Kuna kitu hakijaripotiwa. Mazishi ya wale ndugu waliouliwa na polisi yameshindikana. Wananchi wanataka RPC wa kanda maalum apelekewe miili hiyo yeye mwenyewe ajue ataizikaje. Kuzuia hili lisitokee, polisi wapo kila kona huko Tarime, na katika kujaribu kulitafutia ufumbuzi wa kidplomasia ndipo serikali ikamtuma mbunge ikidhani anaweza kuwa na ushawishi kwa wananchi. Yaliyomkuta ndiyo hayo.
Katika hatua nyingine, polisi wameahidi kutoa ulinzi kwa wanandugu watakaoamua kuchukua miili ya ndugu zao kwenda kuwahifadhi. Lakini kama tuwajuavyo wakurya, hakuna ukoo ambao mpaka sasa wamaitikia wito huo kwa kuhofia kuonekana wasaliti.