PreGE2025 Mchengerwa: Serikali yasaini mikataba, Watoa huduma watatu kuendesha Mwendokasi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,500
Wizara ya TAMISEMI imesema kupitia ubia kati ya Serikali na Sekta binafsi (PPP) imefanikisha hatua ya kihistoria ya kusaini mikataba na watoa huduma watatu wa uendeshaji wa awamu ya pili ya mabasi yaendayo haraka ambapo imesema mabasi hayo yatapunguza foleni za Dar es salaam na kuharakisha uchumi.

Akiongea leo April 16,2025 Bungeni Jijini Dodoma wakati wa hotuba yake kuhusu makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2025/2026, Waziri wa TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa amesema “Kwa muda mrefu Watu wa Jiji la Dar es salaam wamekuwa wakisubiri, wengine kwa matumaini, wengine kwa mashaka lakini wote kwa kiu ya mabadiliko, leo kwa mara ya kwanza tunasema, subira yao haikuwa ya bure, kupitia ubia kati ya Serikali na Sekta binafsi (PPP), tumefanikisha hatua ya kihistoria kusaini mikataba na watoa huduma watatu wa uendeshaji wa awamu ya pili ya mabasi yaendayo haraka”

"Hili ni tukio la mwanzo wa zama mpya siyo tena hadithi ya ahadi zisizotekelezwa, bali ya huduma bora zinazoonekana na kuguswa ‘Great things take time’, Wanafalsafa wanasema, ‘Mambo makubwa yanahitaji muda’ hatua hii si tu ununuzi wa huduma, bali ni ununuzi wa matumaini mapya kwa wakazi wa Jiji letu, hatutaki kurudia makosa ya jana, bali tunajenga mfumo imara, unaozingatia ubora, ufanisi na heshima kwa muda na maisha ya abiria"

"Hope is being able to see that there is light despite all the darkness’ – Desmond Tutu, kwa miaka mingi Wananchi wamepitia usumbufu, foleni zisizokwisha na huduma zisizoeleweka lakimi, tunasema kwa sauti ya matumaini, nuru inaanza kuonekana, mabasi haya hayatakuwa tu magari ya kusafirisha Watu, yatakuwa magari ya kusukuma uchumi, kuunganisha fursa na kupunguza mzigo wa maisha ya kila siku, ‘Progress is not in enhancing what is, but in advancing toward what will be" – Khalil Gibran.

"Mradi huu unaonesha jinsi tunavyotoka kwenye kilichozoeleka foleni, ajali, uchakavu na kuelekea kwenye kile kinachowezekana, usafiri wa kisasa, wa heshima, wa watu wote, tunajenga mfumo wa usafiri wa umma ambao utaweka heshima kwa abiria, uwajibikaji kwa watoa huduma na thamani kwa kila senti inayowekezwa"
 
Hapa Makonde Mbezi beach utanuzi wa barabara umepamba moto

CCM oyeee
 
Hii ndio press release au kuna nyingine tusubirie? Nolitegemea tujue nani na nani wamepewa hiyo mikataba ya kuendesha mwendokasi, kwa vigezo na masharti gani, ila nimesikitishwa kuona maneno ya Desmond Tutu ambayo hata raia mwingine anaweza ku-quote na kuleta ladha kwenye bandiko lake.
 
Maneno mengi, hamna subtance!
 
Njia zote ziingizwe kwenye shindani badala ya monopoly, hao wenye mabasi ya blue wananyanyasa sana watu, waingiziwe mekundu na rangi zingine
 
Taifa limejaa ujinga mtupu. Alipewa Kisena Kaharibu hakufanywa lolote/chochote, Serikali wameendesha mradi, madudu matupu.

Leo wanapeana ulaji watapiga halafu watatafuta mwendeshaji mwingine kama kawaida yao.

Mtanzania aendeshe mradi?

Ndio maana huwa natamani hata nchi wangepewa wawekezaji wanaojielewa, labda tungesogea hata hatua moja mbele.
 
Nadhani ni mambo ya nipe nikupe,Hivi ni mjinga gani anaweza kushindwa kuendesha biashara ya mwendokasi? Wakati umepewa barababra za upendeleo, vituo vya upendeleo, njia za upendeleo,kodi ndogo,mtaji,karakana za taifa,Mwendokasi haisimamishwi na traffic kama daladala.
Lakini haya yote ukiangalia kuna mkono wa mtu asiyejua biashara hiyo lakini analazimisha and i think is very powerful don.,
Usiri usiri usiokuwa na tija.
Kafulila Bwana PPP wakisema unasindikiza incompetence utasema sio kweli,lakini jibu ndio hilo.Kwanza ni aibu hata kulizungumzia.
 

Mstaskia wamepewa waarabu tena kuanzia viwanja vya ndege, misitu, bandari sasa hata mabasi haruwezi kuendesha. Mama oyee
 
Hiyo mikataba wanasaini ya nn wakati uongozi wao umefikia tamati...hii inchi kweli tunahitaji katiba mpya.
 
Wamepewa watu gani? ukute ni waarabu tena.
Huo wa mwendokasi wangenipa tu Mamndenyi waone
 
Mtihani kweli wabunge wenziwe wanagonga meza kama kawaida,ameandika na akairudia kuisoma hapo ndio amemwaga vitu,Mkwe wa Samia huyo kwao Nyamisati hamna barabara.
 
Ingawa kwa kuchelewa ila BORA , maana ninyi Serikali ya CCM hamuwezi kusimamia chochote zaidi ya kuingiza KURA feki kwenye masanduku ya kura kupitia Walimu na Mapolice wenye vibegi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…