Mbunge yule Kijana aliyeniomba Ushauri...!

Mi ninadhani alianza kulishughulikia gari lake ili awafikie hata wale waliokuwa machimbo huko...awape elimu ya uraia!! Safi sana Mbunge kijana
 
Ni Kitabu kipi na Sura ya ngapi katika Biblia simulizi hii ipo?

Asante kwa kuniulizia swali. Asipojibu hilo, atakuwa amefuta hata habari yake inayotutaka tuendelee kutawaliwa na chama chake tulichokichoka!
 
Ni shetani tu anadhani kati ya Msigwa na Komba, Komba ni wa maana! Hata Lulu pamoja na kugawa shonza yake hawezi kusema wala kuwaza hivi.
 
Mara nyingi ninapo soma makala zako Majjid hua naamua kuwa makini kweli na unachotaka kusema, kiukweli hua ninakuona kama ni mtu unayejaribu kuficha chuki fulani kwa watu fulani, heshima yako kwakua ni kubwa kwa wasomaji wako then unatumia akili ya ziada kuzunguka mbuyu, well saidi mwanachama wa siri wa magamba!
 
Unajua ni vigumu kumjua mtu akili zake mpaka umukaribie na kumsikia wewe mwenyewe, MAJJID you are so cheap, mpaka Komba wewe unamuona ana nafuu, sasa nani MCHAFU kama hata KOMBA eti ana nafuu... UKWELIm ni kwamba huyu ALINYIMWA HELA YA MAFUTA NA HUYO MBUNGE KIJANA... Sasa analeta hasira zake hapa....
 
Ni shetani tu anadhani kati ya Msigwa na Komba, Komba ni wa maana! Hata Lulu pamoja na kugawa shonza yake hawezi kusema wala kuwaza hivi.

chilisosi anafikiri kumtumia mjengwa kuna weza kumpa nafasi ya kugombea ubunge muulize mwakalebela
 
huwa nakukubali sana majidi lakini kwa hili ...nashawishika kusema huna jipya na komba wako..tayali umehongwa na ccm..
 
Sasa msigwa anahusika na nini hapa , kwanza msigwa hayuko katika kundi la vijana, huyu jamaa anaitwa chilisosi,naona ana akili ya kuku , anadhani kwa kukaa uingereza watanzania ni wajinga kama akili yake , anashindwa kuunganisha mambo ,hiyo hadithi haina uhusiano wote na jembe msigwa,

Mkuu ni vyema akatujuza anafanya nini UK, usijekuta ni coca cola.
 
Yani mkuu unataka kusema zimwi likujualo halikuli likakwisha????? Tunajitaji watu wengine upinzani nso wzchukue nchi. Tumechoka na ufisadi na unyanyasaji wa ccm. mabadiliko yamechelewa sans ccm wakae pembeni hata rais kasema amechoka.
 
Hivi huyu Chilisosi anamatatizo??? Ya Iringa na Uk yamempataje? njaa yake kali. Mjengwa nilikuwa napenda kupitia blog yake ila hili limenikinahi nimemfahamu yuko wapi.
 
ndugu zangu,

kuna simulizi ya kwenye biblia. Enzi za mfalme suleiman kuna watu waliolalamika sana, kuwa wanaishi kwenye manyanyasiko mno.

Kukawa na vijana waliokuwa na kiu ya kutaka mabadiliko ya uongozi wa mfalme. Walitaka watawaliwe na mfalme kijana.

Wazee walipoombwa ushauri wakatamka; kuwa vijana mara nyingi hupungukiwa na busara. Hivyo, si lazima mfalme awe kijana.

Vijana wale wakakaidi ushauri wa wazee. Wakampata mfalme kijana. Naye alipokuwa madarakani, alitenda mara mbili ya dhambi alizotenda mtawala aliyetangulia.

Mfano, kama mtawala aliyepita alitoa adhabu ya kuchapa kwa mjeledi, basi, mfalme kijana yeye alitaka atumie rungu. Hakukuwa na nafuu walioitarajia.

Ndugu zangu,

juma la kwanza tu baada ya bunge kuanza mwaka 2010, nikiwa njiani kutoka singida nilisimama dodoma. Hapo nilipata bahati ya kukutana na mmoja wa wabunge vijana kutoka kambi ya upinzani.

Tulikaa na kunywa chai pamoja. Alinitaka pia ushauri katika kazi yake. Hakika, niliingiwa na matumaini makubwa juu ya fikra zake za kimaendeleo pale alipoanza mazungumzo. Mathalan, kati ya dhambi kadhaa zinazofanywa na wabunge alizoziona, akaniambia juu ya kustaajabishwa kwake na tabia ya wabunge kufoji risiti za safari zao ili wapate fedha zaidi.

“yaani kaka maggid, sikujua kuwa wabunge hawa wanafanya mambo kama watoto wa shule. Yaani mbunge anahangaika kufoji risiti za mafuta na kudai kuwa ametokea mahali fulani kuja hapa dodoma wakati sio!” aliniambia kwa uchungu mbunge yule kijana.

Lakini, mashaka yakanijia pale nilipomwuliza;

“sasa ukitoka hapa dodoma umejiandaa na kipi cha kwenda kuwaambia wapiga kura wako kwenye mkutano wako wa kwanza wa hadhara baada ya kikao chako cha kwanza bungeni?”

mbunge yule kijana aliniangalia na kuniambia; “ naenda kwanza dar kuhangaikia gari yangu mpya!”

nikawa nimekatishwa tamaa na mbunge yule kijana. Kwamba katika juma la kwanza tu la kukaa bungeni, tayari ameanza kufikiria kuhangaikia masuala yake binafsi, na si masuala ya wananchi waliompigia kura!

Naambiwa, naye siku hizi anapomaliza vikao vya kuongea hata na jamaa zake tu, haraka sana hukimbilia kutoa ‘ bahasha za nauli’.

Siku hizi mbunge yule kijana ana gari zaidi ya ile aliyokwenda kuichukua dar. Amekuwa mbunge-mfanyabiashara.

Sifikirii tena kwenda kumpa ushauri mbunge yule kijana, maana, naweza kuambulia kudhalilishwa kwa kupewa ‘bahasha ya nauli’ ya kurudia nyumbani kwangu.

Naam, ni heri ya ndugu yangu john komba, hata akisemwa kuwa anasinzia bungeni, bado ana mchango kwa jamii; kwa nyimbo zake zenye kuburudisha na kuelimisha.

Ndio, nchi hii inahitaji mabadiliko ya kimsingi, lakini, ni vizuri kutambua, kuwa wengine tunaofikiri kuwa wanaweza kutusaidia katika kuyafikia mabadiliko hayo, hawana tofauti kabisa na baadhi ya tunaofikiria hawatufai.

Na hutokea, kuwa dhambi wafanyayo, na watakayoifanya, yumkini yaweza kuwa ni mara mbili ya inayofanywa na baadhi ya waliopo sasa.

Ni neno la leo.
Maggid mjengwa,
iringa.

akili tope............
 
Back
Top Bottom