Mch. Gwajima: Mimi sio kama wale (kuhusu kashfa)

Mch. Gwajima: Mimi sio kama wale (kuhusu kashfa)

davidm

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2012
Posts
393
Reaction score
129
Tofauti na ilivyotarajiwa na wengi kuwa Mch. Gwajima angejibu kashfa iliyosambaa kwa kasi magazetini kumuhusisha yeye na kesi ya Mbasha ameibuka na kudai yeye sio kama wale.

Katika ibada ya jumapili hii iliyoudhuriwa na maelfu ya watu alisikika akisema, "mimi sio kama wale, sijibu hoja kama zile, mfano ukiwa unaoga alafu chizi akachukua nguo zako na ukamkimbiza nani ataonekana chizi?" akaendelea kusema nanukuu " tatizo la watanzania ni kuwa wakisikia kitu kipya kinaanza kwao badala ya kukithamini wanakididimiza ili kisiendelee, lakini mimi sio kama wao" aliendelea kusisitiza.

Mch. Gwajima alisema, "mimi kila mwaka naenda Japan na ninawalecture wajapan, ambao pia huja hapa kanisani zaidi ya 40 kila mwaka na mwaka huu watakuja Septemba, lakini watanzania hawashtuki na kuja kujifunza wao juu Ufufuo wa wafu wengi wao wanakalia kuandika stori kwenye magazeti lakini mimi sio kama wale"

Ingawa Mch. Gwajima hakueleza moja kwa moja kuhusu tukio la mbasha na maelezo yoyote lakini maneno haya yanaonyesha kujibu hoja zinazomuhusisha yeye na tukio hilo; aliendelea kusema kuwa, "Mimi nimehubiri nchi zaidi ya 53 duniani, na nyingi za ulaya na marekani alafu mtu amekaa magomeni miaka yote anatengeneza story ya gazeti unatarajia niijibu, mimi sio kama wale nimetumwa na nina kazi natakiwa kuifanya duniani na siwezi kufa mpaka niimalize." aliendelea kusema "inawezekana mlishawaangamiza wengi kabla ya mimi, kwa kuwatungia story hizo za uongo lakini mimi sio kama wale; na mwezi huu wa nane ninaendelea na mkutano Iringa; waache waandike lakini mimi ni chombo kingine na sio kama wale"

ibada hiyo ilikatishwa na kelele za waumini wake kila muda mfupi alipokuwa akiongea. Mimi sio kama Wale.
baadhi ya Clip za ibada hii unaweza kuzipata pia youtube!!!

Picha ya Mkutano wa Mch. Josephat Gwajima mkoani Tanga...

DSCN5511.JPG

Picha ya Mkutano wa Mch. Josephat Gwajima mkoani Tanga...
 
Hahahaaa jamaa kiboko naona flora alikua pembeni yke akitabasamu
 
majibu mepesi kwa kashfa nzito,.

Tunamwamini nani sasa,..
 
Mimi....mimi.....mimi.....mimi.....mimi......hii ni hatari kwa mtumishi wa Mungu kama kweli ameongea namna hii....mtumishi wa Mungu mbele za Mungu ni zaidi ya waamini wa kawaida kwakuwa ni muwakilishi wake yeye ili atukuzwe yeye.........Musa aliadhibiwa na Mungu na kuishia kuiona nchi ya ahadi kwa mbali kwa kosa ambalo leo tutaona lilikuwa dogo sana kuliko hata wale aliokuwa anawaongoza waliomkufukuru Mungu mara nyingi tu lakini ndio waliokuja kuiona nchi ya ahadi......Makosa ya Musa hasa pale alipowaambia wana wa Waisrael soma nukuu hapo chini....msisitizo kwenye nyekundu

Numbers 20:8-12 ESV
“Take the staff, and assemble the congregation, you and Aaron your brother, and tell the rock before their eyes to yield its water. So you shall bring water out of the rock for them and give drink to the congregation and their cattle.” 9 And Moses took the staff from before the Lord, as he commanded him. 10 Then Moses and Aaron gathered the assembly together before the rock, and he said to them, “Hear now, you rebels: shall we bring water for you out of this rock?” 11 And Moses lifted up his hand and struck the rock with his staff twice, and water came out abundantly, and the congregation drank, and their livestock. 12 And the Lord said to Moses and Aaron, “Because you did not believe in me, to uphold me as holy in the eyes of the people of Israel, therefore you shall not bring this assembly into the land that I have given them

“Hear now, you rebels: shall we bring water for you out of this rock?” Hii nukuu ilijaa ubinafsi (mimi...mimi..mimi..) na si Utukufu wa Mungu.Nadhani mtumishi anaweza kuteleza sometimes na namuomba Mungu aendelee kuwa simamia hawa watumishi wake ili wasisahau unyenyekevu na utumishi kama wa Yesu alipotoa mfano kwa kuwanawisha miguu wafuasi wake ili wajue wajibu wao mkuu ni utumishi.
 
