Mch. Gwajima: Mimi sio kama wale (kuhusu kashfa)

Mch. Gwajima: Mimi sio kama wale (kuhusu kashfa)

Mimi ni mkristu lakini watumishi dizaini ya gwajima,kakobe,mama lwakatare,mwingira siwakubali,
kama nakosea Mungu atanisamehe.

Ww kumbe ni mkristu na sio mkristo,ungekua mkristo ungechunga sana kauli zako
 
Gide MK yuko sawa, Mungu hapendi mwenye dhambi aangamie! Gide Mk hajahukumu alichosema ndicho binlia inasema zichunguzeni hizo roho! Tusiamini kila mtu, hata shetani hujigeuza awe malaika wa nuru.

hata ww sikuamini ha ha ha ha ha
 
He is nothing, just a scam burg selfish trash. U mimi mwingi! Kazi ya Ibirisi in action
 
Sawa wakuu nyote mlio comment dhidi ya mchg.Gwajima na wengine mnaopenda ku assassinate character za watumishi wa Mungu,lakini kumbukeni kuwa si vyema kuwahukumu na kuwatukana hata kama watakosea,badala yake waombeeni na hata kama wakikengeuka mlio wa Roho warejezeni tena kwa upole,huo ndio ukristo-let love lead!
Aidha kabla hujamnyoshea MTU YEYOTE kidole jichunguze wewe mwenyewe uone u mtakatifu/mwadilifu/mwema kiasi gani,yaani shughulikia banzi kwenye jicho lako kwanza kabla hujageukia boriti kwenye jicho la mwenzako?
Tusinukuu maandiko na kuyatumia kuwahukumu watu,badala yake tuwaombee rehema na hasa kama jambo baya likiwapata watumishi wa Mungu ni muhimu tuwaombee ili kazi yake iendelee.
Ndugu zangu,tusitofautiane na kunyosheana vidole kwa sababu ya dini na madhehebu yetu,tuheshimiane hata kama hatufanani kwa sababu sisi sote tu wanadamu tulioumbwa na Mungu mmoja.
Nahitimisha kwa kusema TUJIFUNZE kusameheana na kuombeana!
MWISHO: "let's not purchase a curse with such a low price-`condemnation'"
Thanks!

Triple hii unatafsiri vibaya au unachanganya, utamrejesha vipi mshirika ambaye hakiri kutenda dhambi? Tena dhambi ya wazi ya kumwaibisha kristo kwa wazi! Gwajima haonyeshwi kidole na mwanadamu ni Mungu. Hana budi kukiri mbele ya waumini wake na arudi ndani ya maji.Hakuna umaarufu ukifanya dhambi
 
Triple hii unatafsiri vibaya au unachanganya, utamrejesha vipi mshirika ambaye hakiri kutenda dhambi? Tena dhambi ya wazi ya kumwaibisha kristo kwa wazi! Gwajima haonyeshwi kidole na mwanadamu ni Mungu. Hana budi kukiri mbele ya waumini wake na arudi ndani ya maji.Hakuna umaarufu ukifanya dhambi

yaani saa kumi na mbili asubuhi umeamka na Gwajima..unalipwa bro!?
 
Mungu hafanyiwi mzaha atii, hakuna mwenye uwezo wa kufufua binadamu zaidi ya mungu kwa mtume wake. Mungu si Athumani jamani wala Renald
 
Mchungaji Gwajima asitake kubadilisha uelekeo wa tuhuma zake. Issue hapo si Flora kuhamia kwake bali ni yeye kutuhumiwa kuwa na mahusiano ya kinyumba na Flora. Kwani Flora kuishi hotelini naye akawa ndo mwezeshaji kuna tofauti gani na kuishi nyumbani kwake ama kuishi naye? Gwajima unachotakiwa kukifanya ni kuachana na hiyo tabia ya kuingilia ndoa za watu na kumpenda na kumheshimu mke wako uliyepewa na Mungu.
Ni mara ngapi umewatumia wake/ wadada ukaenda nao huko mikoani ukifikiri hutoweza kuonekana? Huko nako Mungu yupo cha maana utubu umtumikie Mungu kwa kadri atakavyokuwezesha. Simamia lile unalo fundisha na uache kuwapandikizia waumini wako viburi kwenye ndoa zao.......waheshimu wake na waume zao - waheshimu ndoa zao. Haijawahi kutokea na haitakuwepo hiyo philosophy yako eti ni "mume wa kiroho" nje ya yule mtu aliyepewa na Mungu. Mume/ mke aokoke/ asopookoka haibadili maana ya tafsi ya biblia. Waambie waumini wako tangu mwaka 2010 ni waumini wangapi wameachana na ndoa zao kutokana na wewe kuingilia mambo yao ya ndani? unafikiri kuingilia ndoa ni lazima uzini? Hata kumjengea mtu fikra za kuoheshimu mwenza wake kwenye ndoa nako ni kuingilia ndoas ambao ni mpango wa Mungu. unavyofurahia maisha na mke/ watoto wako kama familia hata wenzako walitaka na familia zao zifurahie hivyo hivyo.
Hizo pesa (mamilioni) unayojifanya kusaidia wale uliowavurugia ndoa zao wawe waume/ wake (kama mlivyofanya kwa Flora) hazisaidii kuinga jamii na hata kanisa unaloongoza.
 
