Mbunge yule Kijana aliyeniomba Ushauri...!

Mbunge yule Kijana aliyeniomba Ushauri...!

maggid potrait himself great thinker!!!!lol. maskini nchi yangu.
 
Duuu Remmy nimekupata sasa. Kumbe huyu jamaa Maggid mwongo.!Kwanini Maggid unatumia muda mrefu kuandika story ya uongo iliyojaa majungu? Na kwa nini Maggid hutaki mabadiliko? Njaa Mbaya sana. Na nimesikia uko kwenye Payrol ya Magamba toka 2007. Kazi kwako

Nimemsoma Maggid ni bendera fuata upepo.
Ni wale wanaoamini mabadiliko baadae baada ya kuona wengine wamefanya, sijui wanaitwa laggards. Atakubali 2015.
 
We unadhani umetusaidia nini kama hauja mtaja? Kwa nini usituweke wazi ili tumjue?

Hii ni ishara ya unafiki na uongo! Alaf ni kawaida yako kuweka habari na kukimbia kwani unajua fika huwezi kujibu ya humu!

Yani unaona bora mtu asinzie bungeni bila kuchangia, kweli we ni mnafiki kwa wananchi!
 
Yaani wadau hata mbunge wenyewe kijana kumjua hamtaki nyinyi mnacheza na mleta mada tu.
Kweli watu wana njaa ya mabadiliko. Wahenga walisema mtoto akililia wembe,...
 
NINA UHAKIKA ENDAPO MAGGID ANGEFANYA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE ULIOPITA LAZIMA ANGEPATA ZERO....... KuMBE MTU AKIWA MBUNGE HARUHUSIWI KUFATILIA GARI LAKE? KUMBE MTU AKIWA MBUNGE HARUHUSIWI KUWAPA NAULI WATU WENGINE.?
 
majid au na wewe unataka ubunge, weka wazi,mi nilijua ukioa mzungu,majungu yanaisha kumbe haijasaidia....
 
NENO LA LEO: MBUNGE YULE KIJANA ALIYENIOMBA USHAURI..!
a1_be7bd.jpg
Ndugu zangu, Kuna simulizi ya kwenye Biblia. Enzi za Mfalme Suleiman kuna watu waliolalamika sana, kuwa wanaishi kwenye manyanyasiko mno. Kukawa na vijana waliokuwa na kiu ya kutaka mabadiliko ya uongozi wa mfalme. Walitaka watawaliwe na mfalme kijana. Wazee walipoombwa ushauri wakatamka; kuwa vijana mara nyingi hupungukiwa na busara. Hivyo, si lazima mfalme awe kijana. Vijana wale wakakaidi ushauri wa wazee. Wakampata Mfalme kijana. Naye alipokuwa madarakani, alitenda mara mbili ya dhambi alizotenda mtawala aliyetangulia. Mfano, kama mtawala aliyepita alitoa adhabu ya kuchapa kwa mjeledi, basi, mfalme kijana yeye alitaka atumie rungu. Hakukuwa na nafuu walioitarajia. Ndugu zangu, Juma la kwanza tu baada ya Bunge kuanza mwaka 2010, nikiwa njiani kutoka Singida nilisimama Dodoma. Hapo nilipata bahati ya kukutana na mmoja wa Wabunge vijana kutoka kambi ya upinzani. Tulikaa na kunywa chai pamoja. Alinitaka pia ushauri katika kazi yake. Hakika,niliingiwa na matumaini makubwa juu ya fikra zake za kimaendeleo pale alipoanza mazungumzo. Mathalan, kati ya dhambi kadhaa zinazofanywa na wabunge alizoziona, akaniambia juu ya kustaajabishwa kwake na tabia ya Wabunge kufoji risiti za safari zao ili wapate fedha zaidi. “ Yaani kaka Maggid, sikujua kuwa Wabunge hawa wanafanya mambo kama watoto wa shule. Yaani Mbunge anahangaika kufoji risiti za mafuta na kudai kuwa ametokea mahali fulani kuja hapa Dodoma wakati sio!” Aliniambia kwa uchungu mbunge yule kijana. Lakini, mashaka yakanijia pale nilipomwuliza; “ Sasa ukitoka hapa Dodoma umejiandaa na kipi cha kwenda kuwaambia wapiga kura wako kwenye mkutano wako wa kwanza wa hadhara baada ya kikao chako cha kwanza Bungeni?” Mbunge yule kijana aliniangalia na kuniambia; “ Naenda kwanza Dar kuhangaikia gari yangu mpya!” Nikawa nimekatishwa tamaa na Mbunge yule kijana. Kwamba katika juma la kwanza tu la kukaa Bungeni, tayari ameanza kufikiria kuhangaikia masuala yake binafsi, na si masuala ya wananchi waliompigia kura! Naambiwa, naye siku hizi anapomaliza vikao vya kuongea hata na jamaa zake tu, haraka sana hukimbilia kutoa ‘ bahasha za nauli’. Siku hizi mbunge yule kijana ana gari zaidi ya ile aliyokwenda kuichukua Dar. Amekuwa mbunge-mfanyabiashara. Sifikirii tena kwenda kumpa ushauri mbunge yule kijana, maana, naweza kuambulia kudhalilishwa kwa kupewa ‘bahasha ya nauli’ ya kurudia nyumbani kwangu. Naam, ni heri ya ndugu yangu John Komba, hata akisemwa kuwa anasinzia Bungeni, bado ana mchango kwa jamii; kwa nyimbo zake zenye kuburudisha na kuelimisha. Ndio, nchi hii inahitaji mabadiliko ya kimsingi, lakini, ni vizuri kutambua, kuwa wengine tunaofikiri kuwa wanaweza kutusaidia katika kuyafikia mabadiliko hayo, hawana tofauti kabisa na baadhi ya tunaofikiria hawatufai. Na hutokea, kuwa dhambi wafanyayo, na watakayoifanya, yumkini yaweza kuwa ni mara mbili ya inayofanywa na baadhi ya waliopo sasa. Ni Neno La Leo. Maggid Mjengwa, Iringa. 0788 111 765
maggid=@Chilisosi???????
 
