Mchange na Mnyika live on Startv asubuhi, Agosti 16, 2014

Mchange na Mnyika live on Startv asubuhi, Agosti 16, 2014

attachment.php

1.hawa polisi waliomuua mwangosi wametumwa na chadema?

Aliyemuua Mwangosi anajulikana kwa jina,sura na anuani. Msipoteze muda, nendeni mahakamani.
 
jualiana unazaa lini

Wakati UKIMWI unaingia nchini kupitia mkoa wa Kagera, ulikuwa na majina mengi kama "slim", "Juliana" nk. Baada ya watanzania kutoa jina ndipo wakenya wakauita "UKIMWI" baada ya kutafsiri kutoka kwenye AIDS.

Sasa hapa naanza kuamini na naona kuna uhalisia fulani wa jina la mtu kubeba tabia ya mwenye jina! Sasa huyu Juliana anatabia zile zile za "juliana-UKIMWI". Anajifanya anakupa raha kumbe ni msaliti wa uhai wa mwanadamu. Yaani Taifa lina angamia kwa sababu ya virus vya juliana, wakiwemo akina Mchange na wachumia tumbo wengine.
 
Mnae mwanasheria mnayemuamini kuwa ana akili na mwerevu kuliko wanasheria wote duniani anaitwa TUNDU, kwanini msimpigie magoti aende akafungue kesi dhidi ya MCHANGE..??? jaribuni kufanya hivyo, kama mnaweza.
hujiulizi kwa nini polisi hawawakamati mnaowaita wauaji?simple..ni propaganda za lumumba.,nyinyi mlishafukuzwa chadema tulieni na ccm yenu,the movement is here to stay,na tatizo la kutumiwa na magaidi ya ccm ni kuwa lazima wakuue mwisho wa siku because you know too much.
 
Aliyemuua Mwangosi anajulikana kwa jina,sura na anuani. Msipoteze muda, nendeni mahakamani.

kwani mwangosi alikuwa kiongozi wa chadema?kuna uhusiano gani kati ya chadema na mwangosi?as far as i know,mwangosi alikuwa ni mwanahabari kama alivyo pasco wa jf!!!
 
Aliyemuua Mwangosi anajulikana kwa jina,sura na anuani. Msipoteze muda, nendeni mahakamani.


Umesema umesikiliza Star Tv leo asubuhi, kwa maelezo ya Machange wauwaji wa Daudi mwangosi ni

1. Dr W. P Slaa

2. A . Mbowe.

Juliana umesema unakubaliana na maelezo ya Habibu Mchange, tunakuuliza ndiyo Mbowe na Dr Slaa.

Tunataka kauli yako sio kuzunguuka. Lengo nikuthibitisha kwamba Mchange yupo sahihi kwa kifo cha mwangosi.
 
na waambie polisi wawakamate viongozi wa chadema wapelekwe mahakamani na hapo ndio mtamjua safari,mabere,lissu ni watu gani!
Nyie ndio mmeshutumiwa,.kwa kawaida anayeshutumiwa huwa anaenda mahakamani kufungua kesi, sasa nyie mmeshutumiwa kwanini msifungue kesi dhidi ya aliyewashutumu.
 
NCHI HII SIO SALAMA TENA.

Tanzania ni nchi yangu tena ni mahali nilipozaliwa, kwa kuwa nchi ni yangu sina budi kujivunia nchi yangu tena inayosifika kama kisiwa cha amani...dah ni kama ndoto..kwa sasa maneno haya yanakuwa adimu kinywani na akilini kwa sasa. Kusema najivunia Tanzania nchi yangu na kusema Tanzania ni nchi ama kisiwa cha amani kumekuwa na ukakasi kwa sasa. Kila ninapojaribu kusema nashindwa kwani maneno yanayonijia ni "navumilia kuwa mtanzania" Kwani Tanzania sio salama tena.

