Mchawi mtu mbaya sana, anaweza kumuonea wivu muuza genge huku yeye ana hardware anawapanga foleni wateja

Kiboko ya Jiwe

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
12,705
36,157
Mchawi ni mtu mshenzi, hapaswi kuwepo kwenye jamii ya watu wastaarabu. Uchawi dhima yake kuu ni wivu.

Anaweza akawa na duka kubwa la vifaa vya ujenzi akapanga wateja kutwakutwa lakini akapandwa na pepo la wivu (uchawi) juu ya mtu anayeuza mihogo ya kukaangwa pembeni yake eti kisa Jamaa anauza sana mihogo.

Anamtoa roho au anampa ulemavu ili ateseke.Mchawi akikomaa sana anaanza kuchukia mafanikio hata ya mtoto wake wa kumzaa. Kuwa makini kazini, mtaani, kwenye biashara n.k. Mimi naongea kitu ambacho nakifahamu.

Kwenye ukoo wetu ukiinuka tu kazi unayo, utapatwa na matatizo mpaka unyooke. Kuna ndugu yetu kavurugwa na mchawi kapigika si mchezo, anadhurula tu hapa Dar. Anataka kuuza site yake ambayo kaanza kujenga hapati mteja. Kila akishusha bei wapi.

Wewe chukulia poa ipo siku utafanywa kafara na ndugu yako wa damu.
 
Mungu angewapa binaadamu kutoa uhai kwa binaadamu wenzao, hi dunia ingekua haina watu tena, watu wana roho mbaya anatamani abaki duniani peke yake na familia yake.
 
Mchawi ni mtu mshenzi, hapaswi kuwepo kwenye jamii ya watu wastaarabu. Uchawi dhima yake kuu ni wivu.

Anaweza akawa na duka kubwa la vifaa vya ujenzi akapanga wateja kutwakutwa lakini akapandwa na pepo la wivu (uchawi) juu ya mtu anayeuza mihogo ya kukaangwa pembeni yake eti kisa Jamaa anauza sana mihogo.

Anamtoa roho au anampa ulemavu ili ateseke.Mchawi akikomaa sana anaanza kuchukia mafanikio hata ya mtoto wake wa kumzaa. Kuwa makini kazini, mtaani, kwenye biashara n.k. Mimi naongea kitu ambacho nakifahamu.

Kwenye ukoo wetu ukiinuka tu kazi unayo, utapatwa na matatizo mpaka unyooke. Kuna ndugu yetu kavurugwa na mchawi kapigika si mchezo, anadhurula tu hapa Dar. Anataka kuuza site yake ambayo kaanza kujenga hapati mteja. Kila akishusha bei wapi.

Wewe chukulia poa ipo siku utafanywa kafara na ndugu yako wa damu.
Watu wengi udhani biashara ya genge sio kazi lakini genge ni kazi inayolipa sana muuza genge akiuza 200000 kwa siku akosi faida ya sh 70,000
 
Back
Top Bottom