Mchele wa plastic; Clouds Fm yaiumbua TFDA

Mchele wa plastic; Clouds Fm yaiumbua TFDA

Elimu, Elimu,Elimu. Watu wakielimika hawawezi kuamini porojo kama hizi. Tujiulize ni watu wangapi wako hospital wanatibiwa kwa kula huo mchele? Mfumo wa uyeyushaji wa chakula tumboni hauwezi kuyeyusha plastic, kwa hiyo watu wengi sana wangekuwa wamedhurika. Hata kutafuna tu, meno gani ya binadamu yanaweza kutafuna plastic hadi kumeza??
Mimi kinachonishangaza ni wanao jiita great thinkers kuamini kirahisi kuamini kuna mchele wa plastic...HAHAHHAHAHA
 
Ikumbukwe wiki kadhaa zimepita paliibuka uvumi wa uwepo wa mchele wa plastic hapa nchini unaosadikiwa kutoka nchini china. Lakini baada ya muda TFDA waliibuka na kusema hakuna kitu kama hicho hapa nchini.

Leo hii katika kipindi cha cha "leo tena" watangazaji wamesema huo mchele waliletewa jana na walifinyanga tonge na kuurusha chini na ulikua unadunda kabisa. Na mpaka naandika uzi huu wamesema huo mchele wanao hapo studio.

Chanzo: Clouds Fm

My Take;
TFDA badala ya kukaa ofisini mnapulizwa kiyoyozi kwa nini msikimbie hapo mikocheni kwenye studio za clouds fm mkachukue sample yao mkaipime pia.

Sent using Jamii Forums mobile app
Plastic inasifa zake (features) na mchele una sifa zake (features). Sifa (features) za mchele haziwezi kuwa za Plastic ! Kwa mfano mchele ukiliwa unageuka mavi, ila ukila plastic ni operation tu inakufaa kuokoa maisha yako. Hivyo kujadili mada kama hii inaonyesha jinsi mbumbumbu walivyo mbumbumbu. Si ajabu wale wanakijiji waliitana wakaua watu wa serikali na kuchoma moto gari lao kwa uzushi kuwa wanyonya damu. Wakati lipo shirika la damu salama, na watu huenda kwa hiari kukamuliwa damu !
 
wametumia kipimo gan kugundua ni wa plastic? kwa nini usiitwe mchele usiofaa baada ya kupimwa kwanza?au kuthibitishwa kuwa ni plastic?
 
Ikumbukwe wiki kadhaa zimepita paliibuka uvumi wa uwepo wa mchele wa plastic hapa nchini unaosadikiwa kutoka nchini china. Lakini baada ya muda TFDA waliibuka na kusema hakuna kitu kama hicho hapa nchini.

Leo hii katika kipindi cha cha "leo tena" watangazaji wamesema huo mchele waliletewa jana na walifinyanga tonge na kuurusha chini na ulikua unadunda kabisa. Na mpaka naandika uzi huu wamesema huo mchele wanao hapo studio.

Chanzo: Clouds Fm

My Take;
TFDA badala ya kukaa ofisini mnapulizwa kiyoyozi kwa nini msikimbie hapo mikocheni kwenye studio za clouds fm mkachukue sample yao mkaipime pia.