Ninaposema Tanzania sio salama tena yawezekana wengi msinielewe kutokana na tongo tongo zito lililojazwa na watawala kwenye macho na akili za watanzania walio wengi kwa kauli laini na nyororo kuwa "NCHI YETU NI YA AMANI" Neno amani limekuwa kama turufu ya watawala kuendelea kujitafutia uhalali batili wa kisiasa (fake political legitimacy).

Ni kama nchi hii haina polisi wala usalama wa Taifa tena kwa mambo yanayoendelea. Nimeshangazwa na kauli za Habib mchange kwamba alishiriki kuandaa mauwaji ya Mwanahabari Mwangosi kule mufundi kwa kushirikiana na viongozi wa CHADEMA na anadai kwamba Mwangosi aliuliwa na wanachama wa CHADEMA kwani walivalishwa sare za polisi pamoja na kupewa silaha na kumuua Daudi Mwangosi aliyekuwa mpiga picha wa CHANEL TEN na kudai kuwa mpango huu ulisukwa na kuratibiwa kwa umakini mkubwa na viongozi waandamizi wa CHADEMA ikiwa ni pamoja na kumuandaa yule aliyepiga picha.

Habibu Mchange ameuaminisha uma kuwa yule askari anayetuhumiwa kumuuwa Mwangosi ni Mwanachama wa CHADEMA na alitumwa kufanya hivyo na viongozi waandamizi wa CHADEMA.

Maswali ya kujiuliza:-

(1) Kama ana ushahidi wote huo ni kwanini asiuwasilishe kwenye vyombo vya Dola ili wahusika wachukuliwe hatua?

(2)Inakumbukwa kuwa katika tukio lile alikuwepo Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Kamanda Kamuhanda. Je Kamuhanda nae ni Mwana CHADEMA?

(3) Kama Habibu Mchange Kakiri Mwenyewe kuujua vyema mkakati kwanini vyombo vya dola havijachukua hatua dhidi yake?

(4) Kwakuwa tukio lile anadai wanachadema walipewa silaha na sare za jeshi la polisi kwanini polisi na usalama wa Taifa wasimkamate ili awaeleze sare hizo pamoja na silaha zilipotoka?

Ukimya wa jeshi la polisi pamoja na usalama wa Taifa unamaniisha kuwa hii nchi sio salama tena.

Itakumbukwa kuwa hivi karibuni madiwani wawili wa chadema waliohamia CCM kwa kurubuniwa na baadae kurudi tena CHADEMA walijitokeza mbeza ya vyombo vya habari na kuweka wazi mkakati wa kigaidi uliosukwa na viongozi waandamizi wa CCM na serikali kwa kushirikiana na HABIBU MCHANGE juu ya kutaka kulipua helcopta ya CHADEMA mjini Shinyanga ili kumuuwa Dr.Slaa, John Mnyika pamoja na mbunge wa maswa mashariki.

Je jeshi la polisi pamoja na usalama wa Taifa wamechukua hatua gani dhidi ya wahusika wa tukio hili ovu?

Je polisi na usalama wa Taifa wamechukua hatua gani ili kuweza kupata ushahidi wa kutosha kutoka kwa Madiwani wale wawili?

Ukimya wa Jeshi la polisi na usalama wa Taifa unamaanisha kuwa nchii hii sio salama tena.

Mchange anadai kuwa Viongozi wa CHADEMA wakiongozwa na Freeman Aikaeli Mbowe walishiriki kumuua aliyekuwa makamu mwenyekiti wa CHADEMA na mbunge CHACHA WANGWE.

Kwanini polisi wasimkamate MCHANGE ili aisaidie polisi juu ya sakata hili?

Ukimya wa jeshi la polisi na usalama wa Taifa unamaanisha nchi hii sio salama tena.

Kama kuna ukweli kwenye haya wahusika wote wakamatwe ili sheria iweze kuchukua mkondo wake.

Kama swala hili ni muendelezo wa siasa za kijinga ninaomba viongozi wa CHADEMA wamchukulie hatua za kisheria HABIB MCHANGE ili kukomesha upuuzi huu.

Amani kwenu...N.NGOWI.