Tapeli tu kwenda japani kunahusiana nini na tuhuma

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

Hii kauli ya ajabu sana, ndio maana huko serikalini wanabinafsisha mali zote kwa fikra duni kama hizi.
 
Tofauti na ilivyotarajiwa na wengi kuwa Mch. Gwajima angejibu kashfa iliyosambaa kwa kasi magazetini kumuhusisha yeye na kesi ya Mbasha imeibuka na kudai yeye sio kama wale.

Katika ibada ya jumapili hii iliyoudhuriwa na maelfu ya watu alisikika akisema, "mimi sio kama wale, sijibu hoja kama zile, mfano ukiwa unaoga alafu chizi akachukua nguo zako na ukamkimbiza nano ataonekana chizi?" akaendelea kusema nanukuu " tatizo la watanzania ni kuwa wakisikia kitu kipya kinaanza kwao badala ya kukothamini wanakididimiza lakini mimi sio kama wao" aliendelea kusisitiza.

Mch. Gwajima alisema, "mimi kila mwaka naenda Japan na ninawalecture wajapan ambao pia huja hapa kanisani zaidi ya 40 kila mwaka na mwaka huu watakuja Septemba, lakini watanzania hawashtuki na kuja kujifunza wao wanakalia kuandika stori kwenye magazeti lakini mimi sio kama wao"

Ingawa Mch. Gwajima hakueleza moja kwa moja kuhusu tukio la mbasha na maelezo yoyote lakini maneno haya yanaonyesha kujibu hoja zilizokinyume naye; aliendelea kusema, "Mimi nimehubiri nchi zaidi ya 53 duniani, na nyingi za ulaya na marekani alafu mtu amekaa magomeni miaka yote anatengeneza story ya gazeti unatarajia niijibu, mimi sio kama wale." aliendelea kusema "inawezekana mlishawaangamiza wengi kabla ya mimi, kwa kuwaanzalia story hizo lakini mimi sio kama wale; na mwezi huu wa nane ninaendelea mkutano Iringa; waache waandike lakini mimi ni chombo kingine na sio kama wale"

ibada hiyo ilikatishwa na kelele za waumini wake kila muda mfupi alipokuwa akiongea.
baadhi ya Clip za ibada hii unaweza kuzipafa pia youtube!!!

Zaidi ya nchi 53 za ulaya na marekani????? Amewapata wa kuwadanganya,by the way,unaweza kwenda ulaya na marekani still ukawa idiot.it doesn't make ant difderences
 
Hujamuelewa, ana maana kuwa hata huko japani anao akina Flora wengi, probably hana haja ya mjukuu wa mwanamarundi
 
Tofauti na ilivyotarajiwa na wengi kuwa Mch. Gwajima angejibu kashfa iliyosambaa kwa kasi magazetini kumuhusisha yeye na kesi ya Mbasha imeibuka na kudai yeye sio kama wale.

Katika ibada ya jumapili hii iliyoudhuriwa na maelfu ya watu alisikika akisema, "mimi sio kama wale, sijibu hoja kama zile, mfano ukiwa unaoga alafu chizi akachukua nguo zako na ukamkimbiza nano ataonekana chizi?" akaendelea kusema nanukuu " tatizo la watanzania ni kuwa wakisikia kitu kipya kinaanza kwao badala ya kukothamini wanakididimiza lakini mimi sio kama wao" aliendelea kusisitiza.

Mch. Gwajima alisema, "mimi kila mwaka naenda Japan na ninawalecture wajapan ambao pia huja hapa kanisani zaidi ya 40 kila mwaka na mwaka huu watakuja Septemba, lakini watanzania hawashtuki na kuja kujifunza wao wanakalia kuandika stori kwenye magazeti lakini mimi sio kama wao"

Ingawa Mch. Gwajima hakueleza moja kwa moja kuhusu tukio la mbasha na maelezo yoyote lakini maneno haya yanaonyesha kujibu hoja zilizokinyume naye; aliendelea kusema, "Mimi nimehubiri nchi zaidi ya 53 duniani, na nyingi za ulaya na marekani alafu mtu amekaa magomeni miaka yote anatengeneza story ya gazeti unatarajia niijibu, mimi sio kama wale." aliendelea kusema "inawezekana mlishawaangamiza wengi kabla ya mimi, kwa kuwaanzalia story hizo lakini mimi sio kama wale; na mwezi huu wa nane ninaendelea mkutano Iringa; waache waandike lakini mimi ni chombo kingine na sio kama wale"

ibada hiyo ilikatishwa na kelele za waumini wake kila muda mfupi alipokuwa akiongea.
baadhi ya Clip za ibada hii unaweza kuzipafa pia youtube!!!

Du!! Nimependa tu VINA.. '' mimi si kama wale'' asante ndugu mchungaji wa kondoo wa ''bwana''
 
Back
Top Bottom