Sent using Jamii Forums mobile app
Jaribu kuufinyanga ule mchele wako wa Mbeya ufinyage sana uone kama haudundi, mbona ni kawaida kwa mchele? Sasa kama hao Clouds wana maabara hapo studio na wataalam watupe maelezo ya kina. Ni upumbavu kuhitimisha kuwa mchele ni wa plastiki eti kwa kwa sababu umedunda mbona usiodunda hamtuoneshi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sisi pia ofisi kwetu tunao tunafatilia kwanza hatua zakisheria hawa tfda hawaeleweki na alama kubwa ukitaka kuutambua kirahisi wacha moto katika jiko weka mkaa Halafu umwage unawaka km makaratasi ya nailon kabisa Halafu ukiwa unawaka unashikana Kabisaaaaaa pamoja pamoja km nailon inavyofanya kazi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo kipimo kimekuwa too cheap yaani kuudundisha chini ukadunda kama kitenesi ndo kusema ni plastic, kwanini wasijaribu kuuchoma moto km utayeyuka na kuwa ujiuji hapo sawa. Hiyo ya kudundisha chini ni local sana
Wakati mwingine hata wasomi wa kitanzania nawaona kama bado elimu haiwasaidii!
Daktari anaweza kupokea mgonjwa,na akaeleza anaumwa "mchango!"Hii ni mwanzo tu,kwani ndiyo lugha anayoweza kuiongea mtu wa kawaida.
Ni kazi ya daktari kuchunguza kujua mchango ni ugonjwa gani.
Sasa watu wanaposema plastic,ni kwa vile wao si wakemia na hivyo hiyo ni lugha ya kuonesha tu si kitu cha kawaida.Inapotokea msomi kama wewe unashangaa eti uchunguzi wao ni too local,ulitaka watangazaji wachunguze vipi zaidi ya hicho wanachofanya?
Hoja ni aina gani ya Michele huo,na imekuwaje ukawa hivyo?
Je ni mchele halisi ama ni synthetic!Kwani katika dunia ya sasa kila kitu kinawezekana kwa nini isiwe huo mchele unaoonekana bandia?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo kipimo kimekuwa too cheap yaani kuudundisha chini ukadunda kama kitenesi ndo kusema ni plastic, kwanini wasijaribu kuuchoma moto km utayeyuka na kuwa ujiuji hapo sawa. Hiyo ya kudundisha chini ni local sana
Uko sahihi sana mkuu. Ubwabwa wote hudunda ukifanywa hivyo na hiyo michezo tumeicheza sana utotoni siku kukiwa na shibe nyumbani tena kwa mchele ambao tumelima wenyewe na kuuona ukikua.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo kipimo kimekuwa too cheap yaani kuudundisha chini ukadunda kama kitenesi ndo kusema ni plastic, kwanini wasijaribu kuuchoma moto km utayeyuka na kuwa ujiuji hapo sawa. Hiyo ya kudundisha chini ni local sana
Wakati mwimgine utumie akili kufikiri. Unaeza chukua tonge la wali wa mchele wa kawaida ukilidundusha likadunDa??? Huo mchele km ni kweli upo hivyo basi exactly sio wa kawaida. Vitu vingine huwa mnabisha hamtumii hata akili kufikiria???

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakati mwimgine utumie akili kufikiri. Unaeza chukua tonge la wali wa mchele wa kawaida ukilidundusha likadunDa??? Huo mchele km ni kweli upo hivyo basi exactly sio wa kawaida. Vitu vingine huwa mnabisha hamtumii hata akili kufikiria???

Sent using Jamii Forums mobile app
Me nnimeshashuhudia hiyo testing ya kudundisha wali wa michele ya aina zote mbili wa kawaida na unaoshukiwa kuwa wa plastic na yote ilidunda kwa level zinazofanana, hence majibu ya research yakawa ni negative. Labda wewe unayewaza kwa kichwa utuambie utafiti wako umefikia wapi
 
Wasomi acheni argument za kitoto!Huku usukumani MTU anaweza akaja hospitali anasema anaumwa "nyoka"(nzoka)Lakini kumbe kiuhalisia anapata maumivu ya vichomi!
Sasa ikitokea wewe ndio daktari utaanza kumuuliza huyo nyoka ulimuona?Ana rangi gani?Mgonjwa atakushangaa tu na ataona unamdharau kwani hiyo ni lugha ya watu wa kawaida,kwa hiyo ni kazi yako kujua anaumwa nini.
Kwa TFDA kuwapuuza watu kwa sababu kama hizi ninazoziona hapa,ni dalili kuwa kiburi cha elimu na jeuri ya rushwa inaweza kuwa ndiyo inayowaongoza.
Nashauri huo mchele upelekwe maabara za nchi nyingine maana watu hawa kama wamekula mrungula,hawawezi kutuambia ni kitu gani hicho.
Sisi wananchi lengo letu ni kujua kama huo ni halisi ama umetengenezwa kiwandani kwa material yoyote ambayo si chakula

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nikuulize swali Kijana wa leo hivi unaamini kabisa kwamba kuna mchele wa plastic?Hembu chukua hata bomba la dripu katakata vipande vidogo size ya mchele then bandika maji kwenye sufuria/rice cooker weka na mafuta ya kutosha bila kusahau chumvi na njegere na karoti kwa mbali then pika mpaka kiive then pakua weka kwenye sahani uone utakachokutana nacho....Haihitaji rocket science kun'gamua vitu vidogo kama hivi Mzee baba,, kwa kifupi hakuna kitu kama hicho.
Umetisha mkuu, nitarudi kuangalia amejibu nini.
 
BBC walishalitolea maelezo, walisema mchele wa kawaida ukipikwa vizuri ukaviringwa kama mpira unaweza kudunda kama inavyoonyeshwa na wala siyo plastic! It is just a myth! Angalizo, hii haimaanishi tfda wasichunguze!

Sent using Jamii Forums mobile app
Tukiambiwa tufanye tafiti za wa nyama hatuwezi,tafiti kibao hatuwezi Hata za wali tunaoula kila siku Naona hatuwezi ufanyia tafiti?? We uchukua uwe wali wa kupika nyumbani kwako au kwa mama ntilie au mgahawani viringisha tongue lako halafu lidundishe ulinganishe na majibu ya Hao BBC unaowataja hapa. Akili za kupewa changanya na za kwako
 
Back
Top Bottom