Nime-record kipindi chote cha mazungumzo hayo ya STAR TV, Kesho J3 nitawasiliana na Wanasheria ili nione namna gani naweza kufungua Kesi mahakamani kuhusu mauaji ya Mwangosi, natumai ushahidi huu unaweza kunisaidia. Nitawasiliana na Tundu Lisu, Mchungaji Mtikila, John Mnyika na wana-JF ambao wataweza kunisaidia. Wana-JF mnisaidie kwenye masuala ya pesa pale nitakapokwama maana kuendesha kesi kunahitaji pesa. KWA HILI MPAKA KIELEWEKE.
 
Kama amazungumza uzushi, ni DEFAMATION mnaweza kwenda mahakamani kumfungulia mashitaka Habib kama mnaona alichokisema mbele ya vyombo vya habari ni uzushi na maneno ya kutengeneza.

HABIBU ANAFAHAMIKA KWAMBA HANA KAZI na ANAISHI KWA KUTUMWA NA WALA HATUNA SHIDA NAYE KWA HILO , LAKINI KUNA HILI LA MWANGOSI AMBALO KATIKA TUME ZOTE ( HATA ZILE ZA KIZUSHI )HAZIKUWAHI KUSEMA UONGO HUU ,AMBAO WEWE UNAUSAPOTI , HAKIKA LAANA HUIKWEPI ! KUNA HILI PIA , DEREVA WA CHACHA WANGWE ALIHUKUMIWA JELA KWA YALIYOTOKEA , LAKINI BAADA YA MUDA MFUPI SANA AKATOLEWA KWA MSAMAHA WA RAIS ! HATA KAMA KUSOMA HUJUI BASI HATA PICHA HUONI ? LAANA YA UONGO KAMA HUU ILIWAHI KUMKUTA JOJI MARATO ,FUATILIA UTAJUA .
 
Wakati UKIMWI unaingia nchini kupitia mkoa wa Kagera, ulikuwa na majina mengi kama "slim", "Juliana" nk. Baada ya watanzania kutoa jina ndipo wakenya wakauita "UKIMWI" baada ya kutafsiri kutoka kwenye AIDS.

Sasa hapa naanza kuamini na naona kuna uhalisia fulani wa jina la mtu kubeba tabia ya mwenye jina! Sasa huyu Juliana anatabia zile zile za "juliana-UKIMWI". Anajifanya anakupa raha kumbe ni msaliti wa uhai wa mwanadamu. Yaani Taifa lina angamia kwa sababu ya virus vya juliana, wakiwemo akina Mchange na wachumia tumbo wengine.
Hoja dhaifu na ambayo haina uhusiano kabisa na linalojadiliwa hapa.
 
kwani mwangosi alikuwa kiongozi wa chadema?kuna uhusiano gani kati ya chadema na mwangosi?as far as i know,mwangosi alikuwa ni mwanahabari kama alivyo pasco wa jf!!!
Unahangaika na huyu ni kupoteza muda tu..........
 
HABIBU ANAFAHAMIKA KWAMBA HANA KAZI na ANAISHI KWA KUTUMWA NA WALA HATUNA SHIDA NAYE KWA HILO , LAKINI KUNA HILI LA MWANGOSI AMBALO KATIKA TUME ZOTE ( HATA ZILE ZA KIZUSHI )HAZIKUWAHI KUSEMA UONGO HUU ,AMBAO WEWE UNAUSAPOTI , HAKIKA LAANA HUIKWEPI ! KUNA HILI PIA , DEREVA WA CHACHA WANGWE ALIHUKUMIWA JELA KWA YALIYOTOKEA , LAKINI BAADA YA MUDA MFUPI SANA AKATOLEWA KWA MSAMAHA WA RAIS ! HATA KAMA KUSOMA HUJUI BASI HATA PICHA HUONI ? LAANA YA UONGO KAMA HUU ILIWAHI KUMKUTA JOJI MARATO ,FUATILIA UTAJUA .

Unamjua Deus Mallya..?
 