Last edited by a moderator:
mimi ni mmoja kati ya wasomaji wa makala zako kaka Mjengwa. Umejitahidi siku zote kujenga hoja zenye mtazamo mpana katika maswala ya kisiasa na kijamii. katika hiki kipande chako cha makala/maoni juu ya mbunge kijana wa "kambi ya upinzani" inanipa wakati mgumu kujua "political inclination" yako na hivyo kushuku umakini na weledi wako katika kujenga hoja zenye mwelekeo wa kimapinduzi. Nashukuru kuwa umekuwa fair kwa kueleza kuwa mbunge huyo alikuwa na kero ya kuona wabunge (watu wazima walioaminiwa na wananchi ya kuwa wanafaa kuwawakilisha bungeni) kufanya kitendo cha kitoto (kukosa hekima kadri ya tafsiri yako ya hekima kuhusishwa na uzee) na kifisadi cha kufoji risiti ili wapate malipo yasiyo halali. "Asiyekuwa mwaminifu katika mambo madogo, vivyo hivyo hawezi kuwa mwaminifu katika mambo makubwa". Kimsingi, kwako hilo hukuona kama ni tatizo linalohitaji kushughulikiwa ikiwa tu ushahidi ungejitoshereza, bali uliona ni vema uulize atasema nini mara tu arudipo jimboni. Mkuki kwa nguruwe, kwa binadamu mchungu. Kumtaka mbunge awe na chochote cha kusema kwa wananchi wake as far as his political obligations are concerned ni kumhukumu mapema sana ukilinganisha na serikali inayoshindwa kutekeleza ahadi zake kwa muda wa miaka 5 na kusema kuwa muda haukutosha na hivyo wapewe miaka mingine 5 ili watekeleze ahadi(sipendi kusema ni serikali ya chama gani). Comparative analysis yako kati ya "mbunge kijana" na Komba inaonesha wazi kuwa uko biased dhidi ya wabunge vijana na hususan wa upinzani, na hivyo unanirahisishia kufahamu itikadi yako kisiasa. Sasa anayeenda kushughulikia gari ili apate usafiri wa kufanyia kazi zake jimboni na yule anayesinzia bungeni, nani wa kusifiwa na kushabikiwa?? je ni Komba eti kwa kuwa anaimba nyimbo za "Chama Cha Mapinduzi" zisizokuwa na faida yoyote kwa watanzania zaidi ya propaganda za chama (ambacho sio cha wananchi wote)? au ni yule anayechukia kufoji risiti za usafiri?. Je, ni mbunge gani ana haki ya kuwa mfanyabiashara na yupi hana haki, au unahusishaje biashara za mbunge kijana na ubunge wake?. Kaka Mjengwa katika hii umeshinwa kujenga hoja zaidi ya kuongozwa na itikadi na chuki kuliko uhalisia, umakini na pia weledi katika kujenga hoja hususan pale unapodismiss hoja na mawazo ya mbunge kijana na kuona ni bora ya komba anayeimba nyimbo za chama. Mjengwa, karibu tujadiri!
 
Majid umelishwa nini au umeahidiwa ukuu wa wilaya? Mmmmh! Ni hatari kama hata tunawowaona wasomi nao ni magamba full. Eeehe nchi hii?!
 
Huhitaji kuwa GREAT THINKER kujua Mbunge alotajwa hapo na Majid ni mmoja tu na ni wa chama twawala* anamaanisha wengi wa Wabunge wa chama twawala hupelekwa kwa mambo binafsi akataja kama kulala na kuimba tu, naongezea uganga, fitna za ndani ya chama, wanamtandao, viburudisho nyumba ndogo),nk hivi ndivyo mjengwa anavyotukana chama twawala na wabunge wake kisanii hataki kuwambia ukweli kuwa zama za kupeana ubunge kiu kada zimepitwa na wakati tuanze kuangalia vijana wanaofanya kazi zao kiutu na kwaajili ya wapiga kura wao huku wakitimiza stahiki zao binafsi kwa haki. hongera majid kwa kutukana chama kisanii.
 
Back
Top Bottom