Mchepuko wa Kikorea umeng'ang'ana nirudi nao Tz

Mchepuko wa Kikorea umeng'ang'ana nirudi nao Tz

Ndio yeye.

Ameleta mrejesho mrefu wa uamuzi wake wa nini aliamua kufanya kiufupi aliamua kwenda nae....kaisome, ila hadi jana bado wa alipofika Tanzania imekuwaje hajaleta habari.
Mkuu Huyu Jamaa Aliondoka Tanzania
Jk Akiwa Rais,Anarudi Anakuta Jpm Ndiyo Rais
Halafu Nchi Iko Tight
Tunasoma Namba Kwa Kabila Zote
 
Mkuu Huyu Jamaa Aliondoka Tanzania
Jk Akiwa Rais,Anarudi Anakuta Jpm Ndiyo Rais
Halafu Nchi Iko Tight
Tunasoma Namba Kwa Kabila Zote

Kamsome huko kama bado...eeeeh, ni kweli re awamu na maisha. Kamsome maana eeeeh...alikuwa na mipango haswa..anampangishia nyumba mbali na anapoishi. Na kumwambia anamsaidia kumfungulia business kwa pesa yake dada mkorea nae awe na kipato kinaingia...sijui amefikia wapi bali alijipanga.
 
Hapo hakuna siri tena, kwanza kubali lazima jamii itakutiza kwa mtazamo tofauti na mwanzo. Cha msingi inatakiwa ukubali kuishi maisha yatakayofuata baada ya siri hiyo kufichuka pande zote mbili. Nakushauri usijaribu kumuumiza mkorea, mlete bongo tumia mbinu hizo qmbazo umeshauriwa za kumuhifadhi sehemu tofauti na nyumbani
Akishafika mueleze ukweli pia muombe msamaha kwa yote yaliyotokea b4 na mueleze nia yako ya dhati ya kumlinda kwa lolote lile akiwa hapa tz. Nenda pia kwa mke wako mueleze makosa uliyoyafanya na muombe msamaha kwa hayo Ila zaidi hata kama ataonyesha kukuchukia wakati huo ndio wakati ambao unatakiwa kuzidiaha upendo kwake. Yakubali maisha yako ya baada ya kuwaambia. Ishi Mao wote vizuri
 
Mwambie umeongea na wazee nyumbani wamekua nyoka. Yaan hawataki kusikia na akifika watamchinja au kumloga. Yaan hawataki kabisa ngozi nyeupe kwenye ukoo na tayari washakuolea mke yupo anakusubiri na siku ya kufika Bongo unapokelewa na mkeo Airport moja kwa moja kijijini kwenye sherehe ya ndoa ya kimila. Hapo vipi?
 
Mimi nachangia kwasababu umeomba ushauri au ulitaka nikwambie kile kinachokufurahisha?!

Mnafki sana na nawish mkeo ajue aina ya nyoka anayeishi naye ndani ya nyumba..

Kama ulitaka ushauri ndio huo nimekupa cheza na mtoto wa watu unyongwe ....

Umechagua kuishi kisanii endelea kuishi kisanii usikimbie kivuli chako..
Mkuu kama wewe mwanaume hupaswi kumuhukumu mtu kiasi hiki maana wahenga wanasema ,"Hujafa hujaumbika".
 
Hakuna kitu kizuri kama ukweli mweleze tu ukweli then ajuwe anafanyaje baada ya yeye kujua ukweli ndo mtaweka muafaka kati yako na yeye pamoja na familia yako
 
Hapo ili usilete madhara zaidi ni bora ukamwambia mkorea after kumaliza kila kitu about shule,mwambie kuwa huwezi kuondoka nae kama familia yake haijaafiki jifanye unajali maelewano ya yeye na familia yake pia (usitaje kuwa una familia) then ili asitengwe na familia yake kubali atoe mimba kama dhambi ushatenda ya kuzini,Usije ukawaza kiafrica hata siku moja kuwa mkorea atakubali kushare yaani awe mke wa pili hata kama mkeo atakubali, ni ngumu watu weupe kuishi kweny uongo uliomfanyia....NB ushauri wangu una base na kauli yako kuwa unaipenda familia yako.
Chukua maamuzi hata kama ni mabaya ya ili kulinda yasiwe mabaya zaidi.....
Ndio maisha yalivyo.
 
