Mbunge yule Kijana aliyeniomba Ushauri...!

Mbunge yule Kijana aliyeniomba Ushauri...!

Naam, ni heri ya ndugu yangu John Komba, hata akisemwa kuwa anasinzia Bungeni, bado ana mchango kwa jamii; kwa nyimbo zake zenye kuburudisha na kuelimisha.


Ni Neno La Leo.
Maggid Mjengwa,
Iringa.
yani hapo sijui ulitaka kuandika nini. Are you serious?huwez kuwa mjinga kiasi hicho.
 
Kweli mtoa mada uwezo wako wa kufikiri uko chini sana! yaani baada ya kuambiwa 'anakwenda dar kushughulikia gari lake jipya' tayari umeshakatishwa tamaa! hukusumbua ubongo wako kwenda mbele zaidi baada ya kupata gari jipya litamsaidiaje kutekeleza ulichomuuliza? Kweli kuna wachambuzi vihiyo sana nchi hii na wewe ni mmojawapo!Hata matumizi ya gari huwezi hoji yatakuwa yapi!
 
Nimeamini maneno yanayosemwa waandisha wa habari na watangazaji wengi niwale waliofeli form 4 mmojawapo niwewe.inaoneka makala zako nyingi za kupewa unapojaribu kutumia akili yako ndio unaandika upuuzi kama huu.
 
Nimeamini maneno yanayosemwa waandisha wa habari na watangazaji wengi niwale waliofeli form 4 mmojawapo niwewe.inaoneka makala zako nyingi za kupewa unapojaribu kutumia akili yako ndio unaandika upuuzi kama huu.
 
Kuna dhambi gani mbunge kijana kushugulikia gari lake?, acha majungu ndugu yangu, mbunge bila kuwa na gari atawezaje kutumikia na kuwafikia wananchi wake?????
Ndugu zangu,

Kuna simulizi ya kwenye Biblia. Enzi za Mfalme Suleiman kuna watu waliolalamika sana, kuwa wanaishi kwenye manyanyasiko mno.

Kukawa na vijana waliokuwa na kiu ya kutaka mabadiliko ya uongozi wa mfalme. Walitaka watawaliwe na mfalme kijana.

Wazee walipoombwa ushauri wakatamka; kuwa vijana mara nyingi hupungukiwa na busara. Hivyo, si lazima mfalme awe kijana.

Vijana wale wakakaidi ushauri wa wazee. Wakampata Mfalme kijana. Naye alipokuwa madarakani, alitenda mara mbili ya dhambi alizotenda mtawala aliyetangulia.

Mfano, kama mtawala aliyepita alitoa adhabu ya kuchapa kwa mjeledi, basi, mfalme kijana yeye alitaka atumie rungu. Hakukuwa na nafuu walioitarajia.

Ndugu zangu,

Juma la kwanza tu baada ya Bunge kuanza mwaka 2010, nikiwa njiani kutoka Singida nilisimama Dodoma. Hapo nilipata bahati ya kukutana na mmoja wa Wabunge vijana kutoka kambi ya upinzani.

Tulikaa na kunywa chai pamoja. Alinitaka pia ushauri katika kazi yake. Hakika, niliingiwa na matumaini makubwa juu ya fikra zake za kimaendeleo pale alipoanza mazungumzo. Mathalan, kati ya dhambi kadhaa zinazofanywa na wabunge alizoziona, akaniambia juu ya kustaajabishwa kwake na tabia ya Wabunge kufoji risiti za safari zao ili wapate fedha zaidi.

“Yaani kaka Maggid, sikujua kuwa Wabunge hawa wanafanya mambo kama watoto wa shule. Yaani Mbunge anahangaika kufoji risiti za mafuta na kudai kuwa ametokea mahali fulani kuja hapa Dodoma wakati sio!” Aliniambia kwa uchungu mbunge yule kijana.

Lakini, mashaka yakanijia pale nilipomwuliza;

“Sasa ukitoka hapa Dodoma umejiandaa na kipi cha kwenda kuwaambia wapiga kura wako kwenye mkutano wako wa kwanza wa hadhara baada ya kikao chako cha kwanza Bungeni?”

Mbunge yule kijana aliniangalia na kuniambia; “ Naenda kwanza Dar kuhangaikia gari yangu mpya!”

Nikawa nimekatishwa tamaa na Mbunge yule kijana. Kwamba katika juma la kwanza tu la kukaa Bungeni, tayari ameanza kufikiria kuhangaikia masuala yake binafsi, na si masuala ya wananchi waliompigia kura!

Naambiwa, naye siku hizi anapomaliza vikao vya kuongea hata na jamaa zake tu, haraka sana hukimbilia kutoa ‘ bahasha za nauli’.

Siku hizi mbunge yule kijana ana gari zaidi ya ile aliyokwenda kuichukua Dar. Amekuwa mbunge-mfanyabiashara.

Sifikirii tena kwenda kumpa ushauri mbunge yule kijana, maana, naweza kuambulia kudhalilishwa kwa kupewa ‘bahasha ya nauli’ ya kurudia nyumbani kwangu.

Naam, ni heri ya ndugu yangu John Komba, hata akisemwa kuwa anasinzia Bungeni, bado ana mchango kwa jamii; kwa nyimbo zake zenye kuburudisha na kuelimisha.

Ndio, nchi hii inahitaji mabadiliko ya kimsingi, lakini, ni vizuri kutambua, kuwa wengine tunaofikiri kuwa wanaweza kutusaidia katika kuyafikia mabadiliko hayo, hawana tofauti kabisa na baadhi ya tunaofikiria hawatufai.

Na hutokea, kuwa dhambi wafanyayo, na watakayoifanya, yumkini yaweza kuwa ni mara mbili ya inayofanywa na baadhi ya waliopo sasa.

Ni Neno La Leo.
Maggid Mjengwa,
Iringa.
 
...we Majjid.....hakuna palipoandikwa kuwa mtu akishakuwa mwanasiasa...hata kama ana mapenzi na watu wake.. haijasemwa awe maskini!!....ndio sababu wabung wanalipwa mishahara kwa kazi zao....hii nayo ni ajira...na kwa maana hiyo wana haki kabisa kujinunulia watakacho....kiwe magari au chochote(kama uwezo wanao)..na hata biashara wanaruhusiwa kufanya (kama tu ni halali...na hamna rushwa)...Cha msingi..je wabunge wanatumia muda wao ipasavyo kuwatumikia watu wao???...hayo ya kununua magari ni njaa zako tu...inaonyesha we mjima sana...Na ndio sababu sikusomi....unaganga njaa sana we mwandishi......Sijui unapataje safu Raia Mwema!!
 
Kwa hiyo katika madhira/mauzi yote ya wabunge, lililokuudhi ni hilo tu? ?

Hujayaona mengine ya magamba wenzio!??

kwani nae gamba? maana atakua mjinga katoka koooote ujerumani kuwa gamba hapa tanzania halafu kuna siku alisema mfutakamba alikua best yake toka wanakula sijui ugali kwa mama nani yule alimtaja inawezekan nae ana akili kama ya best yake maana si unajua kunguru wafananao huruka pamoja ha ha ha haya bana majid karb
 
Back
Top Bottom