1404516_10152047944048856_819595337_o.jpg
ndoa ndoano kweli wahenga walienena
 
Tatizo la Gwajima anajiona ama waumini wake wamejijengea himaya ya kuwa bila Gwajima utukufu wa Mungu hauwezi kuonekana. Gwajima is very trick.......ameandika vitabu vingi sana na amezungumza mambo mengi humo yanayowakingia kifua watumishi wa Mungu kama yeye. Moja ya mafundisho yake ni kuwa mtumishi wa mungu ambaye yeye anawarifaa kama "masihi wa mungu" akikosea hutakiwi kumwambia ama kumsema zaidi mwachie mungu adeal naye.
Hapa utaelewa ni kwa nini anafanya kiburi tena cha wazi kwa kuingilia ndoa za watu akijua hakuna hata mmoja wa waumini ama wasaidizi wake atakaye thubutu kumwambia chochote. Anasahau kuwa Mungu atasema naye hata aende popote?
 
Hata mfalme Daudi aliwahi kuyatamka maneno hayo sasa wote humu tunakushangaa wewe.
Aliokwambia utusemee ni nani?Hebu pelekeni utapeli wenu huko wazinzi wakubwa nyie.Eti "mimi sio kama wale" shame on you.
 
Bado alikuwa hotelini? Bill yake kwa kanisa imefikia bei gani? Ama zile Tsh. 9M zimemtosha?
Gwajima anasafiri karibuni.........Flora haruki naye? Hebu tujuzeni mliokaribu na huyo mkwapua wake za watu?
Msijali ataendelea kuwanunulia magari na kuwapamgishia nyumba.......ajira zenyewe si mnaona za shida?
 
Kushangiliwa si hoja ........ni watu gani wanaomshangilia? Ulitegemea wamzomee? Yawezekana hao hao waliokuwa wanamshangilia ndo hao hao anaotembea nao akielewa fika kuwa wengine ni wake za watu.
 
Mimi ni mkristu lakini watumishi dizaini ya gwajima,kakobe,mama lwakatare,mwingira siwakubali,kama nakosea Mungu atanisamehe.
Hakika mna tofauti kubwa,weye ni MKRISTU wao ni WAKRISTO. Hamtokaa mkafanana milele.
 
yaani saa kumi na mbili asubuhi umeamka na Gwajima..unalipwa bro!?
Anakusuteni na uongo wenu,wewe unatuletea hapa Uzi wa Gwajima amekuajili?au ndio kati ya wale wanaume mmepangishiwa nyumba na kununuliwa Noah na mchungaji mzinzi?
 
Tofauti na ilivyotarajiwa na wengi kuwa Mch. Gwajima angejibu kashfa iliyosambaa kwa kasi magazetini kumuhusisha yeye na kesi ya Mbasha ameibuka na kudai yeye sio kama wale.

Katika ibada ya jumapili hii iliyoudhuriwa na maelfu ya watu alisikika akisema, "mimi sio kama wale, sijibu hoja kama zile, mfano ukiwa unaoga alafu chizi akachukua nguo zako na ukamkimbiza nani ataonekana chizi?" akaendelea kusema nanukuu " tatizo la watanzania ni kuwa wakisikia kitu kipya kinaanza kwao badala ya kukithamini wanakididimiza ili kisiendelee, lakini mimi sio kama wao" aliendelea kusisitiza.

Mch. Gwajima alisema, "mimi kila mwaka naenda Japan na ninawalecture wajapan, ambao pia huja hapa kanisani zaidi ya 40 kila mwaka na mwaka huu watakuja Septemba, lakini watanzania hawashtuki na kuja kujifunza wao juu Ufufuo wa wafu wengi wao wanakalia kuandika stori kwenye magazeti lakini mimi sio kama wale"

Ingawa Mch. Gwajima hakueleza moja kwa moja kuhusu tukio la mbasha na maelezo yoyote lakini maneno haya yanaonyesha kujibu hoja zinazomuhusisha yeye na tukio hilo; aliendelea kusema kuwa, "Mimi nimehubiri nchi zaidi ya 53 duniani, na nyingi za ulaya na marekani alafu mtu amekaa magomeni miaka yote anatengeneza story ya gazeti unatarajia niijibu, mimi sio kama wale nimetumwa na nina kazi natakiwa kuifanya duniani na siwezi kufa mpaka niimalize." aliendelea kusema "inawezekana mlishawaangamiza wengi kabla ya mimi, kwa kuwatungia story hizo za uongo lakini mimi sio kama wale; na mwezi huu wa nane ninaendelea na mkutano Iringa; waache waandike lakini mimi ni chombo kingine na sio kama wale"

ibada hiyo ilikatishwa na kelele za waumini wake kila muda mfupi alipokuwa akiongea. Mimi sio kama Wale.
baadhi ya Clip za ibada hii unaweza kuzipata pia youtube!!!

Picha ya Mkutano wa Mch. Josephat Gwajima mkoani Tanga...

View attachment 165507

Picha ya Mkutano wa Mch. Josephat Gwajima mkoani Tanga...

Kushangiliwa si hoja ........ni watu gani wanaomshangilia? Ulitegemea wamzomee? Yawezekana hao hao waliokuwa wanamshangilia ndo hao hao anaotembea nao akielewa fika kuwa wengine ni wake za watu.
 
Naona hapa ni Mrs Gwajima (Mama Mchungaji) kushoto akiwa na mke mwenza (Flora Mbasha) katikati huku mumewe Emanuel Mbasha akiwa haelewi kinachoendelea. Si Mbasha ama Mama Gwajima aliyekuwa anaelewa kilichokuwa kinaendelea kati ya wawili hawa (Mch. Gwajima na Flora). Wanapewa deal la kwenda kuimba mikoani wanafikiri kwenye mikutano wanachekelea kumbe mshikaji anabanjua kwa kwenda mbele.
 
Back
Top Bottom