Wadau,

Nahitaji mchango wa mawazo yenu kama kichwa cha habari kinavyojieleza. Kisa chenyewe ni hivi mimi ni diaspora ambaye nipo Korea kimasomo tangu November 2014. Mwezi Juni 2016 nahitimu masomo. Nimeoa na tumebarikiwa kuwa na watoto wawili.

Nikiwa huku Korea ya Kusini nilianza mahusiano na mdada wa kikorea, ni mrembo ila si wa kutisha sana si unajua watu wa ukanda huu kinachowapendezesha ni rangi tu waliyonayo vinginevyo kama wangelipakwa rangi nyeusi hakuna atakaye watamani.

Mdada huyu anajiheshimu sana tulianza kuzoeana kama classmate tu. Alikuwa karibu sana na mimi mpaka tukaanza kuvuka mipaka na kuwa wapenzi. Kosa nililofanya ni kwamba sikuwahi kumweleza ukweli kuhusu hali yangu ya ndoa, yaani nilimdanganya kwamba mimi sijaoa.

Tulianza mahusiano kwa siri kwasababu ya kuhofia jamaa zake wasijue kuwa anamahusiano na ngozi nyeusi. Ilifika wakati usiri ukawa unashindikana maana tulikuwa tunaenda club pamoja na kurudi na kulala aidha sehemu ninayoishi au anayoishi yeye. Kuna wakati mama yake aliwahi kuja juu sana akasema kwamba niachane na bintiye vinginevyo ataliwasilisha swala hilo polisi na ninaweza kufutiwa visa ya kuishi Korea.

Tulishauriana na binti kuwa tuachane ili nisije nikaharibu future yule binti akadai yeye akadai hawezi kuachana na mimi kwasababu hajawahi mjua mwanamume mwingine zaidi yangu tangu azaliwe. Na swala la yeye na mama yake anasema hawezi fanya chochote kwasababu yeye ni mtu mzima anapaswa kufanya maamuzi yake bila kuingiliwa na mtu. Nilimsihi tuendelee kwa siri ili nisije nikaharibikiwa kimasomo.

Mwezi uliopita mdada kanimaliza kabisa kaniambia anaujazito wangu, nimechoka mpaka sasa anasisitiza kuwa tunarudi wote Tanzania. Mwanzo nilijua ni utani lakini mpaka nimejua kuwa hatanii. Kwasababu ya urahisi jana Jumatatu nilimtuma yeye aende kunikatia ticket ya ndege amerudi na ticketi mbili yangu na ya kwake tunayosafiri pamoja.

Nimeshikwa na mfadhaiko, nimejaribu kumwambia tu kwa busara kwamba yeye angebaki kwanza ili nikafanye maandalizi ya kumpokea maana mimi nilipotoka nilikabidhi nyumba niliyokuwa naishi hivyo kwenda mahali na mgeni sina mahali pa kufikia itakuwa si vizuri.

Yeye amesisitiza kuna shida gani nikatapo lala naye atalala hata kama kibarazani. Pia akasema hawezi kuendelea kuwepo Korea maana ndugu zake wanaweza hata kumwambia atoe ujauzito wangu na pia wanaweza kumtenga ni heri akaondoka akaenda kuishi na mtu anayempenda hata kama ni sehemu ya tabu.

Kuhusu pesa yeye anasema sio shida anakiasi cha fedha ambazo ukizibadili zinaweza kufikia hadi 150 m ambazo zilikuwa ni mirathi ya marehemu baba yake. Kiukweli mdada huyu amenisaidia sana kifedha. Sikuwahi kuwa na shida ya kifedha muda wote nikiwa Korea.

