Mbunge wa Tarime Vijijni, John Heche anasakwa na Jeshi la Polisi

I wonder
Sheria hairuhusu kumpatiliza mbunge kwa anachoongea bungeni. Lakini sishangai, polisi wetu weledi ni 0% kabisa.
Acheni ujinga wenu. Mtu ahamasishe vurugu msingizie kinga ya kibunge?
 
Tuwe Na tahadhari na hawa wanasiasa ambao wanaweza kutuletea matatizo kama ya Zimbabwe ya kuvamia mashamba ya wazungu. Ni Muhimu mtu mzima kama mbunge kuheshimu utawala wa sheria.
1. Rais na serikali nzima imetwambia kuwa Acacia ni majizi
2. Serikali imetuambia hakuna utaratibu unaotakiwa kufuatwa katika kukamata mwizi wako
3. Kauli ya Heche naamini aliitoa bungeni kama hatua ya kumuunga mkono Rais kwa jitihada zake za kutetea raslimali za wanyonge.

Polisi wanamtafuta kumpongeza au wanataka kumweka ndani?
 
Acheni ujinga wenu. Mtu ahamasishe vurugu msingizie kinga ya kibunge?
Amehamasisha vipi vurugu?
Yeye ameakisi maneno ya Rais, kwamba Acacia ni wezi, hawapo kisheria na migodi ile ni mali ya wananchi. Pia wananchi wamemsikia Rais na pia wamesikiliza ripoti za kamati mbili za rais zilizosema hivyo. na wameambiwa vile vile kuwa hakunaga utaratibu unapotaka kukamata mwizi wako.
Wao kwa kuwa si watu wa maneno-maneno, wameamua kutekeleza azimio kwa vitendo.
 
Polisi wamkamate huyo Heche haraka iwezekanavyo. Wasicheke na nyani. Hatutaki kuvuna mabua.

tumia akili kufikiri acha kutumia sehemu zingine uyu ameongea bungeni hawezi kufanywa chochote ila kwakuwa wenye nchi wana akili kama zako inawezekana
 
Asikamatwe hechetu hata kiongozi wa shighuli za bunge siku kauli hiyo inatolewa asakwe akamatwe na ahojiwe kwasababu hakumuambia afute kauli hivyo aliridhia
 
Tuwe Na tahadhari na hawa wanasiasa ambao wanaweza kutuletea matatizo kama ya Zimbabwe ya kuvamia mashamba ya wazungu. Ni Muhimu mtu mzima kama mbunge kuheshimu utawala wa sheria.

Utawala wa sheria uko wapi.......kama kuna utawala wa sheria yasingelitokea yanayotokea,mnapalilia siasa za chuki sasa mnalia na utawala wa sheria...,bado wananchi hawajachoka,wakichoka subirini makubwa ....
 
Hiyo mitambo iling'olewa?
Kinachoongelewa ni kauli zao. Kwani Heche alikwenda Mara kuwahamasisha hao wananchi? Si yuko Dodoma kwenye vikao vya bunge? Tofauti hapo ni aina ya watu, wasukuma wa huko Koromije na hao "wana-Mara" nadhani wanatofautiana ushupavu/ujasiri/uoga
 
Mbunge wa Tarime Vijijni John Heche anasakwa na Jeshi la Polisi. Heche anasakwa na jeshi hilo huku kukiwa na taarifa kwamba jeshi hilo linataka kumhoji kufuatia kauli aliyoitoa bungeni mjini Dodoma wiki iliyopita ya kuwahamasisha wananchi wa jimbo lake kulinda rasilimali zao.

Mbunge huyo wa CHADEMA, aliliambia bunge kwamba atawaongoza wananchi wa jimbo lake kuzuia Madini na rasilimali nyingine kusafirishwa nje ya nchi na Mgodi wa North Mara. Heche alikuwa anachangia hotuba ya bajeti ambapo katika mchango wake aligusia pia suala la Taarifa ya pili ya Mchanga wa dhahabu iliyoundwa na rais Dk John Pombe Magufuli.

Siku chcahe zilizopita zaidi ya wananchi 300 wanaoishi vijiji vinavyozunguka mgodi huo walivamia mgodini hapo na kufanya vurugu zilizodhibitiwa na Polisi.
Katiba ya JMT inampa mbunge kinga ya kutokamatwa na mamlaka yoyote nje ya bunge kwa kitu alichoongea au kutamka akiwa ndani ya Bunge

100.-(1) Kutakuwa na uhuru wa mawazo, majadiliano na utaratibu katika Bunge na uhuru huo hautavunjwa wala kuhojiwa na chombo chochote katika Jamhuri ya Muungano, au katika Mahakama au mahali penginepo nje ya Bunge.

