Mbunge wa Mwibara (CCM) apoteza kiti

sawa kabisa! kuna wakati tunaweza kuwa na wasiwasi na vyombo vyetu lakini mara nyingi nimekuwa nikiamini sana Mahakama Kuu na ya Rufaa katika mambo mengi kuliko mahakama nyingi za chini. Na upande mmoja ni kuwa wapo majaji na mahakimu ambao bado wanaangalia ushahidi na wanaofuata kokote utakakowapeleka.

Wewe huyo?
 
Kuna kila dalili kwamba mbunge wa Mwibara kwa tiketi ya CCM bwana Kajege atavuliwa kiti chake cha ubunge punde. Taarifa zaidi zitawajia.

Akhsante Mkuu kwa kutuletea hii ambayo ni kutoka jikoni haswa. Sikukuu njema.
 
Ofcourse JF moto!

Ila majaji wakiamua kutenda haki mabadiliko ya kweli yanawezekana, tatizo ni pale wanapo amua kupindisha sheria na kumwachia muuaji Ditto na jambazi sugu yule wa Arusha, hapo ndo wanapo tukosesha imani!
 
wako slow.. habari zinakuja JF kwanza wengine wanafuata!!! we taste the food before it is taken to the table!

Nimeanza kuona kuwa vyombo vingine vya habari vikichapisha habari kutoka JF vinaiongezea nguvu (effect) habari hiyo na kuwezesha watu wengi zaidi kuipata kuliko hapa JF ambako tuko wachache tu. Uhusiano wetu ni synergistic. Nadhani inafaa tuwe tunawashawishi waandishi wachapishe na kutangaza (broadcast) zile habari zetu ambazo tuna uhakika nazo, pamoja na maoni tunayotoa hapa, yatafika mbali zaidi.
 
wako slow.. habari zinakuja JF kwanza wengine wanafuata!!! we taste the food before it is taken to the table!

.....mmmh, and with due care and simple precautions, we make sure we won't suffer from salmonella!!

Back to topic: Jaji aliyesimamia kesi hiyo anasitahili pongezi kwa kweli, tunahitaji wengine kama yeye 7 tu nchini...!!

SteveD.
 
ndiyo maana nimesema sisi tunazionya wao wanajukumu la kuweka kachumbari, pilipili hoho, amdalasini, limau, binzari, pilipili manga na paprika! tukiwafanyia yote hayo itabidi waanze kutulipa!
 
Huyu JAJI naona anafaa kukabidhiwa faili zoote za kesi za kupinga matokeo ya ubunge, coz ndani ya Bongo kushinda kesi ya matokeo mahakamani tena ikiwa mlalamikaji mpinzani, sio mchezo babake!
Tumeona JAJI wengi hapa ukereketwa mbele sheria baadae.

Usimpe jaji credit kwa maamuzi yanayokufurahisha; kumbuka kuna pande mbili za kesi, siku zote anayeshinda hufurahi, siku akishindwa basi jaji anakuwa mla rushwa...jaji huyu huyu anaweza kutoa maamuzi mengine kesho ambayo kwa mujibu wa sheria ni sahihi ukamchukia vibaya; wapo watu kwa maamuzi haya wanataka hata kumnyonga
 
KLHNews said:
mshitakiwa alitoa vitu mbalimbali vikiwemo “kanga, vitenge, chumvi na miche ya sabuni aina ya kanga pamoja na fedha taslimu, kila mwanamke sh 500!

Huu ni utani kabisa, hii ni rushwa kama imedhibitika inabidi ashitakiwe na takukuru
 
Usimpe jaji credit kwa maamuzi yanayokufurahisha; kumbuka kuna pande mbili za kesi, siku zote anayeshinda hufurahi, siku akishindwa basi jaji anakuwa mla rushwa...jaji huyu huyu anaweza kutoa maamuzi mengine kesho ambayo kwa mujibu wa sheria ni sahihi ukamchukia vibaya; wapo watu kwa maamuzi haya wanataka hata kumnyonga

..... Sawa kabisa, Sheria ni Msumeno... au siyo ;)
 
of course, mwendapole that is the nature of the game.. refa akiamua goli lenu linakubalika mnashangilia, akimezea kuzidi kwa adui yenu akasawazisha mnaweza kumkwida.
 
Mwendapole, kinachotokea hapa ni kwamba watu wameichoka sana CCM kiasi kwamba kila jambo baya linalowapata watu hawana budi kushangilia. Ndio maana unaona hapa tunashangilia, wakati yule mbunge wa TLP kule Biharamulo yalipoenguliwa matokeo yake wengi wetu hapa tulisikitika sana tena sana. Kwa maana nyingine ni kwamba watu wengi hapa ni wanachama wa upinzani kwa kadi au bila kadi, which is very much encouraging maana watu wapo ready for change anytime the environment is ripe. Ni hivyo tu kaka.
 
Asante kaka kunielewesha. Bao kwa CCM ni shangwe kwa wapinzani na sisi wakereketwa, hata kama bao hilo haliwatoi madarakani.Cha msingi tusibweteke tukategemea kila siku bao watafungwa wao tu, iko siku tutafungwa sisi, tuwe tayari kukubali matokeo
 
Huo ndiyo ukweli kuwa kutokana na visungura vinavyotolewa kwenye kofia, unapoona ukweli na bila kiini machi inabidi ushangilie tu kwa furahi!
 
Dah, huyu bwana mdogo ameenguliwa?

Aisee, niliosoma na kijana huyu akiwa madarasa matatu nyuma yangu huko shule ya msingi na baadaye tukakutana pale Tabora akiwa pale Kazima wakati mimi namalizia form 6. Alikuwa mchezaji mzuri sana wa mpira wa miguu kwenye timu ya UMISETA. Ninaambaiwa kuwa alipewa kazi pale Mambo ya Nje kwa kuunganishiwa na wazee wa timu ya Asante Tololo mara tu baada ya kumaliza form 6 pale Azania kusudi aichezee timu hiyo. Nadhani baada ya dhahama hili, atatulia na kutafakari jambo la maana analoweza kuifanyia jamii nili kuachana na siasa za kibabaishaji namna hii zinazoweza kumchafulia jina katika jamii. Badala ya kuwa mtetezi wa ufisadi, asimame kuwa mtetezi wa maslahi ya nchi. Jambo zuri ni kwamba alitumia nafasi yake pale mambo ya nje kujiendeleza sana ki-elimu kwa hiyo ninadhani hatakosa jambo la maana la kufanya.
 
Amehukumiwa nini huyu aliyeshindwa (Mwibara) kama vile anacheza bahati nasibu?
 
ukichanganya na ukaribu wake na watoto wa mzee ruksa mambo yake yanaweza bado kuwa mswano. nasema tuu
 
Hawa jamaa wasije kucheza mchezo kwamba wapoteze Mwibara na kumuua Slaa maana CCM ya JK bwana mazingaombwe matupu .
 
Back
Top Bottom