Hofu yangu ni nyumbani ambako mke na watoto wangu wananingojea kwa hamu, nimeshindwa hata kuwanunulia zawadi maana huyu mdada anajua kila kitu ninachofanya. Ndani kwangu ni kama kwake. Jana nilipanga nimwambie ukweli lakini nilipokuwa namtazama nikajua anaweza nivuruga mpaka nikashindhwa kufanya mitihani yangu ya mwisho. Pia nilimwonea huruma sana kwamba naye anaweza asifanye vizuri hiyo mitihani yake. Ananipenda sana mpaka namuonea huruma sijui nikimwangalia.

Nilikuwa nafikiri nimwache wakati narudi nikifika Doha wakati wa kubadili ndege nimchenge potelea mbali hata kama nitakula hasara ya ticket. Lakini nimejikuta naona hiyo itakuwa ni kazi bure maana mdada huyu anajua mpaka ninapofanya kazi anwani yangu ya Tz anazo hata akaunti namba ya benki yangu anayo mana kuna wakati nikiwa likizo Tz alishawahi kunitumia pesa kwenye akaunti zangu.

Mke wangu na wanangu wananisubiria kwa hamu sana, na wanadai niwapelekee zawadi japo natoa kisingizio kwamba nimebakiwa na fedha ya nauli tu. Cha ajabu wife akasema basi atanitumia kwa Western Union mana kuna vitu nilishawahi kuwapelekea ni vizuri sana na vilikuwa vinauzwa bei ya chini sana. Huku mrembo wa kikorea naye anahesabu siku zilizobakia ili aweze kuruka nami kuja Tz.

Msaada wa kutatua tatizo hilo wadau. Niko njia panda nampenda mke wangu nawapenda wanangu. Namhurumia Mkorea alivyojitoa kwangu.

Nawasilisha kwa ajili ya ushauri.

Mkwe ulitisha🙌🙌🙌🙌
 
Nilikabwa kitanzi mkwe ila baadaye mambo yalikwenda sawa. Nilimkwaza sana D.

Anayekupenda na ukamhakikishia unampenda hakuachi

Utamkwaza, mtavurugana, mtaombana msamaha na atakusamehe kabisaaaaa

Mimi na baba yenu tunaelewa 😀😀😀
 
Anayekupenda na ukamhakikishia unampenda hakuachi

Utamkwaza, mtavurugana, mtaombana msamaha na atakusamehe kabisaaaaa

Mimi na baba yenu tunaelewa
Kabisa imetokea kama mara tatu ambazo alijua nimecheat. Hii ya mkorea ilikuwa ni moto. Nilijua ni ndiyo mwisho, lkn tukaweka na tunaendelea.
 
Tupe mrejesho mkuu...

Huko juu tulitumia juhudi sana kukupa ushauri ujue...
Mrejesho huu hapa mkuu
 
Alafu ukidundwa na ndugu zake ulete malalamiko hapa oh watu weupe ni wabaguzi wanachukia black people.


Ni akili za kipumbafu haswaa, umeenda masomoni na huku nyuma umeacha mke wako! Mwafrika bwana!!!!


Africans ni Africans, hii asili haitabadilika. few recognize themselves
 
Kabisa imetokea kama mara tatu ambazo alijua nimecheat. Hii ya mkorea ilikuwa ni moto. Nilijua ni ndiyo mwisho, lkn tukaweka na tunaendelea.

Ukiona tunalia na kuongea sana kuachana kukupo mbali sanaaaaaaa. Ila ukiona tunakuangalia na kukuacha ulivyo ujue tuu umefutwa hadi kwenye ricyclebin

Hata ikitokea akasema amekusamehe ni sababu ya mazingira kama watoto na wazazi na sio upendo. Na utaishi kwa taabu hadi upate magonjwa yasiyoambukiza.

Mungu awasaidie msifike huko🙏
 
Back
Top Bottom