(2) Bila ya kuahiri Katiba hii au masharti ya sheria nyingine yoyote inayohusika, Mbunge yeyote hatashtakiwa au kufunguliwa shauri la madai mahakamani kutokana na jambo lolote alilolisema au kulifanya ndani ya Bunge au alilolileta Bungeni kwa njia ya maombi, muswada, hoja au vinginevyo.
 
Tuwe Na tahadhari na hawa wanasiasa ambao wanaweza kutuletea matatizo kama ya Zimbabwe ya kuvamia mashamba ya wazungu. Ni Muhimu mtu mzima kama mbunge kuheshimu utawala wa sheria.

Wewe hivi ulielewa alichokisema JPM? nani alichochea swala hili? kama Rais wa nchi kasema Acacia ni wezi na hawajasajiliwa kuna kosa kulinda mali za nchi?
 
Mbunge wa Tarime Vijijni John Heche anasakwa na Jeshi la Polisi. Heche anasakwa na jeshi hilo huku kukiwa na taarifa kwamba jeshi hilo linataka kumhoji kufuatia kauli aliyoitoa bungeni mjini Dodoma wiki iliyopita ya kuwahamasisha wananchi wa jimbo lake kulinda rasilimali zao.

Mbunge huyo wa CHADEMA, aliliambia bunge kwamba atawaongoza wananchi wa jimbo lake kuzuia Madini na rasilimali nyingine kusafirishwa nje ya nchi na Mgodi wa North Mara. Heche alikuwa anachangia hotuba ya bajeti ambapo katika mchango wake aligusia pia suala la Taarifa ya pili ya Mchanga wa dhahabu iliyoundwa na rais Dk John Pombe Magufuli.

Siku chcahe zilizopita zaidi ya wananchi 300 wanaoishi vijiji vinavyozunguka mgodi huo walivamia mgodini hapo na kufanya vurugu zilizodhibitiwa na Polisi.
I do support Heche in his political ambitions and deeds, BUT, I must say I do not condone a state of lawlessness! Tungelitafuta namna ya kuwaondo "wezi". Hata kama Rais alitamka, rais ni mtu kama wewe na mimi na si ajabu unamzidi maarifa/kufikiri etc; huwezi kuwaamrisha watu wafanye fujo (lawlessness) kwa vile rais aliwaita "wezi"! Tunazuia mob justice, Heche you are advocating Mob justice! NO!
 
Tuwe Na tahadhari na hawa wanasiasa ambao wanaweza kutuletea matatizo kama ya Zimbabwe ya kuvamia mashamba ya wazungu. Ni Muhimu mtu mzima kama mbunge kuheshimu utawala wa sheria.
Raia wameaminishwa hawa watu ni wezi! What more do you expect
 
Acheni ujinga wenu. Mtu ahamasishe vurugu msingizie kinga ya kibunge?
Nadhani wajinga msioelewa mleta mada anaongelea nini! Kwa nini kuwe na double standards? Mhe. Hamis Kigwangwalla alifanya kitu cha namna hiyo hiyo miaka miwili iliyopita, mbona aliachwa?
 
Tuwe Na tahadhari na hawa wanasiasa ambao wanaweza kutuletea matatizo kama ya Zimbabwe ya kuvamia mashamba ya wazungu. Ni Muhimu mtu mzima kama mbunge kuheshimu utawala wa sheria.
Utawala wa sheria?

Kwani wakati wanaitwa wezi ilikuwa kwa mujibu wa sheria?
 
Kinachoongelewa ni kauli zao. Kwani Heche alikwenda Mara kuwahamasisha hao wananchi? Si yuko Dodoma kwenye vikao vya bunge? Tofauti hapo ni aina ya watu, wasukuma wa huko Koromije na hao "wana-Mara" nadhani wanatofautiana ushupavu/ujasiri/uoga
Tena aswekwe kolokoloni kwa masaa kadhaa. Akili itamrudia.
 
Mbunge wa Tarime Vijijni John Heche anasakwa na Jeshi la Polisi. Heche anasakwa na jeshi hilo huku kukiwa na taarifa kwamba jeshi hilo linataka kumhoji kufuatia kauli aliyoitoa bungeni mjini Dodoma wiki iliyopita ya kuwahamasisha wananchi wa jimbo lake kulinda rasilimali zao.

Mbunge huyo wa CHADEMA, aliliambia bunge kwamba atawaongoza wananchi wa jimbo lake kuzuia Madini na rasilimali nyingine kusafirishwa nje ya nchi na Mgodi wa North Mara. Heche alikuwa anachangia hotuba ya bajeti ambapo katika mchango wake aligusia pia suala la Taarifa ya pili ya Mchanga wa dhahabu iliyoundwa na rais Dk John Pombe Magufuli.

Siku chcahe zilizopita zaidi ya wananchi 300 wanaoishi vijiji vinavyozunguka mgodi huo walivamia mgodini hapo na kufanya vurugu zilizodhibitiwa na Polisi.
Kauli aliyoitoa bungeni haihojiwi popote..
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom