Mchele wa plastic; Clouds Fm yaiumbua TFDA

Mchele wa plastic; Clouds Fm yaiumbua TFDA

mmmm kama ni kweli......😳 basi huu ni ukweli mchungu🙁🙁,umakini wa ziada unahitajika
 
Ikumbukwe wiki kadhaa zimepita paliibuka uvumi wa uwepo wa mchele wa plastic hapa nchini unaosadikiwa kutoka nchini china. Lakini baada ya muda TFDA waliibuka na kusema hakuna kitu kama hicho hapa nchini.

Leo hii katika kipindi cha cha "leo tena" watangazaji wamesema huo mchele waliletewa jana na walifinyanga tonge na kuurusha chini na ulikua unadunda kabisa. Na mpaka naandika uzi huu wamesema huo mchele wanao hapo studio.

Chanzo: Clouds Fm

My Take;
TFDA badala ya kukaa ofisini mnapulizwa kiyoyozi kwa nini msikimbie hapo mikocheni kwenye studio za clouds fm mkachukue sample yao mkaipime pia.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kati ya hao claus wako waliosomea uandishi na utangazajiwa habari za ushilawadu na TFDA waliosomea chakula na dawa ni nani anayeweza kutoa jibu la kisayansi?

Nani aliyewadanganya kuwa kudunda ndio SI unit ya plastic?
 
Umesema kweli mkuu, kama Clouds wamefikia hapo ni vyema serikali wakakifunga hicho kituo wasije kuambukiza ujinga wao vijana wetu..

Umesema kweli hao watangazaji ni wajinga, wapumbavu, malofa!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Hata humu tupo malofa na wapumbavu wengi tena sana yani watu wanavyo jisifu kila leo humu kuwa wana uwezo wa kufikiri nje ya box na kuhoji lakini bado wana amini bila kufikiri kuwa kuna mchele wa plastic....
Upumbavu na ulofa wa kusema kuna mchele wa plastic umechangiwa na ujinga wa kuleta habari za kijinga humu.....
 
VP kuhusu mchele halisi wamejaribu kuufinyanga na kuudundisha chini wakaona haudundi,Sina tatizo na TFDA

Sent using Jamii Forums mobile app
Mi nashindwa kuwaelewa wanao jiita great thinker wanashindwa kujiuliza hata tabia ya plastic...
Hivi kweli unaweza pika plastic ikaiva na ikapoa na ukaila halafu na digestion ikafanyika kama kawaida?
Hivi kweli tunahitaji kuwa wanasayansi kujua kuwa haiwezekani kuwa na mchele wa plastic?
 
Tonge la wali haliwezi kudunda kamwe...ukilitupa chini linasambaa ama linaseleleka na si kudunda kama mpira,
huo ndo uelewa wangu mie na nina uzoefu na aina mbalimbali za matonge
Na
1. Plastic haipikiki ( ukiipika itagandiana kwenye sufuria na kubadilika umbile

2. Plastiki haitafuniki

3. Plastiki haisagiki tumboni na wala haiozi ( ukiula unautoa hivyo hivyo )

4. Plastic haiwezi kuwa na harufu kama ya wali

5. Kwa mtumiaji wa wali wa siku nyingi kama ungekuwepo nchele wa aina hiyo, basi ukiweka mdomoni tuu ungehisi kitu cha ajabu

6. Garama za kuzalisha kitu kama hicho ni kubwa kuliko mchele wa kulimwa

Hakuna ,kitu cha namna hiyo ninyi suseni sisi tunakulaga wali tuu, ninyi suseni mchicha ( eti kidudumtu) sisi tunakulaga na kidudu mwenyewe
 
Kati ya hao claus wako waliosomea uandishi na utangazajiwa habari za ushilawadu na TFDA waliosomea chakula na dawa ni nani anayeweza kutoa jibu la kisayansi?

