Mbunge wa Tarime Vijijni, John Heche anasakwa na Jeshi la Polisi

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,259
2,000
Mbunge wa Tarime Vijijni John Heche anasakwa na Jeshi la Polisi. Heche anasakwa na jeshi hilo huku kukiwa na taarifa kwamba jeshi hilo linataka kumhoji kufuatia kauli aliyoitoa bungeni mjini Dodoma wiki iliyopita ya kuwahamasisha wananchi wa jimbo lake kulinda rasilimali zao.

Mbunge huyo wa CHADEMA, aliliambia bunge kwamba atawaongoza wananchi wa jimbo lake kuzuia Madini na rasilimali nyingine kusafirishwa nje ya nchi na Mgodi wa North Mara. Heche alikuwa anachangia hotuba ya bajeti ambapo katika mchango wake aligusia pia suala la Taarifa ya pili ya Mchanga wa dhahabu iliyoundwa na rais Dk John Pombe Magufuli.

Siku chcahe zilizopita zaidi ya wananchi 300 wanaoishi vijiji vinavyozunguka mgodi huo walivamia mgodini hapo na kufanya vurugu zilizodhibitiwa na Polisi.
 

Bowie

JF-Expert Member
Sep 17, 2016
4,082
2,000
Mbunge wa Tarime Vijijni John Heche anasakwa na Jeshi la Polisi.Heche anasakwa na jeshi hilo huku kukiwa na taarifa kwamba jeshi hilo linataka kumhoji kufuatia kauli aliyoitoa bungeni mjini Dodoma wiki iliyopita ya kuwahamasisha wananchi wa jimbo lake kulinda rasilimali zao.Mbunge huyo wa CHADEMA, aliliambia bunge kwamba atawaongoza wananchi wa jimbo lake kuzuia Madini na rasilimali nyingine kusafirishwa nje ya nchi na Mgodi wa North Mara.Heche alikuwa anachangia hotuba ya bajeti ambapo katika mchango wake aligusia pia suala la Taarifa ya pili ya Mchanga wa dahabu iliyoundwa na rais Dk John Pombe Magufuli.Siku chcahe zilizopita zaidi ya wananchi 300 wanaoishi vijiji vinavyozunguka mgodi huo walivamia mgodini hapo na kufanya vurugu zilizodhibitiwa na Polisi.
Tuwe Na tahadhari na hawa wanasiasa ambao wanaweza kutuletea matatizo kama ya Zimbabwe ya kuvamia mashamba ya wazungu. Ni Muhimu mtu mzima kama mbunge kuheshimu utawala wa sheria.
 

MENGELENI KWETU

JF-Expert Member
Oct 23, 2013
9,167
2,000
Immunity ya mbunge kwa anachoongea bungeni naona inawalinda wabunge wa CCM tu..

Mbunge wa Geita Msukuma na Kibajaji wa Mtera huwa wanaongea vitu vya ovyo na hatari kuliko alivyosema Heche lakini sijawahi kusikia wakati wowote wakitafutwa na jeshi la kupiga walemavu..

Endeleeni tu kutumika..
Yote yana mwisho haya.
 

lukindo

JF-Expert Member
Mar 20, 2010
8,474
2,000
Si aliyasema bungeni, kama ilikuwa makosa ni kwa nini kiti hakikumchukulia hatua!
Na je, si alikuwa anatii maelekezo halali ya rais 'aliyetufumbua' macho kuwa kampuni iliyopo jimboni mwake haijasajiliwa na inaliibia taifa!?
Tusipoangalia huenda tukaja kufananishwa na photocopies za binadamu badala ya binadamu halisi.
 

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
21,191
2,000
Wabunge kusakwa na wahusika vinaanza kuwa vitu vya kawaida ati..!
 

Idimi

JF-Expert Member
Mar 18, 2007
13,891
2,000
Immunity ya mbunge kwa anachoongea bungeni naona inawalinda wabunge wa CCM tu..

Mbunge wa Geita Msukuma na Kibajaji wa Mtera huwa wanaongea vitu vya ovyo na hatari kuliko alivyosema Heche lakini sijawahi kusikia wakati wowote wakitafutwa na jeshi la kupiga walemavu..

Endeleeni tu kutumika..
Yote yana mwisho haya.
I wonder
Sheria hairuhusu kumpatiliza mbunge kwa anachoongea bungeni. Lakini sishangai, polisi wetu weledi ni 0% kabisa.
 

jogi

JF-Expert Member
Sep 25, 2010
25,600
2,000
Tontoni aliwapigaje chenga pale eapoti?

Ghafla wanawapondaponda walemavu kwa marungu kama wawapondavyo wanyang'anyi.

Polishhhhhhiiiiii!!!
 

The Elephant

JF-Expert Member
Dec 18, 2014
4,313
2,000
Immunity ya mbunge kwa anachoongea bungeni naona inawalinda wabunge wa CCM tu..

Mbunge wa Geita Msukuma na Kibajaji wa Mtera huwa wanaongea vitu vya ovyo na hatari kuliko alivyosema Heche lakini sijawahi kusikia wakati wowote wakitafutwa na jeshi la kupiga walemavu..

Endeleeni tu kutumika..
Yote yana mwisho haya.
Na mwisho umekaribia
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom