Mbunge wa Tarime Vijijni, John Heche anasakwa na Jeshi la Polisi

What a silly question from probably the most idiot person! Samahani, hivi una familia inayokutegemea? Mbona itakuwa na Hasara?

Mitandaoni buana....wengine wanajipa vyeo ambavyo hawana...wanajipa kikubwa ambao haupo....wanajitutumua kwa watu wasiowajua. Pole sana
 
Immunity ya mbunge kwa anachoongea bungeni naona inawalinda wabunge wa CCM tu..

Mbunge wa Geita Msukuma na Kibajaji wa Mtera huwa wanaongea vitu vya ovyo na hatari kuliko alivyosema Heche lakini sijawahi kusikia wakati wowote wakitafutwa na jeshi la kupiga walemavu..

Endeleeni tu kutumika..
Yote yana mwisho haya.

NDIO hata mimi nnapochoka hapo,,wabunge wa ccm wanaongeaga ovyo lakini hawatafutwi,,,mfano kuna mbunge sikumbuki anaitwa Nani wa ccm,alisema atawaongoza wapiga Kura wake wakapasue bomba kuu la maji sababu wao wanacheleweshewa huduma
 
Kama hii habari ya Mheshimiwa Heche kutafutwa na polisi kwa kauli ama hoja aliyotoa ndani ya bunge ni kweli basi huo ni dharau/ukiukwaji/uvunjaji wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayotoa madaraka na haki kwa mbunge katika kujadili na kutoa mawazo yake akiwa ndani ya bunge kama inavyoelezwa kwenye Ibara ya 100 (1) na 100 (2) ya Katiba hiyo kuwa;

100 - (1) Kutakuwa na uhuru wa mawazo, majadiliano na utaratibu katika Bunge na uhuru huo hautavunjwa wala kuhojiwa na chombo chochote katika Jamhuri ya Muungano, au katika Mahakama au mahali penginepo nje ya Bunge.

(2) Bila ya kuathiri Katiba hii au masharti ya sheria nyingine yoyote inayohusika, Mbunge yeyote hatashtakiwa au kufunguliwa
shauri la madai mahakamani kutokana na jambo lolote alilolisema
au kulifanya ndani ya Bunge au alilolileta Bungeni kwa njia ya maombi, muswada, hoja au vinginevyo.

Hii ni kwa wabunge wa Ccm tu mkuu,,,
 
Hawo poliCCM watatumika sana kama KONDOMU na mwisho wa siku watatupwa jalalani.
 
Tuwe Na tahadhari na hawa wanasiasa ambao wanaweza kutuletea matatizo kama ya Zimbabwe ya kuvamia mashamba ya wazungu. Ni Muhimu mtu mzima kama mbunge kuheshimu utawala wa sheria.
Aliyekuwa wa kwanza kuwaita wenye migodi ya dhahabu kwamba ni wezi ni nani? Tena kwenye shrehe kuu ya kitaifa with full media coverage!!!!!!!!! Usisahahu na yeye kumshauri kwanza mkuu!!!!!!!!
 
Mbunge wa Tarime Vijijni John Heche anasakwa na Jeshi la Polisi. Heche anasakwa na jeshi hilo huku kukiwa na taarifa kwamba jeshi hilo linataka kumhoji kufuatia kauli aliyoitoa bungeni mjini Dodoma wiki iliyopita ya kuwahamasisha wananchi wa jimbo lake kulinda rasilimali zao.

Mbunge huyo wa CHADEMA, aliliambia bunge kwamba atawaongoza wananchi wa jimbo lake kuzuia Madini na rasilimali nyingine kusafirishwa nje ya nchi na Mgodi wa North Mara. Heche alikuwa anachangia hotuba ya bajeti ambapo katika mchango wake aligusia pia suala la Taarifa ya pili ya Mchanga wa dhahabu iliyoundwa na rais Dk John Pombe Magufuli.

Siku chcahe zilizopita zaidi ya wananchi 300 wanaoishi vijiji vinavyozunguka mgodi huo walivamia mgodini hapo na kufanya vurugu zilizodhibitiwa na Polisi.
chadema bana!waoga sana.Bungeni tu kuna mapolisi wengi akitoka tu nje ya geti wangemnyaka.
hebu weka tangazo la polisi
 
Mbunge wa Tarime Vijijni John Heche anasakwa na Jeshi la Polisi. Heche anasakwa na jeshi hilo huku kukiwa na taarifa kwamba jeshi hilo linataka kumhoji kufuatia kauli aliyoitoa bungeni mjini Dodoma wiki iliyopita ya kuwahamasisha wananchi wa jimbo lake kulinda rasilimali zao.

Mbunge huyo wa CHADEMA, aliliambia bunge kwamba atawaongoza wananchi wa jimbo lake kuzuia Madini na rasilimali nyingine kusafirishwa nje ya nchi na Mgodi wa North Mara. Heche alikuwa anachangia hotuba ya bajeti ambapo katika mchango wake aligusia pia suala la Taarifa ya pili ya Mchanga wa dhahabu iliyoundwa na rais Dk John Pombe Magufuli.

Siku chcahe zilizopita zaidi ya wananchi 300 wanaoishi vijiji vinavyozunguka mgodi huo walivamia mgodini hapo na kufanya vurugu zilizodhibitiwa na Polisi.
"Endelea kuwabana huko ndani, wafukuze wakija huku mtaani nitadeal nao" Hii sio kauli yangu bali ya baba mwenye house
 
Back
Top Bottom