Nani aliyewadanganya kuwa kudunda ndio SI unit ya plastic?
Kwanza ni ulofa na upumbavu kabisa watangazaji kujadili mambo ya kijinga kama yale...eti mchele wa plastic
 
Na
1. Plastic haipikiki ( ukiipika itagandiana kwenye sufuria na kubadilika umbile

2. Plastiki haitafuniki

3. Plastiki haisagiki tumboni na wala haiozi ( ukiula unautoa hivyo hivyo )

4. Plastic haiwezi kuwa na harufu kama ya wali

5. Kwa mtumiaji wa wali wa siku nyingi kama ungekuwepo nchele wa aina hiyo, basi ukiweka mdomoni tuu ungehisi kitu cha ajabu

6. Garama za kuzalisha kitu kama hicho ni kubwa kuliko mchele wa kulimwa

Hakuna ,kitu cha namna hiyo ninyi suseni sisi tunakulaga wali tuu, ninyi suseni mchicha ( eti kidudumtu) sisi tunakulaga na kidudu mwenyewe
Na ukiiweka kwenye sahani ikipoa ina ganda.
Kwakweli ni ulofa na upumbavu kusema kuna mchele wa plastic.
 
Clouds ni chombo cha habari. Kazi yake ni kuhabarisha!

Wizara ya afya ipo kwaajili ya kufuatilia mambo yote yanayohusiana na afya za wananchi.

Kwa maelezo hayo mafupi, nafikiri itakua umeelewa ni nani anatakiwa kuwajibika na kwa namna gani.

Nikutakie siku njema mkuu!

- KANA -
Sio kwamba wana habari bali wana sambaza ulofa na upumbavu kabisa hivi huo utangazaji wa kupotosha mliusomea wapi? kwanini hawakuchua huo mchele na kuupeleka TFDA? Hivi kweli ina hitaji kuwa mwana sayansi kujua kuwa kuna mchele wa plastic? Huu wanaofanya haao watangazi ni ulofa na upumbavu? hivi wameshindwa ku google na kujua tabia za plastic?
 
hao clouds fm plastic wanaijua vizuri kwel? walitakiwa waseme mchele feki lakini sio mchele wa plastic. melting point ya plastic ni 130 -170° sasa napata ukakasi pale kuwa mchele unafinywa mpaka unafinyagika kwa joto la kawaida. kwa kawaida binadamu labda ufinyange kwa kutumia industrial groves.

lazima tulipe kodi
 
Hv Claudz Ni Media Ambayo Habar Zake Mtu Unaweza Zchukulia Serious? Labda Udaku Wa Wasanii, Yaan Kabisa Mtu Unakuja Na Habar Et Umeickia Claudz, Utakua Unashda Ww.
 
hao clouds fm plastic wanaijua vizuri kwel? walitakiwa waseme mchele feki lakini sio mchele wa plastic. melting point ya plastic ni 130 -170° sasa napata ukakasi pale kuwa mchele unafinywa mpaka unafinyagika kwa joto la kawaida. kwa kawaida binadamu labda ufinyange kwa kutumia industrial groves.

lazima tulipe kodi
hahahaha hao ni malofa na wapumbavu kabisa wanapotosha jamii kwa ulofa na upumbavu wao hivi hilo joto linaweza kupatika kabisa kwenye maji ya kupikia wali hahhaha unajua.
Bado najiuliza kweli inahitaji kuwa mwana sayansi kujua hili jambo halipo kabisa.......
 
Tatizo kipimo kimekuwa too cheap yaani kuudundisha chini ukadunda kama kitenesi ndo kusema ni plastic, kwanini wasijaribu kuuchoma moto km utayeyuka na kuwa ujiuji hapo sawa. Hiyo ya kudundisha chini ni local sana

Mhhhh kwani mchele wa kawaida huwa unadunda? We uoni kua Ni kasoro hiyo? WA tz sijui tumelogwa na nan
 
Back
Top Bottom