Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,899
Mbunge wa Tarime Vijijni John Heche anasakwa na Jeshi la Polisi. Heche anasakwa na jeshi hilo huku kukiwa na taarifa kwamba jeshi hilo linataka kumhoji kufuatia kauli aliyoitoa bungeni mjini Dodoma wiki iliyopita ya kuwahamasisha wananchi wa jimbo lake kulinda rasilimali zao.
Mbunge huyo wa CHADEMA, aliliambia bunge kwamba atawaongoza wananchi wa jimbo lake kuzuia Madini na rasilimali nyingine kusafirishwa nje ya nchi na Mgodi wa North Mara. Heche alikuwa anachangia hotuba ya bajeti ambapo katika mchango wake aligusia pia suala la Taarifa ya pili ya Mchanga wa dhahabu iliyoundwa na rais Dk John Pombe Magufuli.
Siku chcahe zilizopita zaidi ya wananchi 300 wanaoishi vijiji vinavyozunguka mgodi huo walivamia mgodini hapo na kufanya vurugu zilizodhibitiwa na Polisi.