Nyie ndio mmeshutumiwa,.kwa kawaida anayeshutumiwa huwa anaenda mahakamani kufungua kesi, sasa nyie mmeshutumiwa kwanini msifungue kesi dhidi ya aliyewashutumu.


1. Nani alimpeleka Lwakatale Lumande? Polisi au sio, kwanini wasifanya vivyo hivyo kwahili?

hili jambo naona mnalifrahia amini nakuambia litamtoa nyongo Habibu Mchange, sio la kushangilia hata kidogo.

muonee huruma Habibu maana kitakachofuata maji yakimfika shingoni ccm na nyinyi akina Juliana mtamruka.

Mtamruka kwasababu, hakuna mwenye uwezo wa kupindisha maelezo na ushahidi wa kifo cha Daudi Mwangosi.
 
Habarini za jumapili wakuu,, Asubuhi ya leo nimemsilikiliza habibu hakika binafsi amenisikitisha ameniachia maswali mengi bila majibu kubwa nihili kwanini haya yasemwe leo alikuwa wapi muda wote wakati matendo yakihalifu yakiratibiwa na kutekelezwa? Ametamka bayana alikua nyuma keyboard wakati waharakati zote,amemtaja mnyika ktl tukio la tindiikali Igunga kuwa alihangaika siku mbili kuficha tindikali,kaeleza mauaji ya Mwangosi, Chacha Wangwe nk,,kimsingi mchange ameturusha nyuma sana kafumua vidonda vilivyo anza kupona kawatesa ndg wamarehemu ameifufua huzuni yao kwafaida yake naami anayo ajenda nahayuko pekeyake kunamradi anautekeleza nawapo wanaougharamia wanaugharimia ilikumliza tena mjane wa Mwangosi wanugharimia ili kuwaumiza upya watoto marehemu Wangwe wanayafanya hayakwafaida zao,, bado naami mchange hayuko peke yake wapo mabosi anaowatumikia Swali Habibu unamtumikia nani? ?
 
Ningestaajabu sana kama msaliti asingemuelewa msaliti mwenzie. Mtahangaika sana mwaka huu na mwaka kesho, lakini usaliti wenu kamwe hautafanikiwa.
 
Iwapo polisi hawatachukua hatua dhidi ya tuhuma hizo ni aidha ccm na polisi ndiyo waratibu wa mipango hiyo.

Na ikumbukwe kwamba polisi ndiyo watuhumiwa dhidi ya mauaji ya mwangosi.

Polisi, usalama wa taifa mnapeleka nchi wapiiiiiiiiiiiii?????????. Kikwete unafanya nini man?
 
Nimenza kusoma hii thread nilipofika na kukutana na mahubiri ya Ukanda.. ndio nikaishia hapo na stori yote nikaona kama katuni ya zombi ike ya necta!?

Chadema wanaendelea na chaguzi zao kila kona ya nchi.. kuanzia ngazi ya nyumba!

kweli kaka chdm inasonga mbele, walisema hatuna viongozi ngazi za chini kabisa sasa hivi wamejaa na kukubalika na wananchi kila kona ya tanzania, ngoja waendelee na propaganda zao kwani hawana la kufanya
 
Iwapo polisi hawatachukua hatua dhidi ya tuhuma hizo ni aidha ccm na polisi ndiyo waratibu wa mipango hiyo.

Na ikumbukwe kwamba polisi ndiyo watuhumiwa dhidi ya mauaji ya mwangosi.

Polisi, usalama wa taifa mnapeleka nchi wapiiiiiiiiiiiii?????????. Kikwete unafanya nini man?
Polisi wanafanya kazi zao kwa weledi mkubwa. Hawakurupuki tu
 
kweli kaka chdm inasonga mbele, walisema hatuna viongozi ngazi za chini kabisa sasa hivi wamejaa na kukubalika na wananchi kila kona ya tanzania, ngoja waendelee na propaganda zao kwani hawana la kufanya
Chadema imebaki jina tu
 
Back
Top Bottom