefu wa uamuzi wake wa nini aliamua kufanya kiufupi aliamua kwenda nae....kaisome, ila hadi jana bado wa alipofika Tanzania imekuwaje hajaleta habari.
 
huu mchezo hauhitaji hasira, unamweleza mke wako kuwa samahani kuna mdada wa kikorea nitakuja naye aliwahi kuwa mpenzi wangu anataka tushirikiane tuanzishe biashara, nakuomba huwe mpole kwani wakorea wanapenda sana kwao awazi kukaa africa hatarudi tu, unaangalia anasemaje, akija juu unasema ninakutania, akisema poa mjoo naye huyo mkorea, akishafika dar umweleze ukweli.
 
Back
Top Bottom